Mwalimu Mkuu shule ya msingi Mavovo Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga ana tabia mbovu, hafai kuwa mtumishi

Kama ni kweli si vyema hata kidogo
 
Ila Kuna taasisi na ofisi za serikali tanga zinaenda taratibu Sana...
 
Nimepata taarifa hili swala limeanza kushughlikiwa leo,wahusika walifika shuleni na wamehojiwa baddhi ya wanafunzi na Mwalimu husika ameanza kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Na hii yote inatokana na wahusika kuona maelezo haya hapa jukwaani,Asante Jf jukwaa letu pendwa lidumu milele

Nitawajuza yatakayojiri zaid wakuu
 
Kapicha ka udhalilishaji
 
Wewe utakuwa ni Mwl WA hiyo shule,vijihela vya madaraka anavyopewa mkuu wako usivionee wivu
Kama Mwl anashida kwanini msiseme kwenye ngazi husika
Acha umbea na ushakunaku

Alooo[emoji23][emoji23]
 
...Poleni. Kwa hiyo Wazazi hawawezi hata kuitisha kikao tu cha kumhukumu??
 
...Kwa hiyo wewe ulishindwa kuwapa ushauri wowote... Mpaka uishirikishe JF??
 
Watakushukia wenzie kama vipanga mkushi mbishi umejiandaa kisaikolojia????
 
Kama unazunguka kusaidia watu mbona hujui sehemu sahihi kufikisha haya majungu yako?
 
Ndugu zangu hawa watu walikuwa hawana pa kusema mattzo yao,nimewasemea hapa hata hazijapita siku tatu wamepata msaada baada ya wahusika kusoma hapa na kwenda kufanya uchunguzi wao,wakajiridhisha kuwa ni kweli na mhusika wakamrekebisha.

Sasa tatizo liko wapi? Tusikae kubishana Tu kuhusu siasa na mapenzi tujaribu kusaidia kutatua mambo ya wazi mtaan yanayowatesa watoto wetu na wanawake.Kwan ni Nani asiyejua kuwa kuna waliopewa mamlaka na wanayatumia vibaya kujiona miungu watu! bila shaka wengi wanaopinga wapo sekta Fulani na wao wana yao wanayoyafanya kama huyu Mwalimu.

Ukiona maovu usikayakalie kimya,yaondoshe Kwa mkono,ukishindwa tumia ulimi kuyasema

Huoni wamesaidika wazaz na wanafunz wangapi ambao miaka yote wanateseka na kadhia hii.

Tuache ujinga bhana tuijenge nchi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…