Mwalimu gani mkali ushawahi kukutana nae katika maisha yako ya shule...!!!??

Mwalimu gani mkali ushawahi kukutana nae katika maisha yako ya shule...!!!??

Mwalimu MJ kwa wale waliosoma shule za msingi manispaa ya temeke,jamaa alkuw noma balaa
 
Nilipokuwa Tambaza alikuwepo H/M Karumuna(Father K), huyu mzee alikuwa noma.RIP
. Nilipokuwa Tosamaganga nilimkuta H/M anaitwa Dudu. Huyu alikuwa anakuchapa fimbo+constant (constant=,fimbo 6)
. Alikuwepo pia mwalimu Soldier. Huyu usiposafisha meza d/h halafu yupo zamu anasafisha yeye, sasa subiri muziki wake akikupata

Kalumuna akicheka siku hiyo tegemea kuokota sh 10000!
 
Mwalimu lufyagile,mdaburo secondary,Mwalimu kinyonga mwaka shule ya msingi
 
Walimu wa dot com hawachapi sijui tuandike nini
 
Primary 96' nilihamia shule moja hv Mtwara inaitwa Ligula.....hapo unakutana na kitu kinaitwa Mwl. Mayere....alikuwa mwl mkuu halafu Mwl wa somo la hisabati vilevile.
Mwalimu alikuwa anatandika fimbo yule sijampatia mwenzake.
Alikuwa akikatiza mtaani hata siku za jumamosi tunaingiaje kwenye vichaka vya uppupu kujificha.
Mwaka 2010 nilikutana nae Kariakoo....kwa kiwewe niliingia dukani kujificha...nikaja kukumbuka kumbe nilishamaliza shule miaka tisa iliyopita....nikatoka dukani kifua mbele kwenda kumsalimia.
Nilivyofika kwangu....nilijicheka sana.

Secondary Mtwara Girls kulikuwa na kitu kinaitwa Mwl. Ngwadakulima a.k.a Mwl. Ngwada wa somo la Biology.
Alikuwa anacharaza bakora sijapata kuona.
Unalala juu ya meza kule laboratory room....unashika bomba afu unachezea mikwaju ole ujifute....aisee.
Mwaka 2011 nikasikia tetesi amefariki....nilisafiri mpaka Mtwara ili nikahakikishe....kufika kule nikakuta si kweli japo anaumwa sana.
Tuliosoma zamani...tumechezea sana mkong'oto.
 
Ebwana 2005 hv shule ya Bwiruboyz tech panamwalim huyo alikuwa anaitwa Mchiz Mox alikuwa anapiga fimbo mpaka mtu unapoteza network,nashukuuru kuskia madogo walikuja anzisha mgomo miaka ya 2008 wakamtoa yy na HM Mr Kisuuu
 
1.Mwl. Ngandu primary school-msasani
2.Afande Mwamasika - Air Wing banana
3.Afande Miraji -Makongo
4.Mwalim Sharifh -kinondoni
Wengine hapo washatangulia -R.I.P
 
Benard Ngozye-H/M Azania Boys. Huyu mbwa anachapa fimbo 6! Kosa lolote lile hata kama hujavaa tai!
 
Back
Top Bottom