Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Inamhitaji mtu roho ya; urafiki, ulezi, ushauri, uzazi, ukaribu na upendo ili kumtengeneza MWANAFUNZI bora. Sifa hizi ni za ndani, ukitoa zile za nje ambazo walimu hufunzwa vyuoni na kufanya walimu wote waishi katika mstari mmoja.
Sifa za nje ni kama haiba na maadili, uwezo wa kutawala darasa na majadiliano yote ya kitaaluma, sambamba na kumjengea MWANAFUNZI uwezo wa kujieleza ndani na nje ya chumba cha mtihani au ndani na nje ya mazingira ya shule.
Kuna aina mbili za wanafunzi ambao huibuka wakikutana na mwalimu bora. Kundi la kwanza ni wanafunzi ambao wanataka kuwa bora kama mwalimu wao na kundi la pili wana tamaa hii pia ya kuja kuwa bora kama mwalimu wao, utofauti uko wapi?
Kundi la kwanza huongozwa na husuda (ENVY) wakati kundi la pili huongozwa na msukumo chanya (INSPIRATION)
Kundi la kwanza hupambana sana ili kumzidi uwezo mwalimu wao bora (outsmarting or outclassing or outshining the master) na kutaka kuongelewa wao.
Hawa wakishindwa kufikia azma yao, huanza kumchukia mwalimu wao na kuanza kuhisi pengine ametumia nguvu za giza kufika hapo huku wengine wakihisi watu wanampendelea ila mwalimu huyo hana ubora wowote. Wanasahau kuwa walipambana sana ili kufika alipofika baada ya kuukubali uwezo au ubora wake.
Chuki hupofusha ila upendo huona kwa uoni sahihi (Hate blinds but love has a right vision)
Kundi la pili hunyenyekea na hujifunza kupita kwenye njia alizopita mwalimu wao bora na hawa hawashindani naye bali huendelea kumwona mwalimu wao kama kioo chao.
These people are really inspired by their mentors na wanafurahia kila mwalimu wao anapopiga hatua mpya ili nao waendelee kujifunza.
Hawa hata wakipiga hatua na kumzidi mwalimu wao kwa ubora, bado wakiulizwa aliyefanikisha kufika walipo humtaja mwalimu wao huyo.
Anayekupenda anaweza akajificha lakini asiyekupenda hawezi kamwe kujificha. Atakuonesha tu. Asipokuonesha kwa kauli kavu atatumia utani kufikisha chuki yake kwako.
ARE YOU ENVIOUS OR INSPIRED BY YOUR TEACHER?