Mwalimu aliyewahi kunyanyaswa na Mkurugenzi wa Tanga Jiji amefariki dunia

Cc mamaSamia Suluhu
 
Ukumbuke waliodhulumiwa wana watoto,afisa aliyeacha kazi kwa kunyanyasika ofisini nae ana watoto anasomesha,anategemezi nk hivyo usione kama mkurugenzi ni muhimu sana kuliko hilo kundi kubwa linaloteseka kwasababu yake
Anakikundi chake cha kutishia watu ingawaje sio mabausa kama hao wa Sabaya lakini hali sio nzuri
 
Mkuu huyo wa shule alifanya ubadhirifu wa fedha za umma bila hofu yoyote akidai hana anayemuogopa kwani anabaraka za mkurugenzi na afisa elimu wake. ,

Siku hizi wakuu wa shule wanakaa na pesa za umma? Ni pesa zipi hizo ,za elimu Bure au,hizi zinazokuja kwa kusua sua?
 
Hili nitatizo kubwa katika sehemu nyingi nchini, labda ingefaa itazamwe namna nyingine ya kudhibiti haya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Nipale kazi inapo changanywa na mapenzi ya watu ndio shida huanza.
 
Mtu kajibiwa vibaya hadi kazimia.

Inanikumbusha usemi fulani kwamba wazaramo wakimkamata mwizi hawampigi wanamsema mpaka anakufa.
🤣🤣🤣🤣🤣🤣 hii kwelii au chai mzee
 
Naamini Kuna viongozi mmojawapo atalifuatilia hili ili ukweli ujulikane na haki itendeke, duniani tunapita jamani
 
Mimi huwa namshangaa sana MTU anaedhulumiwa haki yake na kukaa kimya!?? Pesa huna ,mikwara huna sasa hata kwa babu hupajui!?? Mbona wataalamu wamejaa sana hapo Tanga maeneo ya kwa msisi!?? Yani ukifika kwa wstaalamu wanakuuliza tumfanyaje huyo msumbufu !!! Yan wewe ndio unachagua na hulipi mpaka kijibu yani!! Sasa kwann binadamu akusumbue!??
 
Huyu Gwakisa hafai kabisa Kuna dogo aliwahi kumfuata ofisini kwake kumuomba nafasi ya kujitolea mzee alimuambia"Mimi sitoi ajira hapa" Hawa baadhi ya viongozi hawafai kabisa mtu anaomba kujitolea tuu unamuambia hutoi ajira
 
 
Hawa wakuu huwa wanaangalia sura ..na msimamo wa mtu.. umekaaje Kama wakikuona unamisimamo lazma wakuite na kukusogeza vizr..ukikaa kinyonge kazini lazma unyanyasike tu.
 
Unawajua waganga wa wakurugenzi?
Wakurugenzi wana kila aina ya mganga, hata huyo afisa alieiacha ofisi usifikiri kaacha tu kwa kukerwa na mkurugenzi, hapo 'kamundu' imetumika nakwambia , kapigwa zongo lakuchukia kazi.
Mkurugenzi hawezi kuwa na jeuri kama sio mchawi wa shiriki maana subordinate wake nusu ni wachawi.
Watu wanachangia kitoto sana.
 
Kuna matumizi mabaya sana ya madaraka nchi hii.Mimi nililazimika kuacha kazi kwa sababu ya vitu kama hivi.
 
Wakuu wa Shule hupiga pesa za Captation Fund ,
Hupiga pesa za ujenzi mbalimbali unaofanyika kwenye maeneo yao.
WANAZIPIGA JE?
Nakudokezea kidogo tu.

Kwanza ,Pesa zinazokuja mashuleni zinaingizwa kwenye akaunti ya shule.Ili pesa itoke kwenye akaunti ya shule lazima kikao cha SMT kikae.UPIGAJI UNAANZIA HAPA.

Ili uwe memba wa SMT ni lazima uwe na sifa kuu moja,UWE KAMA HAUNAZO.LAZIMA UIMBE SIFA NA UTUKUFU JUU YAKE YEYE.UKIENDA KINYUME NA HAPO.BASI WEWE SI MSHIRIKA WAKE NA HIVYO UTACHUKIWA NAYE HADI HALMASHAURI UTAONEKANA WEWE NI MKOROFI NA FURSA ZOTE ZA SEMINA,HATA HAKI ZAKO KUZIPATA MAWILI UZIPATE BAADA YA KUZISOTEA SANA AU USIZIPATE KABISA.UTAZISIKIA TU REDIONI KWA WENZAKO WAKIZIPATA.

Pili,Baada ya mkuu wa Shule kuunda SMT ya ndiyo mzee.Mikutano yao hufanyika wakati mwingine haifanyiki isipokuwa katibu wa kikao ambaye huwa mtaaluma huelekezwa na mkuu wa shule aandae taarifa ya kikao kuwa kimefanyika leo na wajumbe wameridhia kutolewa kwa kiasi fulani cha fedha kwa ajili ya kazi fulani.Katibu atafuata kila mtu nyumbani kwake alimwelekeza asaini Shemu yake kwa kuwa taarifa hii ni ya muhimu sana na inatakiwa kesho asubuhi ifike halmashauri.Kumbuka sifa ya wajumbe wa SMT lazima wawe watiifu kwa mkuu wa shule kwa kila kitu.Hivyo hapa watasaini bila ya kuusoma huo muhtasari.Hapa mkuu wa shule amewini anaenda siginatory wake kwenda benki kutoa pesa.

Tatu, Wakishatoa lazima mkuu wa shule apeleke madhabahuni.( Halmashauri) Mkuu wa Idara, Kama ni suala la ujenzi basi injinia wa Wilaya lazima naye achukue kilicho chake.Ile kazi iliyokuwa inatakiwa ifanyike itafanywa chini ya kiwango.Na kwa kuwa wakaguzi ni wao basi wakija kukagua ujenzi hawatumii hata dakika tatu wanaondoka na kummwagia sifa mkuu wa shule.Hadi hapo pesa ya Serikali inakuwa imeliwa.Baada ya zoezi hili kukamilika.

Wanajitokeza waalimu ladhaa hapo ofisini wanang'amua janja janja ya namna hii kuwa pesa zinaliwa.Hao ndoa huandamwa na mkuu wa shule hadi halmashauri.Kosa dogo barua za onyo kama zote

NOTE.BODI ya Shule,Ili uwe mjumbe wa bosi ya shule kwa mujibu wa Waraka uliotolewa na Wizara zimebainisha sifa kuu mbili

Kwanza ,Awe na kuwang'oa cha Elimu kuanzia kidato cha nne kuendelea

Pili,Awe mwenye kazi halali inayomuingizia kipato.

Hapa ukija napo wakuu wa shule wamechezesha wajumbe wa bosi na kuteua wale wasio na sifa ya Elimu ya kidato cha nne ili wasiweze kuhoji maswali yaliyokwenda shule ndani ya vikao Hivyo wamewachukua hata la saba tu na zaidi ya yote ni wale wenye utii mkubwa kwake Hivyo hawana cha kumhoji .Ni kama laba stempu tu.Bodi nako kuna ukakasi.Uchunguzi ukifanyika huenda wakagundua haya.

lakini je nani amfunge paka kengele? Wakaguzi watoke nje ya Wilaya .Watoke makao makuu je wataweza kufika huko kote kwa nchi nzima?

Pili, Na tabia hii inafanyika kwenye shule za vijijini ambako wanajua hata waziri kufika huko ni muhari kwa sababu ya ama umbali mrefu na miundombinu ni mibovu.


TANBIHI , SIMAANISHI KWA SHULE ZOTE ILA BAADHI TU.NA SIMAANISHI
Naweza kusahihishwa au kurekebishwa mahali nilipokuwa.
 
Tunaomba mrejesho
Yule mkurugenzi mfujaji na zulumati mkubwa cheo nacho kimepokwa na mwenye mamlaka.
Anahaha hata haelewi maana alikua mungu mtu wa kanda ya ziwa,alijinasibu kama ndugu wa mamlaka iliyomteua.
Mamlaka ile haipo na iliyopo imempopoa mawe.
Kwakweli yeye na mademu zake baadhi wanahali ngumu
 
Kama aĺikuwa analipwa mshahara wake na anatekeleza majukumu yake vizuri, alikwenda kuomchongea mkuu wa shule ili iweje? Hizo zilizofujwa zilikuwa zake? Tulishuhudia 1.5 tilioni zinafujwa hadharani mbona hakujitokeza kumchongea mfujaji kama yeye alikuwa na machungu sana juu ya ufujaji? Kiufupi uhamisho bila malipo ilikuwa ni halali yake. NI MIMI CR WA SUA AGRIBUSINESS 2008-2011, MKARA MTIIFU NILIYEWAHI KUISHI ETHIOPIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…