Leslie Mbena
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 207
- 678
MWALIMU JULIUS NYERERE FOLLOWERS;WAFUASI WA MWALIMU JULIUS NYERERE.
Leo 14:15hrs 09/12/2020
Niwatakie Watanzania wote bara na visiwani heri na baraka tunaposherehekea kumbukumbu ya siku ya Uhuru wetu,Uhuru na maendeleo ni vitu vinavyohusiana sana,uhusiano wao ni
sawa na uhusiano baina ya kuku na yai! bila ya kuku, hupati mayai; na
bila ya mayai, kuku watakwisha,vile vile, bila ya uhuru hupati maendeleo,na bila ya maendeleo ni dhahiri kwamba uhuru wako
utapotea.
Tunapozungumzia habari ya uhuru maana yetu ni nini hasa? kwanza,kuna uhuru wa wananchi yaani uwezo wa wananchi wa Tanzania kujipangia maisha yao,wakajitawala wenyewe bila ya kuingiliwa na mtu
yeyote asiyekuwa mtanzania,Pili, kuna uhuru wa kutosumbuliwa na njaa,maradhi, na umaskini,na tatu,kuna uhuru wake wa kushiriki katika kujiletea kipato chake Cha mfukoni.
Tulipopata Uhuru mwaka 1961 nchi yetu ya Tanzania ilikuwa kama nyumba mpya,nyumba mpya ni nchi changa sawasawa na nyumba mpya mmeijenga vizuri mmetayarisha msingi mkajenga mkaimaliza mkaanza kuishi mnafurahi,baada ya nusu karne ikatokea mtikisiko ile nyumba ikatikiswa ule mtikisiko ukawaonyesheni sehemu mbovu za nyumba ile mlikuwa kwanza mnaiona yote nzuri, nzuri inapendeza, lakini kama ukija msukumo mtikisiko wa kutosha sasa ndipo mtaanza kuona maeneo mabovu,zitatokeza nyufa nyingine ndogo zaidi katika paa,zisipozibwa basi zitaibomoa nyumba.
Watanzania tutaendelea kuyaenzi yale mazuri aliyotuachia hayati baba wa taifa,Mwalimu Julius Nyerere ambaye wakati wa uhai wake alisisitiza suala la amani na Umoja miongoni mwa Watanzania na Waafrika,Watanzania wengi tunamkumbuka baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifariki Octoba 14 mwaka 1999 ikiwa ni miaka 21 leo,Watanzania tunamuenzi Mwalimu Julius Nyerere kwa mengi,lakini kuu ni ile falsafa yake ya umoja ambayo ilimpelekea kuunganisha Tanganyika na Zanzibar.
Alipenda sana kuiona Afrika inaungana na kuwa moja,Kwame Nkrumah wa Ghana alitaka Afrika yote iungane mara moja,Julius Nyerere alitaka hatua ya kwanza iwe kuungana kwa nchi za Afrika Mashariki,wakati Kwame Nkrumah akitaka ungano la moja kwa moja la nchi zote za Afrika kwa wakati mmoja,basi kwa kushirikiana waliunda Umoja wa nchi huru za Afrika, OAU.Mwalimu Julius Nyerere akiongoza kamati ya Ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, aliwakaribisha wapigania uhuru,baada ya Tanzania kupata Uhuru aliwakaribisha na kuwaunga mkono wapigania Uhuru kama Edward Mondlane,Sam Nujoma Samora Machel, Joachim Chisano,Nelson Mandela, waliokuwa wakizipinga serikali za Msumbiji,Afrika Kusini, Namibia na nyinginezo.
Muungano unaleta Umoja,na Umoja ni nguvu,lakini usiwe Muungano wa kusema sisi Wazanzibari, wao Watanganyika,tukumbuke kwamba muungano ndio unaotufanya tuseme,sisi Wazanzibari, wao Watanganyika,Nje ya muungano hatuwezi kusema hivyo nje ya
muungano hakuna Wazanzibari,Nje ya muungano kuna Wao Wapemba,sisi Waunguja.
“...Hamuwezi kukaa salama baada ya kutenda dhambi
ya kubagua watu wa nchi yenu ile ile moja, mkawaita
wale wao, na hawa sisi. Dhambi ile haishii hapo.
Ndiyo historia ilivyo, ni sheria ya historia siyo sheria
ya Mwalimu Nyerere...”
“...Ndivyo ilivyofanyika Kobe juzi juzi kule Japani.
Tikisiko lile halikumalizika. Lingepita mara moja,
vupu! Kobe isingekwisha. Lakini likaendelea,
yakaanguka majumba mengi sana sana...”
“...vijumba vya kwanza vitapitiwa… Wapemba…
Wapemba, mtamaliza vya Wapemba. Halafu mtakuta
ninyi mliokuwa mnajiita sisi… sisi Watanganyika,
mtakapoanza kuchoma nyumba za Wapemba zile
mtakuta, aah! si sisi… sisi, hawa wote si wamoja...”
Mwalimu Nyerere anaheshimiwa na Watanzania wengi kwa uadilifu na moyo wake wa kutumikia kuliko kutumikiwa.
“Hatuna budi kujenga nchi hii kwa kujitegemea”,hatuwezi kuwa tunataka masilahi yetu ya Watanzania ya afya bora,maisha bora na elimu nzuri, lakini eti tudhani tunaye mjomba huko nje atakuja kutuletea maslahi hayo,hatuna! Tutajenga nchi hii kwa faida yetu wenyewe sisi wenyewe,Akipatikana mtu kutusaidia,tutamshukuru,Lakini kazi ya kujenga nchi hii kwa manufaa ya Watanzania wote ni kazi ya Watanzania,si kazi ya mtu mwingine,Msimamo huo tukauita Siasa ya Kujitegemea.“Nchi ya Ujamaa”, tukasema, “ni nchi ambako kila mtu anafanya kazi,Kama ni mkulima,anafanya kazi,kama ni mfanyakazi, anafanya kazi”,lililokuwa la msingi na linalotawala ni mfanyakazi,maslahi yanatokana na kazi yake na jasho lake,
-Je Mashirika ya Umma yananuka!?
Mwalimu Julius Nyerere alisema kidogo juu ya hiki kitu kinachoitwa mashirika ya umma,Je Mashirika ya Umma yananuka? Hata hivyo, hata kama yananuka, nataka kujua kwa nini yananuka,Lazima tujiulize kwa nini yananuka,sababu ya kusema hivi ni kwamba mimi nilikuwa sijui,lakini vijana walinikumbusha wakaniambia “Mwalimu, ulipoondoka, uliacha kumi na mbili”, Mimi kitu kimoja nilichokuwa nakifikiria ni kwamba sasa viwanda vyetu vya nguo vilikuwa vinafikia shabaha ile tuliyokuwa tunataka ya kuweza
kutumia asilimia themanini na tano (85%) ya pamba hapa nyumbani,
Watu tunaafikiana na wazo,lakini mawazo ambayo wazi wazi ni ya kijinga lazima tuyakatae,Kwa sababu mtu mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu,usipoyakataa, atakudharau. Narudia, mtu yoyote mwenye akili akikupa mawazo ya kipumbavu na wewe una akili na unajua ni ya kipumbavu na ukayakubali,atakudharau. Sasa hatuwezi tukakubali mambo ya kipumbavu Tanzania,Hali hiyo inaendelea na wala haijabadilika mpaka leo, kwani bado duniani tunaona nchi zenye viwanda huvibana viinchi vidogo viache
mambo ya viwanda,sasa taabu yetu, wala si Tanzania peke yake kuna viinchi vingi,ni kwamba viongozi wetu hawakatai,Wanakubali tu,
Lakini Je sisi ni madodoki?Dodoki ulitumbukize katika maji, hata yenye takataka, linazoa tu!kusema kweli, duniani watu wanafikiri kwamba labda sisi ni maskini,Lakini umaskini mbaya kuliko wote ni umaskini wa mawazo,ni mbaya sana,duniani kuna kujitegemea na kutegemea,unaweza kutegemea,lakini kutegemea kokote ni kubaya sana,kwa hali yo yote ile, kutegemea kubaya kupita kote kabisa ni kutegemea mtu mwingine kwa mawazo,huku ni kwa ovyo sana kwa maanakunakunyima utu wako.
Niwakumbushe nukuu hizi za Mwalimu Julius Nyerere,ni baadhi, lakini ni sehemu ya kuelewa mchango wa Julius Nyerere katika kumakinika katika
jitihada za kusaidiana kuelewa tunatoka wapi, tuko wapi na tunakwenda
wapi,Na kama tunataka kwenda huko,tufanyeje ili tufike huko,tusije
tukashtukia tunapelekwa mahala ambako siko tulikokuwa tunakusudia,
“...Jeuri ya ukoloni ni jeuri ambayo inazidi jeuri
yoyote nyingine duniani. Ni jeuri ambayo, waliyo
nayo jeuri ile, wanakata usawa wa watu wote. Maana
huwezi ukaamua kwamba utawatawala watu wengine
wakipenda wasipende, bila kukana usawa wa
binadamu. Lazima kwanza uukane usawa useme watu
siyo sawa na wewe...”
“...Waingereza wanawadanganya, Waingereza
wametumwa na ule Umoja wa Mataifa uliokufa
(League of Nations), waje kuishika Tanganyika kwa
muda tu; watusaidie, na wakati tutakapokuwa tayari,
watuachie tujitawale...”
“...Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu, nikawa
ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi.
Baadaye wazee wakanipa baiskeli, nikawa ninakuja
mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.
Hivyo ndivyo tulivyofanya...”
“...Katibu wakati huo. Nilipelekwa na Kasela Bantu
ambaye naye aliteleza teleza na hatunaye hapa
(kwenye mkutano). Kasela Bantu alikuwa mwalimu
mwenzangu. Tulifundisha pamoja Milambo.
Nilipokuja Dares Salaam, nikakuta anafanya kazi
Redio (Tanganyika Broadcasting Corporation). Ni
Kasela Bantu aliyenipeleka kwa Abdul Sykes...”
“...Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana cha
matatizo. Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni.
Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana.
Katika muda wa miezi mitatu, wakanichagua Rais wa
TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya
kuandika Katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa
ya shabaha ya kuleta uhuru...”
“...Wazee na Ndugu zangu! Wazee hasa ndiyo
walikuwa na mikutano ya awali ya TAA na TANU.
Walikuwa na msimamo wa hali ya juu kabisa!
Hawakuyumba hata kidogo! Vijana walikuwa na
mashaka. Wengine walikuwa na vikazi vyao,
waliogopa kuvipoteza...”
Wanasema ngoma ya watoto haikeshi! Mimi nilipata baraka za wazee,tangu zamani. Tangu awali kabisa,Siku moja, Dosa akanifuata
Magomeni (Dar es Salaam). Akasema: Leo wazee wanakutaka,wapi? Kwa Mzee Jumbe Tambaza. Wanakutaka usiku. Nikasema haya, nitakuja,nikaenda,Nikakuta wazee wameshakaa; wameniita kijana wao
kuniombea dua. Mimi Mkristo, wao Waislamu watupu,Wakaniombea
dua za ubani,tukamaliza. Tulipomaliza,wakasema kuna dua pia za wazee wao.
Basi wakanitoa nje,tukatoka,zilipomalizika zilikuwa za Korani,sasa zikaja dua za wazee za jadi,Walikuwa na beberu la mbuzi,Wamechimba shimo,wakaniambia simama,Nikasimama. Beberu akachinjwa, huku anaambiwa, “Twining (Twainingi)umekwisha!”
(Edward Twining alikuwa Gavana wakati huo),ndipo nikaambiwa:
Tambuka! Nikavuka lile shimo,hapo nikaambiwa na wazee,Basi nenda
zako; tangu leo Twainingi amekwisha! Sasa mimi Mkristo; hao waislamu,na mimi mkorofi korofi katika mambo haya (ya kutambika),lakini tulikuwa tunaelewana na wazee wangu hao,Kwa hiyo nilitambuka pale na kuambiwa,Nenda nyumbani salama,Twaining hawezi tena! Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa tunakwenda Bagamoyo,kwenye makaburi kule! Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee wangu,
Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa wa Kenya, hawa
akina Tom Mboya (marehemu) walishitakiwa,Tukasema tuwasaidie,tuwasaidie vipi? Tukasema tufunge. Tukaomba nchi nzima kufunga siku hiyo,tufunge! Tukafunga. Hakuna kula.Na siku ya kufunga tulikuwa na mkutano Bagamoyo. Tukaenda huko,tukafanya mkutano hadi saa 12 jioni. Baada ya mkutano tukaenda nyumbani kwa Mzee Mohamed Ramia (marehemu). Hapa ndipo tulikuwa tumefikia,Mimi nikamuuliza mzee,Sheikh, una Aspro? Akajibu,Kwa nini unataka Aspro? Nikajibu kuwa kichwa kinaniuma kweli kweli,akasema subiri,Tulisubiri hadi saa ya kufuturu,Tukafuturu vizuri,Mzee Ramia akaniuliza bado unataka Aspro? Nikajibu kichwa sasa hakiumi,kumbe ilikuwa njaa,Nawaelezeni haya kwa sababu huko tulikotoka,tulishikamana sana,tulishirikiana sana na wazee…”
“...Wazee wangu wengine wanakumbuka tulikuwa
tunakwenda Bagamoyo. Kwenye makaburi kule!
Tunapiga dua huko kwenye makaburi na wazee
wangu. Baadhi yetu mtakumbuka safari moja jamaa
wa Kenya, hawa akina Tom Mboya (marehemu)
walishitakiwa Tukasema tuwasaidie. Tuwasaidie
vipi? Tukasema tufunge...”
“...(Edward Twining ndiye alikuwa Gavana). Ndipo
nikaambiwa: Tambuka! Nikavuka lile shimo. Hapo
nikaambiwa na wazee: Basi nenda zako; tangu leo
Twainingi amekwisha! Sasa mimi Mkristo; hao
waislamu. Na mimi mkorofi korofi katika mambo
haya (ya kutambika)...”
“..huko kwamba Tanzania ukishalivunja hili
hawatalijenga tena. Lakini vijana wakalijenga. Daraja
lile wakalijenga kwa muda mfupi kabisa likesha
wakavuka Walipovuka Amini akapiga kelele, Jama!
Wameniingilia! Niliwahi kuona mchezo mmoja watu
wawili wanapigana, sasa mmoja huyu maneno yake
mengi sana...”
“...Akasema Tazama Afande, mimi shujaa kweli
kweli; nina moyo kama wa simba. Taabu yangu mimi
ni miguu. Kila ikipigwa risasi miguu inakimbia
pamoja na moyo wake” Amini hodari sana kwa
kupiga makelele. Lakini vijana walipokwisha vuka
mto si kelele hizo. Na mbio hazikuwa ndogo…”
Nimalizie kwa kusema Mwalimu Julius Nyerere ni kiongozi ambaye
alikuwa na kipaji cha uongozi hali iliyofanya kuwa na ushawishi mkubwa kwa
wananchi hata baada ya kuondoka madarakani.Pia ni kiongozi aliyekuwa anayaishi yale yote ambayo alikuwa anayasema katika hotuba zake na kuyasimamia,Aidha,
alikuwa ni kiongozi mwenye uthubutu jasiri na anayejiamini na alikuwa hayumbishwi ovyo,alikuwa ni muumini wa ukweli na uwazi,Kwa hakika
baadhi ya mambo aliyoyasema katika hotuba zake iwapo yatapuuzwa taifa
litayumba.
Natoa Wito kwa jamii kujenga utamaduni wa kusikiliza, kutazama na kusoma hotuba za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ili kuona na kuelewa mambo muhimu kwa taifa aliyoyasema ili jamii iweze kuyafuata na kuyaishi kwa kuwa yana mchango mkubwa kisiasa kiuchumi na kiutamaduni katika taifa la Tanzania,Vyombo vya habari vinavyorusha hotuba za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika redio na runinga watenge muda wa kutosha ili waweze kurusha hotuba nzima kwa wasikilizaji na watazamaji waweze kupata maudhui ya hotuba nzima,
Natoa wito kwa taasisi ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ijitangaze katika vyombo vya habari kwa kubainisha kazi zake na,ikiwezekana, iwe na kipindi maalumu katika vyombo vya habari, hususani katika kituo cha runinga cha taifa ambacho ni TBC1 ili wananchi waweze kupata elimu kuhusiana na kazi za taasisi hiyo.Natoa Wito pia kwa taasisi ya Julius Nyerere kufuata na kuenzi misingi yote iliyoasisiwa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Aidha, nashauri iwepo Tuzo ya Kitaifa na kimataifa ya Mfuasi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.