Mwalimu Nyerere alikuwa mroho wa madaraka ila sio mali, Hayati Magufuli alikuwa mroho wa madaraka na mali

Kisiasa bado hakuna chama ambacho kinauwezo WA kuitoa CCM madarakani hata wakati wa magufuli.lakini huenda kulikuwa na Jambo lingine kubwa ambalo lilisababisha hao wanaojiita wapinzani kuumia enzi hizo.hawakuwa na uwezo wa kuitoa CCM madarakani.
Kumbe kinachokuuma ni utaratibu wa kuiondoa ccm madarakani?Umuhimu wako na Watanzania wengine huuangilii?Wewe kazi yako ni kuangalia usalama wa Chama na siyo usalama wa nchi na wananchi wake kwa ujumla?
 
Mimi hata sio kusuma gang Kwanza hakuna kitu kama kusuma gang.mimi najaribu kuwaelewesha nyie ambao hamtumii Akili.
Sukuma ipo na isingekuwepo au kama usingekuwa unaifahamu ungeishangaa ni kitu gani lakini kile kitendo kukana kwamba haujihusishi au si miongoni mwa hao Sukuma gang it means unatambua uwepo wa hiyo click lakini unachokataa ni kuwa miongoni mwao.
 
Mkuu nakubaliana nawe, lakini nataka nijazie nyama kidogo. Mwalimu alikuwa mtu wa maono; Muungano wa Tanganyika na Zanzibar aliufanya, pamoja na sababu zingine tunazojua lakini yeye alilenga zaidi wakoloni na waarabu wasije kuweka base pale Zanzibar. Ili Tanganyika iwe huru na usalama ni lazima Tanganyika na Zanzibar iwe Nchi moja.

Mwalimu aliona mbali. Leo Nchi kubwa Duniani, zinatafuta urafiki na
nchi ndogo ndogo zilizopo karibu na adui yake kwa ajili ya kuweka base ya ulinzi kwa nchi yake. Tunamuona Mmerikani anavyo zungukia vinchi vilivyo pakana na Mrusi, Mchina anavyo hangaika na Japan na Hong Kong sababu za kiulinzi. Hivyo JKN alikuwa na maono ya miaka mingi ijayo. Ndio maana waelewa wakampatia jina la kumuenzi kwa kazi zake zilizo tukuka "BABA WA TAIFA"
 
Unamuongelea Nyerere ambaye hujawahi kumuona wala kumsikia, ila kwa kumsoma tu vitabuni.
Una kalaana fulani.
 
Lakini Sasa Tunamshukuru Mungu tuna kiongozi mwenye hofu ya Mungu asiependa kuona wananchi wake wanateseka katika vitu watanzania tunatakiwa kuungana na kumshukuru Mungu kila siku ni kumpata kiongozi kama Rais Samia Suluhu ambaye anasimamia haki, Sheria na katiba ya nchi
 
Kijana acha upotoshaji wa makusudi/kutokujua Nyerere kuondoa mfumo wa kichifu haikuwa hoja yake ilikuwa hoja ya Afrika nzima ukiwemo Kabaka system kule Uganda maana machifu kabla ya uhuru kwenye maeneo yao walikuwa na limitless power na waliendelea hivyo hata baada ya uhuru,viongozi wa kitaifa walikosa ushawishi mbele ya machifu ili kuleta umoja wa kitaifa mfumo wa kichifu uliondolewa.
Upotoshaji mwingine ni juu ya jina la mtoto wa Nyerere "Madaraka" halikutokana na Nyerere kuwa mroho wa madaraka ila jina limetokana na watu waliozaliwa mwaka 1962 ambapo madaraka yalipelekwa mikoani(decentralization)maana baada ya uhuru mfumo ulikuwa centralized,ambapo Nyerere alikuwa anafanya maamzi ya kila kitu,kabla ya 1962 wakuu wa wilaya na mikoa walikuwepo lakini hawakuwa na uwezo wa kutoa maamzi isipokuwa Nyerere mwenyewe,kwa kifupi serikali za mitaa zilianza muda huo(madaraka mikoani)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…