Mwalimu Nyerere: Hii Katiba ya Tanzania, tukimpata Rais asiye na busara anageuka kuwa Mungu

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?
Mzee aliyajua.....na sasa tumempata pogba ambae ni busaraless
 
Katiba ya USA iliandikwa mwaka 1787 na inatumika mpaka leo. Mwl Nyerere na uwanafalsafa wake wote alichokishindwa ni kutuachia katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi. Ila kutuambia eti akija mtu mwenye nia tofauti katiba haifai ni udhaifu mkubwa. But kila kitu alichofanya nyerere kinaonekani ni chakishujaa
Call a spade a spade plz.
sio kila kilichotamkwa na nyerere ni cha kishujaa/busara.
Hili la katiba mwl. yupo sahihi kabisa.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?
Nakubaliana naye kwa asilimia nyingi......

Kitu cha kushangaza clip ya speech hiyo ya busara sana, stations zote za TV ni kama wamepigwa mkwara wasiiweke kwenye TV stations zao na ndiyo sababu hatuisikii wala kuiona kwenye TV station yoyote!

Katiba yetu ya nchi inamwezesha Mkuu wa nchi kuendesha nchi kwa staili ya ONE MAN SHOW.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?
Kwa nini hakufanya mchakato wa mabadiliko ya katiba ili impunguzie madaraka kwa kwa kipindi hicho?
 
Katiba ya USA iliandikwa mwaka 1787 na inatumika mpaka leo. Mwl Nyerere na uwanafalsafa wake wote alichokishindwa ni kutuachia katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi. Ila kutuambia eti akija mtu mwenye nia tofauti katiba haifai ni udhaifu mkubwa. But kila kitu alichofanya nyerere kinaonekani ni chakishujaa
JKN hapa ametuingiza chaka-kwa faida ya nani siku zote najiuliza! Nahisi alijua ni kwa faida ya watawala. ??????????????? Na hata vyama vingi vilipoanzishwa aliliona hili na hakuchukua hatua yeyote-alijua likatiba hili litawasaidia watawala ambao si wengine bali CCM. Likatiba hili limetumiwa na hata Jecha kufanya yake achilia mbali maraisi mbalimbali waliotufanyia. Naambiwa huwezi kuwashitaki-wengine hadi banki kuu wametoa fedha, wameidhinisha malipo kutoka escrow wanatuambia siyo pesa zetu lakini Tanesco inalipa madeni kwa kutumia pesa zetu, wanapiga mikutano ya siasa marufuku na hapo hapo wanatukejeli kuwa tutaisoma namba. Chaguzi ndio wanajua wenyewe wanaziendesha vipi.
 
  • Thanks
Reactions: ydn
Busara Zipi kwa kuitengeneza Katiba na kutuachia , akijua kuwa ni bomu?

think out of the box
Umlaumu au vyovyote vile, sasa hayupo. Ila ujumbe aliyoutoa upo, swali la msingi ni tunautumiaje?
 
Nakubaliana na wewe, Mzee
Katiba ya USA iliandikwa mwaka 1787 na inatumika mpaka leo. Mwl Nyerere na uwanafalsafa wake wote alichokishindwa ni kutuachia katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi. Ila kutuambia eti akija mtu mwenye nia tofauti katiba haifai ni udhaifu mkubwa. But kila kitu alichofanya nyerere kinaonekani ni chakishujaa

Nakubaliana na wewe, Mzee Mandela aliona mbali na akaiacha nchi yake katiba ambayo haiwezi kuchezewa na kufinyangwa finyangwa kwa matakwa ya kiongozi aliyepo madarakani ndiyo maana Zuma anaona kiti cha moto. Kinachomtia kiwewe ni katiba ambayo inalinda maslahi ya taifa na siyo matakwa na utashi wa aliyekalia kiti cha urais.
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa hii katiba yetu, inampa mno madaraka makubwa sana, mwalimu alisema kuwa kama tukimpata Rais asiyekuwa na busara, kwa katiba hii Rais anageuka kuwa mungu, unakubaliana na kauli ya mwalimu Nyerere?

huyo itakuwa Mwalimu wa Nursery School...ila kama ni Mwalimu nyerere itakuwa alisema Mungu...na sio mungu
 
Back
Top Bottom