Mwalimu Japhet Maganga wa CWT hafukuziki? Jibu hili hapa

Mwalimu Japhet Maganga wa CWT hafukuziki? Jibu hili hapa

Nimeshangaa jinsi suala la Katibu Mkuu wa CWT mwalimu Japhet Maganga linavyofanyiwa siasa badala ya kuchukuliwa kama suala la kiutumishi. Kwanza sio jambo la kawaida mtumishi wa umma kufukuzwa kazi kwa mujibu sheria na jambo hilo kugeuzwa kuwa suala la umma.

Mwalimu Maganga kateuliwa kuwa DC amegoma kwenda kuapishwa. Ameomba aongezewe kibali cha kuendelea kutumikia CWT, serikali imegoma kumuongezea muda licha ya kwamba siku za nyuma serikali imekuwa ikimuongezea muda bila tatizo lolote. Kana kwamba hilo halitoshi, barua ya kukataliwa kuongezew muda imewekwa kwenye public domain na pia barua ya kuombwa kurudi kazini imekuwa public.

Nimebaki najiuliza: ni watumishi wangapi wamefukuzwa kimyakimya bila serikali kuutangaziia umma? Kwanini hili suala binasi linageuzwa kuwa la umma? Je, serikali hawaoni kuwa tayari wamevunja sheria kwa kuingilia faragha ya mwalimu Maganga kuhusu masuala ya kazi na kwamba anaweza kuwashtaki mahakamani wakamlipa mabilioni ya shilingi kwa kumchafua na kudhalilisha utu wake hadharani?
View attachment 2785979
Mtu kukataa kuwa chawa ni utashi wake binafsi. Maganga aliona future yake haipo kwenye siasa ndio maana akaamua kugomea nafasi ya uteuzi. Kukataa uteuzi ndio iwe nongwa kiasi hiki? Acha hizo bhana. Serikali inajidhalilisha sana kwa kuendelea kukomalia jambo hili bila kufuata sheria.

Sheria za kazi zipo wazi. Mtu alitakiwa kuripoti kazini tarehe 1 lakini hadi leo tarehe 18 hajafanya hivyo na bado serikali inaweweseka mitandaoni kumtaja kama ni mtumishi wa umma wa Manispaa ya Temeke. Sheria inasema mtumishi asiporipoti kazi kwa siku 3 mfululizo bila sababu wala ruhusa kutoka kwa mwajiri anakuwa amejifuta kazi mwenyewe. Inakuwaje maganga anakuwa nje ya kituo cha kazi kwa siku 18 bado serikali inahangaika naye? Au mtu akiteuliwa kuwa DC akagoma sheria za kazi kwake zinatumika tofauti na watumishi wengine? Maswali ni mengi kuliko majibu.

Ukifikiria kwa undani utagundua nia ya serikali kuwateua viongozi wakuu wa CWT kuwa wakuu wa wilaya haikuwa bahati mbaya. Watakuwa walifanya hivyo kwa nia ovu baada ya kuona hawa viongozi labda wamekuwa vikwazo kwao kujipenyeza CWT kuchota mapesa kwa ajili ya kujipanga na uchaguzi mkuu 2025 na mambo mengine ndani ya chama. Ndipo Maganga na wenzake wakashtukia ishu na kugoma. Baada ya kugoma kuondoka kupisha mwanya wa uchotaji wa hela, serikali imeamua kumkomesha kwa kutomuongezea muda wa kuendelea kubaki CWT. Hii ndio kete ya mwisho kwa serikali kupata nafasi kuingia CWT kujichotea mapesa ya bwerere.

Kwa hali ilivyo, serikali watakuwa wanatafuta sababu ya kumkomoa Maganga kwa kuwa amekuwa kikwazo kwao kutimiza kutimiza jambo lao. Na huenda kuna mahali serikali imejichanganya, hivyo Maganga anasubiri wamfukuze kazi halafu awashike pumb* washindwe kuchomoa. Bila shaka atakuwa anasubiri wautangazie umma kuwa wamemfuta kazi kisha akimbilie mahakamani kuwakamua mamilioni ya fidia. Usidhani yeye ni bwege agome kwenda kazini tangu tarehe 1 hadi leo terehe 18 lakini bado serikali inaweweseka kutafuta huruma mitandaoni.

Kuna shida mahali sio bure. Let us wait and see what gona happen.
Drama hii
 
Drama hii
Watajua wenyewe. Kipindi wanamuongezea muda abaki CWT walikuwa wanafanya hivyo kimya kimya. Baada ya kugomea nafasi ya uteuzi ndipo sasa wanakuja hapa kulialia kutafuta public sympathy. CCM ni majitu ya ajabu sana.
 
Ukiwa mwizi au kibaka, siku ukitiwa kati na wananchi wenye hasira kali unatakiwa kuchutama lakini sio kwa CCM. Wezi hawa wameshtukiwa na Maganga kutaka kuiba hela za CWT lakini hawataki kuchutama. Badala yake wanamuandama na kumsakama mwalimu Maganga kutaka kumkomoa kwa kuwakatalia kuiba hela za wanachama wa CWT. Haya majitu hayana khaya hata kidogo.
 
Majuzi walitangaza hali yake si shwari, ni kama akili yake imeathirika
CCM ni majitu ya ajabu sana. Yaani huyu jamaa ni jasiri mno kupambana na kiijiji kizima cha CCM wakiwa wamembebea mawe. Walitangaza redioni au mitandaoni mkuu?
 
CCM ni majitu ya ajabu sana. Yaani huyu jamaa ni jasiri mno kupambana na kiijiji kizima cha CCM wakiwa wamembebea mawe. Walitangaza redioni au mitandaoni mkuu?
Humu jamvini
 
Fungua uzi kabisa "Aliyepigwa mawe na wanaccm Dodoma"
Asante mkuu. Nashukuru nimeupata uzi. Huu uzi uliandikwa 2020 sijui sasa hivi huyu kamanda atakuwa na hali gani:
 
Asante mkuu. Nashukuru nimeupata uzi. Huu uzi uliandikwa 2020 sijui sasa hivi huyu kamanda atakuwa na hali gani:
🙏👍
 
Toka lini mtumishi anachagua aina ya kazi ktk field aliyoajiriwa??

CWT ni ya waalimu,mwalimu yeyote anawezafanya kazi CWT kwa kuteuliwa na anaweza kutenguliwa pia.
Kwa sababu anajua sio haki yake ya milele ndio sababu ALIOMBA kuendelea,sio kugomea kutoka,sasa watu kwanini washangae ombi lake kukataliwa!!!!
Ni ujinga mtupu kujiona miungu watu kumkatalia mtu maombi kwa sababu za kisiasa. Kwasababu zile zile walizo mruhusu ,mwanzo wamruhusu sasa. Kama hawana sababu ya kumzuia kuendelea kuwa huko CWT, Ndiyo aliomba na wakamruhusu, na akaomba tena na tena sasa leo kumetokea nini hadi wasimruhusu. Leo ndio wameona umuhimu wake au leo ndio wamekumbuka anatakiwa kufundisha?
CCM na Setrikali ya Ki ccm ni wapumbavu sana.
 
Ni ujinga mtupu kujiona miungu watu kumkatalia mtu maombi kwa sababu za kisiasa. Kwasababu zile zile walizo mruhusu ,mwanzo wamruhusu sasa. Kama hawana sababu ya kumzuia kuendelea kuwa huko CWT, Ndiyo aliomba na wakamruhusu, na akaomba tena na tena sasa leo kumetokea nini hadi wasimruhusu. Leo ndio wameona umuhimu wake au leo ndio wamekumbuka anatakiwa kufundisha?
CCM na Setrikali ya Ki ccm ni wapumbavu sana.

CWT kiko chini ya CCM,hao waliotaka sasa atoke akaitumikie CCM hiyo hiyo kwenye UDC.

Kama ameamua kukataa ofa ya pili anajivua sifa ya kuendelea na ofa ya kwanza,hana anachomiliki hapo zaidi ya huo ualimu ambao nao kaamua kuunyea kwa kuona hauna maslahi tena kwake.
Watamfilimba,watu wenyewe ndio hawa akina makonda na bananga!!!!!
 
Kwa Maokoto hayo unamfukuzaje. Waalimu acheni hela zenu zipigwe mtapewa T shirt siku ya Maadhimisho ya Mwalimu Duniani
 

Attachments

  • IMG-20231129-WA0000.jpg
    IMG-20231129-WA0000.jpg
    97.1 KB · Views: 4
Kwa Maokoto hayo unamfukuzaje. Waalimu acheni hela zenu zipigwe mtapewa T shirt siku ya Maadhimisho ya Mwalimu Duniani
Du! Kweli huu mfuko unaliwa sana na viongozi huku walimu wakiwa wamekaa kimya kama makondoo. Inauma na inahudhunisha sana.
 
Back
Top Bottom