Mwalimu Nyerere alitukosea Sana

Mwalimu Nyerere alitukosea Sana

Restless Hustler

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
5,150
Reaction score
20,025
Mwalimu Nyerere ndiye aliyesimika lugha ya kiswahili kuwa ya Taifa.

Wengi watasema English ni lugha ya mkoloni lakini kiukweli ni lugha ya Maendeleo ya teknolajia na ustaarabu dunia. Mataifa Yote ya Afrika yanayotumia English Kama lugha ya Taifa, Yana Maendeleo makubwa ukilinganisha na yanayotumia kiswahili.

Chanzo Cha mkwamo wa Maendeleo ya Jamii na uchumi na wa Tanzania ni kuitumia kiswahili.

Kiswahili ni laana kwa Taifa. Angalia ukanda wote wa pwani kuanzia ghuba ya Aden, Mombasa, Tanga, Mtwara Hadi Sofala, japo Kuna mvua za kutosha, ardhi yenye rutuba na usafiri wa meli kwenda Ulaya na Asia lakini umaskini umeota mizi.

Mikoa yote yenye tamaduni za kiswahili zina Umasikini wa kutisha.

Hata mtu yeyote ambaye kiswahili ni lugha yake ya kwanza hata kama Ni msomi, Mara nyingi hapendi Maendeleo ya Watu na ni dramatic, majungu kazini. Ofisini kazi inakuwa ngumu kwa sababu ya upumbavu wa hali ya juu wa waswahili.

Nyerere Alitukosea Sana kwa kweli. Ningepata nafasi ya kimaamuzi ya Taifa, jambo la kwanza ni kufuta kiswahili kama lugha ya Taifa.
 
Mwalimu simdai kitu kwa kweli naweza kuzunguka Tanzania bila kubaguliwa kwa kabila langu wakati Nchi nyingi za Afrika wameweka ukabila mbele na unaweza hata kukosa huduma muhimu kwa sababu tuu sio kabila lao hapo Kenya kinachowasumbua ni ukabila tuu...
 
Mataifa mangapi yameendelea na wanatumia lugha zao?

Elimu mbovu hiyo changamoto, viongozi wabadhilifu, wachumia tumbo wenye kujali maslahi, hapo ndipo tunakwama kama taifa.
Ubinafsi sana umekithiri kwa watawala.
 
NYERERE WAS A GENIOUS OF TANZANIA ANGEWEZA KUWA DICTATOR ACHA UJINGA KUMDHARAU MWALIMU NDIO MAANA ATA NYUMBA YA BUTIAMA JWTZ WAMEMJENGEA USIMTUKANE MWALIMU KAMWE HE IS A GENIOUS OF TANZANIA
 
Kitu usichokijua ni kuwa kipindi nyerere anachukua nchi wazungumzaji wa Lugha ya kiswahili ilikuwa ni ndogo kulinganisha na wasiojua kukizungumza.
 
Kuna vijana wapumbavu sana, kila siku lawana kwa mwalimu, ukiwauliza wao wamelifanyia nini Taifa hawana hata moja la kukumbukwa .

AFRIKA HAIJAWAHI PATA KIONGOZI BORA ANAYETANGULIZA MASLAHI YA TAIFA MBELE ZAIDI YA MWALIMU.
 
Kaka ni ngum kuhusianisha umaskini na lugha fulani ishu ni mifumo mibovu ya serikali kuanzia kwenye elimu, utawala , biashara nk mfano china wao wanaongea lugha yao na wapo vzur sana kiuchumi
 
Back
Top Bottom