Mwalimu auwawa Itilima baada ya kuua mwanafunzi

Mwalimu auwawa Itilima baada ya kuua mwanafunzi

nyilaegenge

Senior Member
Joined
Apr 13, 2014
Posts
198
Reaction score
105
Mwalimu mmoja ajira mpya ameuwawa kikatili na wananchi wenye hasira baada ya kusababisha kifo cha mwanafunzi wake.

Mwalimu huyo alikuwa anafundisha Shule ya Sekondari Chinamili iliyopo wilaya ya Itilima mkoa mpya wa Simiyu.

Mwalimu alikuwa anamwadhibu mwanafunzi kwa viboko lkn bahat mbaya akapoteza maisha.

Mungu awapumzishe kwa amani!
 
Duh hizi kazi nazo full risk,mimi nawashauri waalimu acheni hizi adhabu za viboko maana afya za watu zimekua mbovu mno.
R.I.P both of them.
 
high risk with low return,kazi nyingine kweli majanga tu
 
:llama:duuu! hii ni hatari, sidhan kama kweli fimbo ndo imemtoa uhai huyo mtoto
 
r.i.p wote. walimu nawashauri waache kuchapa watoto wa siku hizi maana magonjwa ni mengi huwezi kujua labda mtoto alikuwa na tatizo la kiafya maskini
 
Jf ina sifa ya kutaja majina ya wahusika,yapo wap hayo majina?au ni story tu
 
Watoto Wa siku hizi bwana wako delicate sana! Viboko tu mpaka unakata roho? Labda kama umepigwa kichwani! Enzi zetu unanyeshewa viboko ulikuwa na ujasiri wa kuvihesabu mpaka unapoteza hesabu maana unaanza 1,2,3,4.......50............70.......baadaye steam inakata unapoteza mahesabu lakini ukitoka hapo mwendo mdundo tu!!! Nakumbuka nilikamatwa na second master nimetoroka school Baraza nikaenda town niliburuzwa fimbo sina hamu! Sijui second Kikome yuko wapi siku hizi?

R.I.P wote, mwanafunzi afya mgogoro na mwalimu katiri!
 
Huwa naskia kuwa wanafunzi hasa wa kike na hasa wa vijijini wana tabia ya kuweka Vitunguu, na vitu vingine mbalimbali makwapani mwao. Hii tutokea pale Mwanafunzi anapokuwa na kosa kama uchelewaji na kweli inasadikika kuwa awekapo huyo mwanafunzi na mwl akamwadhibu kwa viboko mwanafunzi huweza kuzimia kwa muda. Tukio hili huokolewa na Wanafunzi wenzie ambao huwa wamepanga nao njama, hivyo huvitoa baadae e.g. baada ya dk 15 au 30 hivi. Na hivyo mhusika kurudia hali yake ya awali. Iwapo ataweka bila kuwasitua wenzao anaweza kupoteza maisha.
Hii hufanyiwa hasa kwa walimu wawaitao "WANONKO".
Huwa naskia tu ila sina uhakika
 
mwlalimu mmoja ajira mpya amepigwa kikatili na wananchi wenye hasira baada ya kusababisha kifo cha mwanafunzi wake... mwlalimu huyo alikuwa anafundisha shule ya sec chinamili iliyopo wilaya ya itilima mkoa mpya wa simiyu...

mwlalimu alikuwa anamwadhibu mwanafunz kwa viboko lkn bahat mbaya akapoteza maisha...Mungu awapumzishe kwa amani


Hii nchi kila mtu ana stress, mwalimu, mwanafunzi, askari, etc mpaka rais nafikiri.

Kuna kila dalili za hizi stress kutokutatuliwa hata na recent 'discovery' of resources na badala yake zinaonekana kuwa amplified.
 
Kizazi cha vidonge na sindano kitaja chapwa na maisha huku duniani. Bakora ni mzigo tu....!!
 
Du hii ishakuwa balaa. So auaye kwa upanga atauwa kwa upanha pia. Lakini mbo hii haingii akilini kuchapwa mpaka kufa. Palw Mbeya day kuna mwl.enzi hizo alikuwa anaitwa mwakasala aka Nangalufu anachapa wanafunzi wote wa shule Nzima kama 400 viboko vinne vinne kila mwanfunzi. Vikiwemo viboko vya kichwani lakini hakuna aliyekuwa anaanguka hata mmoja
 
Back
Top Bottom