Mwalimu Nyerere alikuwa akijiaminia nini?

Mwalimu Nyerere alikuwa akijiaminia nini?

Umepiga humo humo, hakuna cha maana alichofanya hapa Tanzania huwa sikioni
Huwezi kukiona kwa sababu hujui ulipotoka umedandia treni kwenda mbele. Hujui historia ya nchi yako na hilo ndio tatizo kubwa linalokusumbua. Ni sawa uende china au usa useme honi walichofanya hao founders wa nchi hizo. Labda nikusaidie kimoja tu cha maana kuliko vyote ambacho wewe kilaza hujui. Nyerere ndiye aliyeongoza kudai uhuru wa nchi hii hadi ukapatikana mwaka 1961. KAMA HATA HILO HULIONI WEWE NI KILAZA WA KIWANGO CHA RELI CHAKAVU.
 
Huyu baba alikuwa akiwatukana wazungu mara kwa mara na kuwaita majina ya ajabu ajabu

Aliwavimbia wareno kule Angola mpaka wakasepa zao Ulaya

Akawa mwenyekiti wa nchi zilizo mstari wa mbele kupambana na kaburu kule SA

Akamvagaa mbabe Idd Amini na kumfurusha kutoka Uganda

Akastaafu akarudi kijijini akafa kifo cha kawaida kabisa

Alikuwa akilindwa na nini huyu baba,ama aliwahi kuwa komandoo

Genetic Mara. People with ver high self esteem .
Watu hudhoofu kutokana na hofu na kutojiamini na kulamba lamba watu na ma beberu viatu.
 
Huyu baba alikuwa akiwatukana wazungu mara kwa mara na kuwaita majina ya ajabu ajabu

Aliwavimbia wareno kule Angola mpaka wakasepa zao Ulaya

Akawa mwenyekiti wa nchi zilizo mstari wa mbele kupambana na kaburu kule SA

Akamvagaa mbabe Idd Amini na kumfurusha kutoka Uganda

Akastaafu akarudi kijijini akafa kifo cha kawaida kabisa

Alikuwa akilindwa na nini huyu baba,ama aliwahi kuwa komandoo
Mwl hakuwai kuvaaa zile nguo za kijani
 
Sala na majitoleo, na kufunga kwa siri sio funga za kujitangaza. Kifupi alikuwa mtu wa ibada na alilindwa na Mungu
 
Hayo uliyoyasema kuwa aliyafanya ndio maana Tanzania hadi sasa tuko poor sababu ni yeye.Magufuli alifanana sana Nyerere kwa kiburi kisichokuwa na maana ambacho kinatokana na mawazo binafsi.

Mfano,Nyerere aliona kabisa Sera za ujamaa zinafeli na dunia inabadikika kutoka ujamaa kwenda ubepari baada ya USA kushipa power lakini kwa makusudi kabisa yeye akashikilia msimamo wake wa kijinga na mwisho wake kuifanya Tanzania Nchi fukara.

Kingine,Vita ya Uganda ili tu amulinde rafiki take Obote-alitupa hasara sana.ugomvi wa Idd amin na Tz unatokana na Nyerere kumpa hifadhi Obote-hata ungekuwa wewe ndio Idd Amin nadhani unge react tu.
Kuhusu vita ya uganda ndugu yangu utamuonea bure nyerere,iddi amin aliingia misenyi hadi kyaka akisema ni sehemu ya uganda,mtu kama huyo unamfanyaje
 
Back
Top Bottom