Mwalimu apigwa darasani na Mwalimu mkuu baada ya kuchelewa kazini

Mwalimu apigwa darasani na Mwalimu mkuu baada ya kuchelewa kazini

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2009
Posts
16,908
Reaction score
19,123
Mwalimu mmoja katika Kaunti ya Nyamira nchini Kenya amelazwa katika hospitali ya Ikonge baada ya kushambuliwa na mwalimu mkuu kwa madai ya kuchelewa kufika shuleni.

Mwalimu huyo wa Sekondari aitwaye Vincent Onyancha amesema alifanyiwa vurugu mbele ya wanafunzi wake darasani wakati akifundisha ambapo mkuu huyo alimpiga makofi na kumpiga mateke.

“Niliwasili shuleni nikiwa nimechelewa kidogo, kisha mwalimu mkuu aliingia darasani na kunipiga nikiwa nafundisha. Alinipiga teke, makofi na kuniburuta hadi ofisini kwake ambako aliendelea kunipiga,” amesema Onyancha.

Maafisa wa Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari (KUPPET) wamelaani tukio hilo na kuitaka Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwalimu mkuu huyo.

Chama hicho kimeongeza kuwa iwapo hatua za kisheria hazitachukuliwa dhidi ya mwalimu mkuu huyo, walimu watalazimika kugoma ili kulalamikia ukatili huo.

Mkurugenzi wa TSC katika Kaunti ya Nyamira, Erick Magak, amethibitisha kupokea malalamiko hayo na kusema kuwa uchunguzi umekwishaanza.

Screenshot_20250226_162952_Gallery.jpg
 
Duuh hatari sana, ila wakenya 🙌🏽
Hata waTz yapo sema watu hawayaripoti tu.

Hata mimi niliwahi wafanyia staff wangu washenzi na ikawa ni siri.

Fikiria staff mwizi ama mtoro sugu unamfanyaje?

Ukimfukuza, umeangamiza familia nzima.

Unamwita ofisini achague anachoona kina maslahi kwake, dismisal au nimburuze mboko alafu tupotezee yaishe?

Issue siifanyii hadharani, namuita ofisini tunabagain.
 
Mwalimu mmoja katika Kaunti ya Nyamira nchini Kenya amelazwa katika hospitali ya Ikonge baada ya kushambuliwa na mwalimu mkuu kwa madai ya kuchelewa kufika shuleni.

Mwalimu huyo wa Sekondari aitwaye Vincent Onyancha amesema alifanyiwa vurugu mbele ya wanafunzi wake darasani wakati akifundisha ambapo mkuu huyo alimpiga makofi na kumpiga mateke.

“Niliwasili shuleni nikiwa nimechelewa kidogo, kisha mwalimu mkuu aliingia darasani na kunipiga nikiwa nafundisha. Alinipiga teke, makofi na kuniburuta hadi ofisini kwake ambako aliendelea kunipiga,” amesema Onyancha.

Maafisa wa Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari (KUPPET) wamelaani tukio hilo na kuitaka Tume ya Huduma kwa Walimu (TSC) kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwalimu mkuu huyo.

Chama hicho kimeongeza kuwa iwapo hatua za kisheria hazitachukuliwa dhidi ya mwalimu mkuu huyo, walimu watalazimika kugoma ili kulalamikia ukatili huo.

Mkurugenzi wa TSC katika Kaunti ya Nyamira, Erick Magak, amethibitisha kupokea malalamiko hayo na kusema kuwa uchunguzi umekwishaanza.

View attachment 3250515
uchunguzi tena wakati alichapwa mbele ya wanafunzi zaidi ya 50
 
Mwanaume mwenzio anakupiga vipi kizembe tena ndani ya darasa kisa cheo/kazi?

Mie ningerusha hata madawati
Mkuu unapigwa na unashukuru kwamba yameisha na maisha yasonge.

Sema huyo mkuu wa shule kapiga kipumbaf, katengeneza kesi hiyo.

Mi kuna mtu aliwahi toroka kazi kwa muda wa miezi 6.

Aliposikia sijaunda board kwa ajili ya kumfuta akatumia mbinu ya Lipumba, akajirudisha mwenyewe.

Ile kumuona akanijaza ghadhabu, maana alinikuta naandaa bord na sikuwa na wasi wasi kama anaweza kufanya timing ya hivyo.

Nilipomuita kumhoji sababu zilizomfanya akahuni kazi, majibu yake eti wanamazingaombwe wenzake walimchezea akajishitukia anasahau kazi, akaniomba nimsamehe.

Nikamwambia achague option mbili tu, nimjazie fomu za kuachishwa kazi au nimlambe hamsa ushirini tuiue soo, nikampa dk10 anipe majibu.

Akanipa jibu kwamba nimpige ili yaishe.

Nikamwambia:'siyo nikutandike hapa nikute yamezagaa kwa staff nzima, sitaki, nikakata mkwaju, 'haya bwana lala, na ukishika kupoza tunafuta', tukawa tumeelewana hivyo.

Nikawa nimempima na ubavu wake kwamba hata ajae upepo hawezi kunifanya kitu, buruza mboko hadi kojo.

Na wengine staff wezi, ulipopatikana ushahidi wa kuwatia hatiani, nikawaita kubagain nini chaguo lao sahihi, jela au mboko ili yaishe.

Wakachagua mboko kwa madai kwamba 'zimwi likujualo...'.

Piga yangu sasa ni ile ya kuua mwizi ni kufuru.
 
Back
Top Bottom