Mwalimu Japhet Maganga wa CWT hafukuziki? Jibu hili hapa

Mwalimu Japhet Maganga wa CWT hafukuziki? Jibu hili hapa

Tumeambiwa aliomba kibali Utumishi,sasa mm na ww tujiulize Hv kibali huwa hakiishi ,mm naamini kibali kinaisha kulingana na muda uliopewa.JANETH hakuajiriwa CWT,waliomuajiri ndio walimpa kibali pale alipoomba kutumikia CWT,Kumbuka mwajiri mkuu ni serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania na CWT sio mwajiri na kuigomea serikali iliyokupa kibali kwenda huko uliko ni kosa lingine,kama kibali kimeisha muda wake basi turudi tulipotokea ndio busara kuliko kuwa na kiburi kisicho na maana.Angeenda kutumikia CWT bila kibali kutoka Ofisi ya Utumishi kwa muda wote ambao amekuwa huko,ningewashangaa sana Utumishi kumtaka arudi kule alikokuwa ilhali hawakumuandikia kibali.Ni vema tukazingatia taratibu za Utumishi na tusi sikilize bush loyals ambao mwisho wa siku hawana cha kutusaidia.
Sasa kisha onyesha nia yake ni kubaki kule cWT mumuache aende, tatizo la watu kama wewe mnadhani roho mbaya ni sifa. Yeye hataki kurejea Temeke anataka kubaki CWT, kwanini msimwache afanye anachotaka? kwanini kulazimishana? mwajiri mkuu, mwajiri mkuu kwani serikali ni Mungu? Tumieni busara na hekima mumuache akafanye apendacho, mkimlazimisha mnapata nini?
 
Sasa kisha onyesha nia yake ni kubaki kule cWT mumuache aende, tatizo la watu kama wewe mnadhani roho mbaya ni sifa. Yeye hataki kurejea Temeke anataka kubaki CWT, kwanini msimwache afanye anachotaka? kwanini kulazimishana? mwajiri mkuu, mwajiri mkuu kwani serikali ni Mungu? Tumieni busara na hekima mumuache akafanye apendacho, mkimlazimisha mnapata nini?
Arudi Temeke tu kwa sababu hakusomea ukatibu mkuu alisomea ualimu.
 
Let's assume kwamba huyo Maganga amezuia serikali isichote pesa huko Cwt kwa maelezo yako.Je hizo hela za walimu zimekuwa safe kiasi gani na lini ? Mbona bado kuna malalamiko kibao kwamba huko Cwt hela za walimu zinatafunwa ovyo ni kama hazina mwenyewe na ripoti ya CAG ya mwaka 2017/2018 ilithibitisha hivyo na mwaka huo huyo Maganga alikuwa kiongozi huko Cwt .Niombe mama Samia akiona inafaa atume tena CAG aone ni kwa namna gani hela za walimu wetu zinakuwa monitored tangu ukaguzi wa mwisho enzi za Magu
Hata hela za serikalini zinaliwa hovyo hilo pia ujue
 
Nimeona hata Jamii Forum wameandika habari hii kishabiki ,Jamii Forum ni chombo cha kutetea wananchi ,nilitegemea viongozi wa jamii Forum chini ya mtu bingwa @maxmello wangekua mstari wa mbele kuwa katika jukwaa la utetezi wa viongozi wa vyama vya Wafanyakazi kwa kusoma sheria ya kazi na mahusiano kazini ,pamoja na kusoma mkataba namba 87 wa ILO na Mkataba namba 98

Lakini wameandika taarifa kama gazeti la Nipashe ambalo limenunuliwa na kundi lililokua na mirija CWT sasa imekatwa,sitaki kusema kuwa JF nayo itakua imewekwa mfukoni baadhi ya watendaji wake .ndio maana hawataki kuchimba ukweli

Mbona Dr Mhina aliekua Mkurugenzi serikali za Mitaa pale TAMISEMI aliteuliwa kuwa DC ,akwenda na haikuandikwa kuwa ni mgomo kwa Rais ..
Jamiiforum ni hela yako tu ukitaka kumchafua mtu mwaga hela kwa viongozi wa JF utamchafua mpaka uchoke na ukitaka usichafuliwe fanya ivoivo
 
Sheria ya ajira na mahusiano kazini namba 7 ya mwaka 2004 inapiga marufuku kukata mshahara wa mtumishi pasipo ridhaa ya mwajiriwa anayoitoa kwa mwajiri wake kwa kujaza fomu iitwayo Tuf 15 na kutuma maombi ya kujiunga kwenye chama cha wafanyakazi. Ila kwa bahati mbaya siwitiii wakishirikiana na maafisa utumishi kwa makusudi wameamua kwa makusudi kuikanyaga sheria halali kwakuingiza makato kwenye check number za walimu pasipo indorsement za wenye mishahara hasa kwa walimu walioanza kazi kuanzia mwaka 2015 kurudi nyuma .Hivi hao Cwt kiburi cha kudharau sheria hiyo halali ya nchi mpaka sasa watendaji wake wamediriki mpaka kukataa teuzi toka kwa mh Rais wanakipata wapi?
Na hata kama kaingia kwa hiari bado anayo haki ya kujitoa muda wowote.......ndo maana jamaa kakataa teuzi ili aendelee kulamba maokoto ya bwerere huko cwt ila ndo hivyo wamemkamia.​
 
Ndg, tpaul na wasomaji wengine.
Mie naujua mgogoro huu wa CWT nje ndani. Kufupisha ni kwamba huu mgogoro hauwezi kuisha kamwe hadi siku Mh. Jenista Mhagama, atakapopoteza uwaziri wake.
Huyu ndiye injinia wa kuanzia uteuzi wa hawa kina maganga kwenda kuwa wakuu wa wilaya.
Katika hili hata mh. Rais Samia nakiri ni majina tu aliletewa na wala hakuwajua.

Mhagama na aliyekuwa Rais wa CWT aliyefungwa kwa matumizi mabaya ya ofisi, ambae aliwahi kuhudumu ktk chama cha walimu, na ndio kisa cha mbivu na mbichi huko CWT.

Kiufupi Mhagama na mkubwa wake flani walikuwa kwenye payroll ya CWT, hawa kina maganga waliwatoa.

Stori ni ndefu. Ipo siku nitaiandika yote.

Ogopa sana mirija ya fedha na siasa za ovyo.
Hiyo kitu nimesikia ila nilikuwa sijui huyu uliyemtaja
 
Sio lazima na hata yeye sio chawa, ila ni Mwalimu na kituo chake ni Temeke kuna maelfu na maelfu ya walimu ambao wanaweza kuongoza hiko chama kama muajiri kakataa arudi kwenye kazi aliyoiomba
Yeye amechagua kutoenda kufundisha na pia aliukataa uchawa. Wewe unatakaje?
 
Hata ile kupewa ukuu wa wilaya ilikuwa ni mipango ya kuelewa wamnase vipi. Akastuka. Ana team kiubwa sana nyuma yake.
Sasa mbona wanaogopa kumfuta kazi? Unadhani yeye hawasomi? Kama kweli wana ubavu wamfute kazi awawashie moto wa makaa ya mawe.
 
Mwajiri ana haki ya kukuita kazini. Mnamjaza tuu huyu Jamaa.
Kuitwa kazini ni suala la binafsi kati ya mtumishi na mwajiri. Kwanini mwajiri anafanya suala la mtumishi mmoja katika halmashauri yake kuwa la kitaifa? Wewe unadhani mwajiri hajavunja haki ya faragha ya mtumishi huyu?
 
Hata ile kupewa ukuu wa wilaya ilikuwa ni mipango ya kuelewa wamnase vipi. Akastuka. Ana team kiubwa sana nyuma yake.
Sasa wameshindwa kumnasa wanalazimisha mambo. CCM ni majitu wa ovyo sana.
 
Mbona walimu wengi tu, kwanini wanalazimisha mwalimu asiyetaka kufundisha? Haya ni matumizi mabaya ya ofisi za umma. Kiongozi unapotumia wadhifa wako kuadhibu watu badala ya kutatua matatizo ya watu. Mwalimu humlipi mshahara, analipwa na CWT. Yeye anataka kuendelea kuwa huko, nyie hamtoi sababu ya kwanini mnataka arejee, mmegeuka miungu. Hamtaki tu, bila sababu yoyote.
Reading between the lines....wanataka kumtumia kama case study kwa watumishi wengine kwamba wasijisahau wanapokuwa kwenye secondment kama huyo bwana...kwamba ukijisahau mwajiri wako anao uwezo wa kutia kitumbua chako mchanga kama ambavyo watatia kitumbua cha huyo mwalimu mchanga.

His options are very limited...for him to save his ass ni bora arudi halmashauri akafundishe au aache ualimu akalime...very likely shule za binafsi pia zikamkataa...hiyo ndiyo practical meaning ya ule usemi: serikali ina mkono mreeeefu!
 
Back
Top Bottom