Mwalimu Nyerere anaishi katika sura ya Magufuli

Baada ya danguro la billicanas kufungwa na biashara ya madawa ya kulevya kupigwa marufuku .

Majizi chadema watapata taabu sana awamu hii.
 
Usimfananishe nyerere na viru vya ajabu. Uongozi ni zaidi ya kufuata sheria na misingi.

Kuna kitu ambacho maguli anakosa sana, nayo ni busara na staha.. kifua cha kujua aongee nn na wakati gani. Daima hatakaa amkute nyerere kwa performance..
 
Leo ninawaletea ufafanunuzi wa mambo yanayoashiria ufanano wa kiutendaji kati ya Mwl Nyerere na Ndg Magufuli Mwkt wa CCM na Rais wa Tanzania, kwa kuwa viongozi hufananishwa na hutofautishwa kwa utendaji wao katika kutoa uongozi.

-Ukweli

Mwalimu mwanzoni mwa miaka ya 1960 alipojiuzulu Uwaziri Mkuu kwenda kujenga Chama nakumuachia Serikali Mzee Kawawa, aliandika vitabu vitatu kimojawapo ni TUJIJISAHIHISHE ni kitabu kidogo chenye kurasa zisizozidi ishirini ambapo amesisitiza katika kusema kweli na neno Kweli limetajwa zaidi ya mara ishirini.
"Ukweli unatabia moja nzuri sana, haujali mkubwa wala mdogo, haujali adui wala rafiki. Kwake watu wote ni sawa. Pia ukweli unayo tabia ya kujilipiza kisasi kama ukipuuzwa.."

Hayo ni baadhi ya maneno katika kitabu hicho, yanayosisitiza kusema ukweli na kuheshimu ukweli. Hii ni sawa kabisa kwa Magufuli ambaye toka awali amekuwa ni kiongozi anayesisitiza kusema ukweli na kwa sasa ni mwasisi wa msemo "Msema kweli ni mpenzi wa Mungu".

-Kusimamia Misingi

CCM ina msingi wa vitu viwili, Haki na Watu. Mwalimu mwaka 1968, akitoa hotuba aliyoiita, "Lazima Chama Kiwasemee watu" na moja ya kauli zake ni, "kazi ya Chama cha Siasa kilicho imara ni lazima kiwe kama daraja la kuwaunganiaha watu na serikali walioichagua." Mwalimu alisema akiwaasa viongozi wa Chama kuwa karibu na wananchi na kuwa watetezi wa haki za wanyonge.

Hiyo tunaishuhudia tena kwa Magufuli ambapo kwa kiasi kikubwa amekuwa akiwasisitiza viongozi wa Chama kuwa sikio la wananchi na hata mageuzi ya Chama yamelenga kukifanya kuwa "Chama Cha wanachama na kinachoshughulika na shida za watu"

-Falsafa ya kazi

Mwaka 1976 Mwalimu aliandika kitabu "kila mtu afanye kazi" kinachoeleza kwa undani umuhimu wa kazi katika maisha binafsi na kwa taifa. Sasa ni miaka 40 Magufuli amekuja na falsafa inayofanana ya "Hapa Kazi Tu".

- Sera ya Viwanda na Kilimo

Mwalimu aliweza kuanzisha programu za kilimo ikiwemo "utekelezaji wa siasa ni kilimo" - 1974, sera ya viwanda vidogo vidogo (SIDO), vya kati ikiwemo viwanda vya nguo urafiki, Mwatex, Mutex, Mbeyatex, n.k Sawa kabisa na Magufuli ambaye ndoto yake ni Viwanda. Miezi miwili iliyopita amezindua mradi mkubwa wa kilimo awamu II utakaogusa maisha ya wakulima wadogo kwa kuwapatia mikopo nafuu ya kilimo.

-Udhibiti wa madini

Katika suala la madini Mwalimu alifanya utambuzi wa maeneo yenye madini, hakuruhusu uchimbaji uanze mbali na changamoto tulizokuwa tukizipitia kama Taifa, kwa kuwa Watanzania hatukuwa na elimu ya kutosha ya Madini. Magufuli amekuja amekuta mikataba kandamizi iliyoingiwa na watangulizi wake baada ya mwalimu hivyo ameifumua mikataba yote ya Madini na kufanya haki ya mtanzania kuheshimiwa na kuweza kuingia makubaliano kutoka 3% ya awali mpaka 50/50%.

- Reli, Umeme na Anga.

Mwalimu aliweza kujenga Reli ya TAZARA miaka ya 1970, kwa upande mwingine alikuwa na ndoto kubwa ya ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme maarufu kama Stiegler's Gorge ambao ulikwamishwa, shirika la ndege lilikuwa na ndege za AirTanzania kabla halijafa katika awamu zilizofuata. Miaka 30 sasa Magufuli amefufua shirika la ndege na mpaka sasa serikali imefanikiwa kununua ndege Saba ndogo za kati na kubwa. Ujenzi wa Reli ya kisasa unaendelea naujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Stiegler's Gorge umeanza.

Vijana wa miaka ya 1990, Nyerere tunayesimuliwa nakumsoma amerejea katika sura ya Magufuli na ni jukumu letu kumpa ushirikiano na kufanya naye kazi kuhakikisha tunatekeleza na kufikia ndoto ya TViwanda.

Na mwandishi wetu,
Said Said Nguya
[email protected]
Ptuuu!
 
Haya unayoyasema ni maneno mazito sana. Nikisema hizo ni stori za vijiwe vya kahawa nitakuwa nimekosea?
Umeambiwa ya Kebby's hotel unasema ni porojo. Lakini uliyoandika wewe unataka kila mtu ayaamini kama msaafu. Naomba unijulishe haya:-
1.Je, hii Kebby's hotel inayosemwa ipo Dar au haipo?
2.Je, mmiliki wake ni Bibie Kabula au anasingiziwa?
3.Je, aliwahi/ana mahusiano na huyo unayemsifia au hana?
 
Leo hii mada imewapoteza kwenye njia michadema.
 
Huo muda uliopoteza kuandika huu utakotako wako ungefanya kitu productive ungekuwa mbali!!
 
Sasa tukija kwenye huduma za kijamii. Kuongeza bajeti za afya, elimu na kusukumwa kwa nguvu usambaji wa maji na hilo kwako ni baya tu?
Kwanza kabisa, umekubali kwamba Magufuli hafai kulinganishwa na Nyerere kwa sababu Magufuli anashindwa mtihani wa msingi kabisa wa uongozi, wa kauli ambazo zina staha za kiuongozi? Unakubali hili?

Sio unarusha mjadala sehemu nyingine kabla hujamaliza moja.

Unataka kumlinganisha Nyerere, aliyemsomesha Magufuli na kumpa nafasi ya kuweza kufanya hayounayoyaona mazuri, na Magufuli aliyesomeshwa na serikali ya Nyerere?

Wewe kwa akili yako unaona ufananisho huo uko sawa kabisa?
 
Hii ni ripoti ya mwaka jana tu je unaiongeleaje?

1280px-GPI_2017.jpg
Umekubali Magufuli kashindwa kujieleza kwa staha inayofaa kwa mtukwangazi yake ya uongozi?

Serikali ya nchi yenye mbunge wa upinzani anayepigwa risasi kama target kwenye target practise utasemajeinajivunia amani?
 
Hakuna mada ya kujadili mkuu Nyerere na JPM wapi na wapi mkuu? Nyerere hakuzuia mikutano ya siasa,Nyerere aliunga sera za vyama vingi ingawa baadhi ya washauri wake walimwambia akatae kwa sababu waliokubali walikuwa 20% lakni nyerere hakuwapuuza hao 20%,Nyerere aliktaaa kuishi kwenye jumba la milioni 100 aliyojengewa alitaka aishi kwenye nyumba yake ya kawaida,Nyerere hakuwahi kujengea kimada hotel,nyerere hakugawa vyeo kama njugu kwa mademu na wapiga ngenga wakumsifia,nyerere hakuiba fedha za serikali kama 1.5T ilivyopigwa,Nyerere hakufanya manunuzi ya serikali bila kushirikisha bunge,Nyerere hakuwapa nafasi wanae kwenye serikali yake ,Nyerere haku .......Mambo ni mengi sana mkuu,NDIO maana nikakwambia Weka Namba ya simu ugewe Shavu,Awamu hii wewe jitoe akili tu sifia wewe sifia siku utakuja stukia unapigiwa simu umekuwa DAS ndio maana nikakushauri weka namba ya simu.
Nimekupenda bure kabisa kwa ukweli huu
 
Kwahiyo wabunge wanaongea Story za vijiwe vya kahawa? Wabunge wanavyosema Fedha za kununua ndege haizjapitishwa na bunge ni story za vijiweni?

CAG alivyosema awamu ya 5 imepiga 1.5t nayo ni story za vijiwe?
Chato International Airport
 
Acha kumfananisha baba wa taifa na muuaji wa wanasiasa
 
Humtendei haki baba wa taifa hayati mwalimu J.K. Nyerere. Yule anafananishwa na akina Kwame Nkurumah, Patrice Lumumba, Martin Luther King, Mahatma Gandhi, Nelson Mandela, Mother Teresa japo hakuwa mwanasiasa, Indira Ghandhi, Fidel Castro, na wengine wanaofanana na hao.
 
Back
Top Bottom