By Pascal Mwakyoma TZA
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Momba, Shela Mwangoka amesimamishwa kazi na Naibu Waziri wa TAMISEMI David Silinde kwa kudaiwa kumtusi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika kadamnasi ya watu kwa dhihaka kwa lugha zisizofaa kwa Rais.
Hayo yamebainika baada ya mkutano wa shina kati ya wananchi wa Kijiji cha Washo Kata ya Myunga Wilaya ya Momba Emily Skanyika na Jacob Miyala ambao walitoa kero yao kwa Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa CCM Shaka Hamdu Shaka kuwa mwalimu huyo amekua akitoa lugha za matusi mara kwa mara hali ambayo inawachafua wananchi hao kuona Rais wao anatukanwa.
Kwa upande wake Naibu waziri wa TAMISEMI David Silinde amesema amefanya uchunguzi mdogo baada ya kusikia malalamiko hayo kujiridhisha na kugundua kua ni tabia ya Mwalimu huyo kufanya hivyo na mara ya mwisho ni wiki moja iliyopita akiwa sokoni alipoona Rais Samia kaongeza madaraja na mishahara kwa watumishi wa umma akasema ni hongo ili amuunge mkono akasema hawezi muunga mkono sababu ni mwanamke.
Credit: Millard Ayo, Jul 10, 2021
Huyu naibu waziri ni mpumbavu, na ndo hao watafuta sifa KWa uongonzi wasiostahili, kujipendekeza Kama yale ya mwendazake , kwani mtumishi wa umma Hana mawazo yake mbadala?
Aliniambia mzee wangu siku moja nikiwa tanga mwaka mmoja,
Kwamba wakati wa Mchakato wa Vyama vingi yeye akiwa ameamia kiwanda Cha mkonge akitoake fire Dar ,KWa mshahara wa 350 tsh TOKA tsh 300, yalipita maoni KWa wafanyakazi wa umma akiwemo yeye ,akakubali kwenye form ya maandishi kwamba anaunga Vyama vingi basi,anakwambia kila siku wanausalama walikua hawapungui kwake,(KWA kujipendekeza KWA Mwalim ) na walipata haibu ya mwaka baada ya mwl ruhusu vyama vya siasa ,
So SILINDE NI MNAFIKI Rais asisemwe kwani ndo Mungu wa Tanzania shame at you Silinde, na je amejuaje kwamba Mwl alicho kisema hata Rais hakioni sawa?
Eti kafanya uchunguzi ,yeye Kama nani fanya uchunguzi, vyombo vya uchunguzi si vipo , ngoja nifuatilie hii kitu , bado Niko maskini ila uonevu spendi, ,Hawa lazima kupigwa maombi watenguke viuno,wasife ili adabu iwakae,
Una msimamisha mtu KWa Mambo ya kijinga na upumbavu, familia yake anailisha yeye,? Na li v8 lake mjinga Sana, sifa za teuzi zitawaua Kama sio kuwatokea puani ,wait and see