Mwalimu Nyerere alikuwa mroho wa madaraka ila sio mali, Hayati Magufuli alikuwa mroho wa madaraka na mali

Hicho ni kisa cha kweli fuatilia,
 
Ongezea kuvunja vyama vya ushirika (original), baadaye kuvirejesha na kuviweka chini ya makada wa TANU, kupunguza nguvu (autonomy) ya halmashauri (local governments), n.k.

Kifupi Nyerere alitaka kuwa na udhibiti kamili juu ya taasisi zote kuu za wananchi za kiutawala, kiuchumi na kijamii - hata za dini. Alikuwa na nia njema ya dhati ya kuliletea taifa maendeleo lakini kupitia one man show. Hakuwa tayari kwa mawazo mbadala wala kugawana utukufu na mtu mwingine.
 
Hata nchi kubwa kubwa watu ambao wanaonekana ni wasaliti WA nchi na wanahatarisha usalama WA nchi huwa wanaondolewa hata marekani yenyewe labda Kina lisu walikuwa haohao wasaliti.
Karne hii unakuwa na mawazo ya kuuana kisa madaraka?? Sio poa ndugu yangu,siasa zinataka akili badala ya mabavu,mbona sasa tunaishi kwa amani na nchi inakwenda,tusiuane kisa madaraka
 
Hayo yote kikwete na JK waliyafanya
Hata wakati wa kikwete watu wengi waliuawa na serikali.ila kina kikwete walishindwa kujenga ikulu Dodoma,walishindwa kuanzisha mradi WA bwawa la maji,walishindwa kuanzisha kujenga Reli ya kisasa,alileta nidhamu makazini,ufisadi ulipungua lakini sasa hivi umerudi. ni uongo kusema Magufuli alikuwa raisi muovu kuliko wote.
 
Karne hii unakuwa na mawazo ya kuuana kisa madaraka?? Sio poa ndugu yangu,siasa zinataka akili badala ya mabavu,mbona sasa tunaishi kwa amani na nchi inakwenda,tusiuane kisa madaraka
Hata sasa hivi kwenye nchi hizo kubwa mtu unaweza kuondolewa kama umeenda kinyume na mfumo.
 
Uko sahihi mkuu na hapo ndio walipofanana na JPM one man show
 
Mim siwez jisumbua na mtu ambae tayali katangulia mbele za haki.
 
Kujenga ikulu dodoma sioni kama ni big deal,haina impact na maisha ya ntanzania ya kila siku,ipo kisiasa tu,Nyerere alijenga mabwawa meni sana mtera,kidatu,hale nk.reli ya Tazara nk,kikwete shule kata zote,mikopo vyuoni,ajira lukuki na kukuza demokrasia
 
Mroho wa madaraka.
Mroho wa mali
Mroho wa damu za watu
Mroho wa mali za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…