Mwalimu Nyerere alikuwa mroho wa madaraka ila sio mali, Hayati Magufuli alikuwa mroho wa madaraka na mali

Mwalimu Nyerere alikuwa mroho wa madaraka ila sio mali, Hayati Magufuli alikuwa mroho wa madaraka na mali

Kijana acha upotoshaji wa makusudi/kutokujua Nyerere kuondoa mfumo wa kichifu haikuwa hoja yake ilikuwa hoja ya Afrika nzima ukiwemo Kabaka system kule Uganda maana machifu kabla ya uhuru kwenye maeneo yao walikuwa na limitless power na waliendelea hivyo hata baada ya uhuru,viongozi wa kitaifa walikosa ushawishi mbele ya machifu ili kuleta umoja wa kitaifa mfumo wa kichifu uliondolewa.
Upotoshaji mwingine ni juu ya jina la mtoto wa Nyerere "Madaraka" halikutokana na Nyerere kuwa mroho wa madaraka ila jina limetokana na watu waliozaliwa mwaka 1962 ambapo madaraka yalipelekwa mikoani(decentralization)maana baada ya uhuru mfumo ulikuwa centralized,ambapo Nyerere alikuwa anafanya maamzi ya kila kitu,kabla ya 1962 wakuu wa wilaya na mikoa walikuwepo lakini hawakuwa na uwezo wa kutoa maamzi isipokuwa Nyerere mwenyewe,kwa kifupi serikali za mitaa zilianza muda huo(madaraka mikoani)
Mkuu leo pamoja na Local Government kuwepo lakini bado Central Government inainyang'a Local Government wajibu wake; sasa unadhani nini kifanyike?
 
Nyerere alitamani Afrika iwe nchi moja. Super power isiyotishwa na Marekani wala Urusi ya enzi hizo. Viongozi wengi waliopigania uhuru waliamini umoja ni nguvu. Hakutaka kuongoza Afrika kama yupo kiongozi sahihi anayelijua hilo. Alikuwa mwanamapinduzi mzalendo.
 
Kijana acha upotoshaji wa makusudi/kutokujua Nyerere kuondoa mfumo wa kichifu haikuwa hoja yake ilikuwa hoja ya Afrika nzima ukiwemo Kabaka system kule Uganda maana machifu kabla ya uhuru kwenye maeneo yao walikuwa na limitless power na waliendelea hivyo hata baada ya uhuru,viongozi wa kitaifa walikosa ushawishi mbele ya machifu ili kuleta umoja wa kitaifa mfumo wa kichifu uliondolewa.
Upotoshaji mwingine ni juu ya jina la mtoto wa Nyerere "Madaraka" halikutokana na Nyerere kuwa mroho wa madaraka ila jina limetokana na watu waliozaliwa mwaka 1962 ambapo madaraka yalipelekwa mikoani(decentralization)maana baada ya uhuru mfumo ulikuwa centralized,ambapo Nyerere alikuwa anafanya maamzi ya kila kitu,kabla ya 1962 wakuu wa wilaya na mikoa walikuwepo lakini hawakuwa na uwezo wa kutoa maamzi isipokuwa Nyerere mwenyewe,kwa kifupi serikali za mitaa zilianza muda huo(madaraka mikoani)
Kuhusu jina madaraka nilichomekea tu uko sahihi.
Lakini kuhusu machifu ukiangalia kwa jicho la tatu kulikuwa na hofu kw viongozi wa kiserikali kuzidiwa ushawishi na machifu.
Ilionekana watu wanawatii machifu kiliko wanasiasa, kupiga marufuku uchifu ilikuwa ni kujilinda tu kisiasa
 
Nyerere alitamani Afrika iwe nchi moja. Super power isiyotishwa na Marekani wala Urusi ya enzi hizo. Viongozi wengi waliopigania uhuru waliamini umoja ni nguvu. Hakutaka kuongoza Afrika kama yupo kiongozi sahihi anayelijua hilo. Alikuwa mwanamapinduzi mzalendo.
Sawa lakini alitaka mchakato huo uchukue muda kwanza,yaani nchi zijiimarishe kipitia regional intergration,huu ilikuwa ni uoga wa kupoteza nafasi yake tu hakuna kingine,that time Nkrumah alikuwa na ushawish sana kuliko Nyerere kumbuka,na angegombea urais wa Africa angeshinda tu
 
ANDIKO LAKO nimelisoma pamoja na Mapungufu Mengi. Kutokujua historia vizuri., Kutokusoma vitabu ni changamoto sana.

1:Hoja ya Mwalimu ilikuwa ni kuunga mkono Jumuiya kama ECOWAS, COMES A, EACOMUNITY NK.

2: Lengo la kuua ucheef lilikuwa ni
a)KUTENGENEZEA umoja wa kitaifa. b)Kuwa na KIONGOZI mmoja.
c)kupambana na Ukabila nk.

3.Historia ya Muungano ni pana mno
TUKISEMA sababu za Muungano ni ilinzi na usalama, undugu na Zanzibar, nguvu ya ukomonisti, vita za kibepari.
Tutafika kesho.

Soma vizuri Historia Ya nchi MUOGOPE SANA NYERERE.
NDIO MYANZANIA WA KWANZA KUSOMA MASTERS NJE.

NYERERE ALIKUWA MTY MKUBWA MNO.
SOMA HISTORIA YA NCHI NA NYERERE VIZURI.
Kwenye history ya nchi na Nyerere ngoja Mzee wetu Mohamed Said aje
 
Kuna watu huwa wananishangaza kuwafananisha hawa viongozi wawili. Wanachofanana ni kitu kimoja tu, uroho wa madaraka. Huu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar hakuna agenda nyingine bali uroho wa madaraka, lengo likiwa kutawala nchi mbili. Tukija kwenye ishu ya kupiga marufuku uchifu hakuna kingine zaidi ya uroho wa madaraka, kupiga marufuku vyama vingi pia ni uroho tu wa madaraka, mpaka kijana wake akamuita madaraka.

Kuna mroho wa madaraka mwingine enzi hizo akiitwa Kwame Nkrumah wa Ghana, kwenye kikao cha Pan Africanism miaka ya 60 huko kidogo wazipige kavukavu na Nyerere, Kwame Nkrumah alitaka USA (United States of Africa) fasta fasta na yeye awe Rais wa hiyo State kama olivyo Biden kule USA ya America. Nyerere akawaza akaona atapoteza kiti chake maana hapa anaenda kuwa gavana, hizi nchi zote zingekuwa majimbo tu na marais wake wangekuwa magavana. Nyerere akainuka kitini akasema haiwezekani, hizi nchi zinatakiwa zijimarishe kikanda kwanza yaani regoonal intergration kama EAC,SADC,ECOWAS nk.
zitaunda hiyo USA taratibu taratibu, mjadala ilikuwa mkali kikaoni Nkrumah akazidiwa pwenti akataka kurusha ngumi, walinzi wakamdaka. Mwisho wa siku ndoto yake ikafeli akapinduliwa na kufa uhamishoni mwaka 1972.

Nyerere hakuwa mwizi, Nyerere hakuwa fisadi, Nyerere hakuwa na tamaa ya mali, kupenda kwake madaraka ni kwa vile alizaliwa kwenye familia ya kichief. Chief ni mfalme, mfalme hatoki kitini mpaka afe. Nyerere aking'atuka 1985 sio kwa kupenda bali maji yalimfika shingoni, shinikizo la wazungu lilimzidia.

Tuje kwa hayati JPM, huyu ni mroho wa madaraka, alivyokuwa akipata ubunge ni figisu hadaa na umafia wa hali ya juu. Kuzuia mikutano ya wapinzani, kutekana, nk ni uroho wa madaraka. Uroho wa mali nao si haba, akaunti yake kule China ina mabilioni kadhaa, bado kuna mabilioni yapo hapa nchini. Huo ndio utofauti wao na ufanano wao.

Kuna vitoto humu vinashangaa Lema na Lissu kukimbia nchi enzi za JPM. Ulizeni Oscar Kambona, rafiki wa karibu kabisa na Nyerere, alisomeshwa namba akajificha Uingereza miaka kibao.

Tuliosomea China tumeelewa kuwa mama Samia huwa anapita humu na kusema ningemkamata huyu mtoa mada ningemfinya mashavu

Yote umeandika kuntu lakini hili la madaraka mimi naona ipo hivi;
Magufuli hakuwa mroho wa madaraka bali alikuwa mroho wa mali kupitia madaraka, yaani madaraka ilikuwa ni njia yake ya kujichotea mali na ndio maana aliyanajisi madaraka.

Hivyo Nyerere alipenda madaraka na Magu alipenda mali.
 
Nyerere ndio chanzo cha matatizo tuliyo nayo kama nchi.

Katiba mbovu alijitungia yeye kwa manufaa yake binafsi.

Angeacha mfumo wa wakoloni uendelee kuanzia Elimu

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Kuhusu jina madaraka nilichomekea tu uko sahihi.
Lakini kuhusu machifu ukiangalia kwa jicho la tatu kulikuwa na hofu kw viongozi wa kiserikali kuzidiwa ushawishi na machifu.
Ilionekana watu wanawatii machifu kiliko wanasiasa, kupiga marufuku uchifu ilikuwa ni kujilinda tu kisiasa
Mdukuzi,unajua historia! Big up!
 
Back
Top Bottom