tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Nimeshangaa jinsi suala la Katibu Mkuu wa CWT mwalimu Japhet Maganga linavyofanyiwa siasa badala ya kuchukuliwa kama suala la kiutumishi. Kwanza sio jambo la kawaida mtumishi wa umma kufukuzwa kazi kwa mujibu sheria na jambo hilo kugeuzwa kuwa suala la umma.
Mwalimu Maganga kateuliwa kuwa DC amegoma kwenda kuapishwa. Ameomba aongezewe kibali cha kuendelea kutumikia CWT, serikali imegoma kumuongezea muda licha ya kwamba siku za nyuma serikali imekuwa ikimuongezea muda bila tatizo lolote. Kana kwamba hilo halitoshi, barua ya kukataliwa kuongezewa muda imewekwa kwenye public domain na pia barua ya kuombwa kurudi kazini imekuwa public.
Nimebaki najiuliza: ni watumishi wangapi wamefukuzwa kimyakimya bila serikali kuutangaziia umma? Kwanini hili suala binasi linageuzwa kuwa la umma? Je, serikali hawaoni kuwa tayari wamevunja sheria kwa kuingilia faragha ya mwalimu Maganga kuhusu masuala ya kazi na kwamba anaweza kuwashtaki mahakamani wakamlipa mabilioni ya shilingi kwa kumchafua na kudhalilisha utu wake hadharani?
Mtu kukataa kuwa chawa ni utashi wake binafsi. Maganga aliona future yake haipo kwenye siasa ndio maana akaamua kugomea nafasi ya uteuzi. Kukataa uteuzi ndio iwe nongwa kiasi hiki? Acha hizo bhana. Serikali inajidhalilisha sana kwa kuendelea kukomalia jambo hili bila kufuata sheria.
Sheria za kazi zipo wazi. Mtu alitakiwa kuripoti kazini tarehe 1 lakini hadi leo tarehe 18 hajafanya hivyo na bado serikali inaweweseka mitandaoni kumtaja kama ni mtumishi wa umma wa Manispaa ya Temeke. Sheria inasema mtumishi asiporipoti kazi kwa siku 3 mfululizo bila sababu wala ruhusa kutoka kwa mwajiri anakuwa amejifuta kazi mwenyewe. Inakuwaje maganga anakuwa nje ya kituo cha kazi kwa siku 18 bado serikali inahangaika naye? Au mtu akiteuliwa kuwa DC akagoma sheria za kazi kwake zinatumika tofauti na watumishi wengine? Maswali ni mengi kuliko majibu.
Ukifikiria kwa undani utagundua nia ya serikali kuwateua viongozi wakuu wa CWT kuwa wakuu wa wilaya haikuwa bahati mbaya. Watakuwa walifanya hivyo kwa nia ovu baada ya kuona hawa viongozi labda wamekuwa vikwazo kwao kujipenyeza CWT kuchota mapesa kwa ajili ya kujipanga na uchaguzi mkuu 2025 na mambo mengine ndani ya chama. Ndipo Maganga na wenzake wakashtukia ishu na kugoma. Baada ya kugoma kuondoka kupisha mwanya wa uchotaji wa hela, serikali imeamua kumkomesha kwa kutomuongezea muda wa kuendelea kubaki CWT. Hii ndio kete ya mwisho kwa serikali kupata nafasi kuingia CWT kujichotea mapesa ya bwerere.
Kwa hali ilivyo, serikali watakuwa wanatafuta sababu ya kumkomoa Maganga kwa kuwa amekuwa kikwazo kwao kutimiza jambo lao. Na huenda kuna mahali serikali imejichanganya, hivyo Maganga anasubiri wamfukuze kazi halafu awashike pumb* washindwe kuchomoa. Bila shaka atakuwa anasubiri wautangazie umma kuwa wamemfuta kazi kisha akimbilie mahakamani kuwakamua mamilioni ya fidia. Usidhani yeye ni bwege agome kwenda kazini tangu tarehe 1 hadi leo terehe 18 lakini bado serikali inaweweseka kutafuta huruma mitandaoni.
Kuna shida mahali sio bure. Let us wait and see what gona happen.