Herymiller
JF-Expert Member
- Jul 8, 2018
- 612
- 861
Hakuna mwenye muda mchafuSiyo mbaya uka subscribe kisha baadaye ukiwa umetulia ukapitia taratibu. Maana mchango wako ni muhimu.
Magufuli msema ovyo hajui maana ya neno maadili, hivyo hawezi kusimamia maadili.Umejadili vizuri sana. Lakini kinachonishangaza zaidi ni kwamba wachangiaji walio wengi wamejiundia habari yao wenyewe.
Badala ya kujadili kilichopo mezani wameanza kujadili kitu tofauti.
Hebu tujikite kujadili masuala na tuone inakuaje.
Kwanza tukianza na kusimamia maadili ya utumishi wa umma.
Tunaona kabisa Rais wa awamu ya tano amejikita katika kusimamia maadali ya umma. Kadili ya siku zinavyozidi kusonga mbele watumishi wa umma wamekuwa wakiwajibika katika kazi zao.
Ukienda kwenye maofsi ya umma utaona kabisa uwajibikaji unaongezeka siku baada ya siku.
Hebu tuanze kwa hilo kwanza na kisha tuendelee. Tuachane na gilba na chuki zisizo na maana, kwa sababu hazijengi.
Njaa imempanda kuchwaninyie CCM kweli mmerogwa.
yaani mnamfananisha Mwalimu (GT) na vitu gani hivi??!
Anafananisha usa na rwandaHakuna mada ya kujadili mkuu Nyerere na JPM wapi na wapi mkuu? Nyerere hakuzuia mikutano ya siasa,Nyerere aliunga sera za vyama vingi ingawa baadhi ya washauri wake walimwambia akatae kwa sababu waliokubali walikuwa 20% lakni nyerere hakuwapuuza hao 20%,Nyerere aliktaaa kuishi kwenye jumba la milioni 100 aliyojengewa alitaka aishi kwenye nyumba yake ya kawaida,Nyerere hakuwahi kujengea kimada hotel,nyerere hakugawa vyeo kama njugu kwa mademu na wapiga ngenga wakumsifia,nyerere hakuiba fedha za serikali kama 1.5T ilivyopigwa,Nyerere hakufanya manunuzi ya serikali bila kushirikisha bunge,Nyerere hakuwapa nafasi wanae kwenye serikali yake ,Nyerere haku .......Mambo ni mengi sana mkuu,NDIO maana nikakwambia Weka Namba ya simu ugewe Shavu,Awamu hii wewe jitoe akili tu sifia wewe sifia siku utakuja stukia unapigiwa simu umekuwa DAS ndio maana nikakushauri weka namba ya simu.
Anapalilia uteuziUsichoshe akili za watu kwa maslahi unayohitaji wewe, Nyerere hawezi kufanana hata kidogo na huyo unayempigia chapuo, kinachoonekana una mahaba tu na huyo unayemtaja, lkn ukweli unabaki ukweli kuwa hawafanani hata kidogo, unachotaka kufanya ni kushusha hadhi ya Mwl Nyerere
Nadhani umejikita katika eneo hilo la kuongea uonavyo wewe.Kwahiyo wabunge wanaongea Story za vijiwe vya kahawa? Wabunge wanavyosema Fedha za kununua ndege haizjapitishwa na bunge ni story za vijiweni?
CAG alivyosema awamu ya 5 imepiga 1.5t nayo ni story za vijiwe?
Point haiwezi kutolewa na chumia tumbo kama weweHebu nakuomba utulie uwenze kuandika vizuri.
Nakuomba tujadiliana point kwa point bila kuandika vitu kwa hisia tujadiliane kama wasomi.
Je, haya unayoyasema umeyapata wapi? Kama msomi unaweza kutupatia references ya haya unayoyasema kutoka credible source?
Injaa imekupanda kichwaniNadhani umejikita katika eneo hilo la kuongea uonavyo wewe.
Kwanza kabisa nakuomba tujadili sasa kwa kina kuhusu suala la ununuzi wa ndege.
Ununuzi wa ndege ni suala lililopigiwa kelele muda mrefu na wanasiasa kuhusu shirika la ndege linakufa.Sasa sielewi upande wako sasa unasimamia nini. Maana suala hili ni zuri na litaleta faida mtambuka katika nchi.
Tunaweza tukaongeza pato la taifa kupitia utalii maana watalii watakuwa wanakuja moja kwa moja katika nchi yetu.
Halafu ifahamike kwamba shirika la ndege ni neno ya taifa kwenye anga za kimataifa. Sasa basi tutakuwa tunalitambulisha taifa letu kwatika anga za kimataifa kupitia shirika letu la ndege. Hiyo itavutia watu kuja kutembelea nchi yetu na wengine kufanya uwekezaji.
Tukija kwenye suala la hiyo pesa unayosema tayari CAG alishalitolea ufafanuzi labda imebaki tu husda kwa watu wachache wenye nia mbaya na nchi yetu.
Nadhani umejikita kutumia maneno mabovu mabovu.Magufuli msema ovyo hajui maana ya neno madili, hivyo hawezi kusimamia maadili.
Tofautisha kutisha watu na kuwaonesha "there is a new sherrif in town" kwa kutumia karata ya maadili na kusimamia maadili.
Magufuli angejua na kujali maadili ni nini, angeanza kuongea maneno kama mtu anayejali maadili.
Sasa hivi uharo wake wa mdomo hauwezi kumfanya mtu anayefuatilia maadili kusema Magufuli anajali maadili.
Kaongea vibaya sana kuhusu kupiga shangazi za watu, kuwapa rushwa trafiki, kuingilia uhuru wa mahakama, bunge na serikali za mitaa, na ujinga mwingine mwingi sana ambao haufuati maadili.
Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete pamoja na mapungufu yao yote, hawakufikia uharo wa mdomo anaouonesha Magufuli sasa hivi.
Hayo si maadili.
Huwezi kurudisha maadili serikalini kama hata kauli yako tu huwezi kuidhibiti.
Si mimi niliyeanza kutumia maneno mabovu.Nadhani umejikita kutumia maneno mabovu mabovu.
Nadhani kuna kundi lilikuwa na mazoea ya kuishi nyakati za nyuma. Zama zimebadilika inabidi kundi hilo libadilike katika kuwaza.
Hata hivyo kutumia maneno mabovu katika comment haisaidii chochote. Kinachotakiwa ni kujadili hoja.
Nimekuwekea hoja mezani kwamba. watumishi wa umma kwa sasa wanawajibika ipasavyo. Ukienda kwenye ofsi za umma utaona kabisa mabadiliko yanayoleta faraja katika nchi.
Ilakuna baadhi ya watu waliokuwa wamezoea kuishi katika maisha ya rushwa na ufisadi hakika hawataweza kumpenda. Na kwa bahati nzuri kundi hilo ni dogo sana.
Sasa tujikite kwenye mada kujadili maadili ya watumishi wa umma. Kufanya kazi ipasavyo kwa faida ya taifa zima.
Naam.
Sasa tukija kwenye huduma za kijamii. Kuongeza bajeti za afya, elimu na kusukumwa kwa nguvu usambaji wa maji na hilo kwako ni baya tu?Si mimi niliyeanza kutumia maneno mabovu.
Natumia maneno unayoweza kuyaita mabovu kwa sababu naelezea ubovu wa maneno mabovu ya Magufuli.
Unakataa kwamba Magufuli anaongea maneno mabovu yasiyofaa kimaadili kwa rais?
Rais anayeongea kuhusu kupiga shangazi za watu unaweza kusema anajua maadili?
Hii ni ripoti ya mwaka jana tu je unaiongeleaje?Naam.
Magufuli asingekuwa country bumpkin, angejua hakuwa na haja ya kuongea habari za kupiga shangzai za watu.
Taifa lina tatizo la violence, watu wanapiga wake zao, etc.
Rais anatakiwa kuwa the voice of reason kukemea violence.
Yeye badala ya kukemea violence, anakuwa mtetezi wa violence.
Kwa sababu ni country bumpkin.
Umeandika utumbo hakuna vya kulinganisha hapo, point kwa point zipi? Nyerere aligigia promo sana "critical thinking". Utamlinganisha na jiwe anayefanya majaribio kila uchao kuua critica thinkers?Hebu nakuomba utulie uwenze kuandika vizuri.
Nakuomba tujadiliana point kwa point bila kuandika vitu kwa hisia tujadiliane kama wasomi.
Je, haya unayoyasema umeyapata wapi? Kama msomi unaweza kutupatia references ya haya unayoyasema kutoka credible source?