Mwalimu Nyerere alikuwa mroho wa madaraka ila sio mali, Hayati Magufuli alikuwa mroho wa madaraka na mali

Mkuu watu wanakusubiri
Chozi...
Naomba niweke kitu hapa:

''Wakati nikifundisha Minaki nilijiandikisha katika Woolssey Hall College ya London, Uingereza ili kupata masomo kwa njia ya Posta .

Masomo hayo pamoja na cheti nilichopata cha London Matriculation ndivvyo vilivyoniwezesha kukuballiwa kupata Scholarship Ya British Council mwaka 1950 kwenda kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Scotland, Uingereza.

Huko Edinburgh nilisoma kwa miaka mitatu na kupata degree yangu ya M.A katika masomo yafuatayo:- Political Economy,Economy History,British History,Constitutional Law, Botanical Science,Moral Philosophy na English Literature. Mwaka 1954 nikarudi nyumbani na kwenda Minaki kuendelea kufundisha wakati huo nikiwa makamu wa mkuu wa chuo.

Niliporudi mwaka 1954 nilikuta chama cha siasa cha TANU (Tanganyika African National Union) kimekwisha kuanzishwa, kwa hiyo nikajiunga nacho na nikachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Tawi la TANU Wilaya ya Kisarawe.''

John Keto


Waliosimama wa nne kulia ni John Keto University of Edinburgh 1953​
 
Mkuu watu wanakusubiri
Chozi...
Naomba niweke kitu hapa:

''Wakati nikifundisha Minaki nilijiandikisha katika Woolssey Hall College ya London, Uingereza ili kupata masomo kwa njia ya Posta .

Masomo hayo pamoja na cheti nilichopata cha London Matriculation ndivvyo vilivyoniwezesha kukuballiwa kupata Scholarship Ya British Council mwaka 1950 kwenda kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh, Scotland, Uingereza.

Huko Edinburgh nilisoma kwa miaka mitatu na kupata degree yangu ya M.A katika masomo yafuatayo:- Political Economy, Economy History, British History, Constitutional Law, Botanical Science, Moral Philosophy na English Literature.

Mwaka 1954 nikarudi nyumbani na kwenda Minaki kuendelea kufundisha wakati huo nikiwa makamu wa mkuu wa chuo.

Niliporudi mwaka 1954 nilikuta chama cha siasa cha TANU (Tanganyika African National Union) kimekwisha kuanzishwa, kwa hiyo nikajiunga nacho na nikachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Tawi la TANU Wilaya ya Kisarawe.''
John Keto


Waliosimama wa nne kulia ni John Keto​
Wa
 
Mkuu vijana wa leo wanapaswa wasome historia kama hizi. Enzi hizo wasomi wenye elimu ya juu walipenda kuendelea kuwa Waalimu kwenye Shule na Vyuo Vikuu ili kuendelea kuzalisha wasomi bora kwa manufaa ya Nchi. Leo, wengi wa wasomi wa ngazi hiyo hawapendi kufundisha vyuoni wanakimbilia Kwenye Siasa na hasa Ubunge. Wakati mwingine unashikwa na butwa unapomkuta msomi wa Udaktari wa Binadamu, kabukua miaka 7 Chuo badala aendelee na fani yake, aidha akafundishe Vyuoni ili akawatengenezi wasomi wengi kama yeye au aendelee na utabibu wake ili atoe huduma yake ya utabibu kwa wahitaji, yeye anamua kwenda kwenye Siasa. Anakuwa katika mijadala na watu wa darasa la 7 au form V1 eti naye anachangia hoja. Ifikie mahali Serikali ilioni hii kwa jicho la TATU
 
Jiwe alipenda vyote, mali pamoja na madaraka. Madaraka yalimuwezesha kuua anayetaka kumuua, kutesa anaotaka kutesa na kupoteza anaotaka wapotee na huko kwenye uroho wa mali ndiyo balaa zaidi yaani kampuni yake ya Mayanga construction ilikuwa ikila tenders si mchezo bado zile za plea bargain zilizohufadhiwa kwenye mabenki ya ughaibuni. Lile jibwa lilikuwa ni jizi kinoma.
 
Nyerere alitawazwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanganyika tarehe 9 Desemba 1961. Miezi miwili baadaye akaachia ngazi na kumpisha Rashidi Kawawa kuwa Waziri Mkuu wakati yeye alirudi kufanya kazi ya Chama cha TANU, kukiimarisha. Alibakia kwenye Chama hadi tarehe 9 Desemba 1962, Tanganyika ilipobadilika na kuwa Jamhuri, ndipo akarudi madarakani na kuwa Rais.
Jee, kuachia madaraka ya Waziri Mkuu kwa karibu mwaka mzima ni uroho wa madaraka?
Nyerere ni mzawa wa ukoo wa kichifu. Hivyo, alikuwa kwenye mstari wa kuwa chifu siku za usoni, sawa na mfalme wa sasa wa Uingereza aliyesuburu zaidi ya miaka 70 kuja kuupata ufalme. Akiwa Rais wa Tanganyika, Nyerere alifutilia mbali mambo ya uchifu mwaka 1963. Hoja yake ilikuwa kwamba mtu apewe madaraka kwa kustahili kwake na siyo kwa kuwa amezaliwa kwenye ukoo fulani.
Jee, kufuta huko kwa uchifu ni uroho wa madaraka wa Nyerere?
 
Pamoja na mazuri yoooooote! Muungano na Mwenge, pamoja na uzuri wake, kwa sasa tufanye yaishe tu.

Sent from my SM-G977B using JamiiForums mobile app
 
Usichanganye mambo,chief wa wazanaki hawezi kuwa sawa na Rais wa Tanzania,nyerere alikuwa kwenye line ya kuwa chief wa uzanaki sio Tanzania.
So aliona machifu watahatarisha kiti chake cha urais,nawasilisha mkuu
 
Asante sana mzee Mohamed Said kuweka kumbukumbu sawa ,hakika wewe ni kisima cha historia ya Tanzania
 
Usichanganye mambo,chief wa wazanaki hawezi kuwa sawa na Rais wa Tanzania,nyerere alikuwa kwenye line ya kuwa chief wa uzanaki sio Tanzania.
So aliona machifu watahatarisha kiti chake cha urais,nawasilisha mkuu
Sawa sawia, alikuwa kwenye lineage ya chief wa Wazanaki si chief wa Tanzania(Tanganyika) hivyo akawa amebaini tofauti ya Uchifu wa Wazanaki na uraisi wa Tanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…