Mwalimu asimamishwa kazi kwa kumtukana Rais Samia

Mwalimu asimamishwa kazi kwa kumtukana Rais Samia

DeepPond

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2017
Posts
41,728
Reaction score
103,997
By Pascal Mwakyoma TZA

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Momba, Shela Mwangoka amesimamishwa kazi na Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde kwa kudaiwa kumtusi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika kadamnasi ya watu kwa dhihaka kwa lugha zisizofaa kwa Rais.

Hayo yamebainika baada ya mkutano wa shina kati ya wananchi wa Kijiji cha Washo Kata ya Myunga Wilaya ya Momba Emily Skanyika na Jacob Miyala ambao walitoa kero yao kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa CCM Shaka Hamdu Shaka kuwa mwalimu huyo amekua akitoa lugha za matusi mara kwa mara hali ambayo inawachafua wananchi hao kuona Rais wao anatukanwa.

Kwa upande wake Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde amesema amefanya uchunguzi mdogo baada ya kusikia malalamiko hayo kujiridhisha na kugundua kuwa ni tabia ya Mwalimu huyo kufanya hivyo na mara ya mwisho ni wiki moja iliyopita akiwa sokoni alipoona Rais Samia kaongeza madaraja na mishahara kwa watumishi wa umma akasema ni hongo ili amuunge mkono akasema hawezi muunga mkono sababu ni mwanamke.

Credit: Millard Ayo, Jul 10, 2021
 
Sasa wanaona kazi ya ualimu ni bonge la kazi mpaka wamfukuze Hugo mwalimu mwenye stress ya kutokuongezewa mshahara kwa miaka 6 ya yule sanamu
Ili aendelee kupata teuzi,jinga Sana hili

2479786_20200720_200050.jpg
 
Ndio kazi pekee wanayo iweza..ila shughulikia matatizo ya wananchi ambao ndio wamewatuma hawewezi..kweli chama chakavu kimekosa ubunifu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
In a real situation mawaziri hawana mamlaka ya suspend au kusack mtuMoshi yeyote wavserikali. Ni katibu mkuu Utumishi tu au mfanyakazi mwingine ambaye katibu mkuu amedelegate hizo powers. Wengine wote wana weza kupendekeza tu kaw huyo kwenye mamlaka. waziri Hana mamlaka maana siyo mwajiri. Mawaziri wetu wana akili ya bata ndiyo maana wanafanya hivyo. Yes, mwalimu Ana makosa, huyo mwalimu mkuu yuko wapi kumripoti. Kuna DAS, RAS? Wote ho wana mamlaka waliyopewa na Karibu mkuu. Means siasa Hana mamlaka, Hana powers za kuajiri.
 
Back
Top Bottom