Mwalimu Nyerere hakuishinda Serikali ya Kikoloni kwa maandamano, alitumia akili. CHADEMA ipo kwenye njia sahihi?

Mwalimu Nyerere hakuishinda Serikali ya Kikoloni kwa maandamano, alitumia akili. CHADEMA ipo kwenye njia sahihi?

Big Shaman

Member
Joined
Dec 22, 2014
Posts
22
Reaction score
73
Kulikuwa na vyama viwili TANU & UTP, Baada ya kushinda ubunge akaenda UN kuishtaki UTP iachie nchi, akashtakiwa kwa uhaini na kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara, akajiweka karibu na mkoloni TANU ikashinda majimbo 70/71.

Je, kwanini Nyerere hakuitisha maandamano kuindoa serikali ya kikoloni?
 
Kama mama ameahid katiba mpya hata mm ningejifanyajinga kama mbowe ili ipatikane
Nyie mnamuona mbowe fala hamtak awe kondoo lin maanaadamano yalileta katiba mpya? Wangap mko tayal kuandamana? Siasa za kutukana jukwaan zimewahi saidia lini?
Mbowe ametumia akili jifanye mjinga acha wakutukane ili lengo lako litimie na likitimia utakuwa na uwezo wa kushinda uchaguzi
 
Serekali ya muingereza walikabidhiwa Tanganyika na UN hadi tutakapokuwa tayari kujitawala. Sasa maandamano ya nini wakati muingereza alipewa Tanganyika kama nyongeza?
 
Wacha Mbowe aonekane mjinga kwa wajuaji lakini aseme hivi mbele ya Samia.
FqtCSZoXwAAiYYk.jpg
 
Independence was inevitable, we weren't the first or the last to get it from the Brits. The British empire was crumbling, it was just a matter of time.

On the contrary, CCM can rule forever! They are stronger and smarter than the opposition.
 
Kulikuwa na vyama viwili TANU & UTP, Baada ya kushinda ubunge akaenda UN kuishtaki UTP iachie nchi, akashtakiwa kwa uhaini na kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara, akajiweka karibu na mkoloni TANU ikashinda majimbo 70/71.

Je, kwanini Nyerere hakuitisha maandamano kuindoa serikali ya kikoloni?
Tabganyika was a protectorate! Tulikuwa tunaagaliwa na kuandaliwa kujitawala..... sema Nyerere aliwaharakisha wakiwa bado wanaitaka Tanganyika. Tanganyik was not a colony
 
Kama mama ameahid katiba mpya hata mm ningejifanyajinga kama mbowe ili ipatikane
Nyie mnamuona mbowe fala hamtak awe kondoo lin maanaadamano yalileta katiba mpya? Wangap mko tayal kuandamana? Siasa za kutukana jukwaan zimewahi saidia lini?
Mbowe ametumia akili jifanye mjinga acha wakutukane ili lengo lako litimie na likitimia utakuwa na uwezo wa kushinda uchaguzi

Umeandika mengi ya msingi,kongole kwa hilo ndugu Mubby777 ,lakini umepuyanga ulivyoandika kuwa lengo la Mbowe ni kushinda uchaguzi ndio ninapokupinga.

Lengo la ndugu Mbowe ni kuwe na maisha bora kwa kila Mtanzania.
Maisha bora kwa kila Mtanzania yatapatikana tu kwa kuwa na katiba bora inayotoa miongozo na uwajibikaji kwa watendaji wa serikali.

Hilo naamini ndilo analolipigania ndugu Mbowe na "wapinzani" wote wa serikali inayokuwa madarakani.

Katiba Mpya ni kwa ajili ya kuweka mazingira bora sana ya kuipeleka Tanzania kwenye nchi ambayo kila mwananchi atakuwa na ujasiri wa kuitetea na kuitumikia Tanzania kwa moyo wake wote akiamini kuwa kila Mtanzania atanufaika na upendeleo wa Mungu Baba Muumba wa kuipa Tanzania rasilimali za kila aina tofauti na nchi nyingi za dunia yetu.
 
Ili kushinda kuna njia mbili tu moja ni ya maridhiano na mazungumzo au ya pili ni ya kumwaga damu, ipi ingefaa ifuatwe na chadema kufikia malengo, kwa kuzingatia historia ya nchi hii kabla na baada ya uhuru tujadili!
 
Back
Top Bottom