Mwalimu Maganga, Katibu Mkuu CWT aliyekataa uteuzi wa Ukuu wa Wilaya arudishwa kwenye Ualimu

Kwa nini barua ya mwajiri na mwajiriwa inawekwa kwa umma. Kwani alipoomba kuazimwa alituandikia?
Anyway kwani KAZI ya ualimu ni adhabu? Si ndio aliisomea?
 
Safii sana, ilikuwa dharau sana kwa Mamlaka ya uteuzi, yaani unamchagua mtumishi wa Umma kuwa DC anakataa kweli? Safii kabisa
Kwa hiyo kama hana uzoezi na hiyo KAZI ya UDC na anaona ataharibu akubali tu?
 
Safii sana, ilikuwa dharau sana kwa Mamlaka ya uteuzi, yaani unamchagua mtumishi wa Umma kuwa DC anakataa kweli? Safii kabisa
Si aliona wanamtoa kwenye ulaji

Ova
 
Huu utawala wa kukomaa, visasi na vinyongo hautakuwa na mwisho mzuri, wangejifunza kwa awamu iliyopita
 
Kwamba tangazo haliwezi kuwa taarifa?
Haliwezi, Tangazo na Taarifa ni vitu viwili tofauti kabisa. Kimsingi hili halikupaswa kuwa Tangazo bali Taarifa.

Tangazo linakaribisha walioandikiwa kushiriki hilo jambo mf. Kununua, kuuza, kuomba, kutaarifu

Ila Taarifa ina lengo moja tu, kufahamisha, na halihitaji sisi umma kufanya jambo.

Hivyo hapo ilitakiwa kutupa taarifa tu na sio kututangazia sababu hakuna tutakachofanya juu ya hilo tangazo lao.
 
Sijaelewa mantiki ya kututangazia sisi, wakati barua hiyo ilipaswa kuwa confidential
 
Hizo akiliiiii au tope?
 
Akaache kazi
 
Hizi ndizo akili za watanzania maana 99.9% ni machawa hawana msimamo na wala hawafuati wanachotaka.
Yeye hakutaka uteuzi akakataa, ila watu wanamnanga kama vile kuna kosa alilofanya

Hajafanya kosa lolote ila na wao wanamuhitaji hapo Temeke akashike chaki! Kuna tatizo mwajiri wako kukuita kazini?
 
Ndiyo watawala wako hao. Siku zote wanatumia njia za aina hii ili kutengeneza mazingira ya kuogopwa.

Ningekuwa mimi ndiyo huyo Mganga, nisingeripoti hiyo tarehe 1 Oktoba. Halafu wakinifukuza kazi yao, poa tu.

Au sio😁
 
Jamaa watakua wameshamtengea ka kesi kake saafi ka either kubaka Mwanafunzi.
Ni swala la muda tu.
Huyo jamaa angekuwa anajielewa ni bora angekimbia nchi tu.
mpaka sasa Jamaa watakua wameshamtengea ka kesi kake saafi ka either kuja kudharirisha Mwalimu mwenzake au kubaka Mwanafunzi. Lakini kabla ya hizo kesi wataanza kwa kumpandisha Cheo.

Ni swala la muda tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…