Mwalimu Nyerere anaishi katika sura ya Magufuli

nyerere aliwapiga wapinzani wake risasi ile mbaya nyerere alikuwa noma ni shaba tu.
 
Kama na wewe ni msomi, basi hakuna haja ya kwenda shule.
 
Usimlinganishe Nyerere na vitu visivyoeleweka.
Najua unauwezo mkubwa sana wa kuchambua mambo. Umejaribu kupitia huu uzi na kuuelewa vizuri?
Kichwa cha habari kinasema "NYERERE ANAISHI KATIKA SURA YA MAGUFULI
Hebu tuanzie hapo kwanza.
 
Kama na wewe ni msomi, basi hakuna haja ya kwenda shule.
Aise yamekuwa hayo tena!!! Mimi nijuavyo wasomi hujadili issues badala ya kujadili mtu. Je, unaweza kuja na hoja zenye nguvu ili tujadili kuhusu mada hii!!?
 
Nyerere ni namba ingine ile huwezi mlinganisha na mtu yeyote awaye. He was unique, focussed visionary and humble to the people
 
Mkuu hayo ya nyerere nimeyapata katika hotuba zake mwenyewe na ndio uhalisia...Chukua TRA,BRELLA,PCCB waende Kebby'S hotel wakakague tuone Kabula kapata wapi pesa za kujenga hotel na kama alikopa BANK aliweka dhamana ipi na kama likopa kama mfanyabiashara alikuwa anafanya biashara gani?

1.5T muulize CAG anajua kila kitu na yeye ndio aliotoa ripoti ya 1.5T haionekani,fuatilia bunge pesa ya nchi inatoka kama mtu anaenda k/kko kununua njungu mawe.
 
Nyerere alijua enlightenment philosophy, alisoma na kujadili sana falsafa Fabian Society Uingereza. Aliandika sana kuhusu John Stuart Mill.

Alijua kuishi na watu, kujenga ushawishi kwa kauli na matendo.

Kuna wakati Nyerere alikuwa anataka kufanya mambo yake kinyume na sheria, mwanasheria mkuu wa serikali, wakati huo Joseph Warioba, akamfuata na kumwambia mwalimu, hapo unavyoenda, ukifanya hivyo, serikali itakuwa inavunja sheria na kukutetea itakuwa vigumu. Nyerere akajirudi, akamsikiliza Joseph Warioba.

Pamoja na sifa yake kwamba "haambiliki", lakini alikuwa anaambilika, tatizo watu walikuwa wanamuogopa na alikuwa anapenda philosophical arguments, na watu wengi hawakutaka au kuweza mijadala naye.

Magufuli hataki mjadala, hajui enlightenment philosophies na nina shaka anamjua John Stuart Mill ni nani.

Sisemi Nyerere hana makosa, anayo mengi tu.

Lakini kumlinganisha a crude country bumpkin kama Magufuli na a world class statesman kama Nyerere ni kuonesha hujui sanaa wala sayansi ya kulinganisha vitu.
 
Haya unayoyasema ni maneno mazito sana. Nikisema hizo ni stori za vijiwe vya kahawa nitakuwa nimekosea?
 
Binafsi naishi maisha yangu; nafanya kazi, narudi nyumbani mapema, naangalia mipango yangu....nadhani vinanitosha.
 
Haya unayoyasema ni maneno mazito sana. Nikisema hizo ni stori za vijiwe vya kahawa nitakuwa nimekosea?
Kwahiyo wabunge wanaongea Story za vijiwe vya kahawa? Wabunge wanavyosema Fedha za kununua ndege haizjapitishwa na bunge ni story za vijiweni?

CAG alivyosema awamu ya 5 imepiga 1.5t nayo ni story za vijiwe?
 
Umejadili vizuri sana. Lakini kinachonishangaza zaidi ni kwamba wachangiaji walio wengi wamejiundia habari yao wenyewe.
Badala ya kujadili kilichopo mezani wameanza kujadili kitu tofauti.
Hebu tujikite kujadili masuala na tuone inakuaje.
Kwanza tukianza na kusimamia maadili ya utumishi wa umma.
Tunaona kabisa Rais wa awamu ya tano amejikita katika kusimamia maadali ya umma. Kadili ya siku zinavyozidi kusonga mbele watumishi wa umma wamekuwa wakiwajibika katika kazi zao.

Ukienda kwenye maofsi ya umma utaona kabisa uwajibikaji unaongezeka siku baada ya siku.
Hebu tuanze kwa hilo kwanza na kisha tuendelee. Tuachane na gilba na chuki zisizo na maana, kwa sababu hazijengi.
 
Wacha kukufuru wewe ndondocha wa lumumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…