punguza povu acha kujitekenya jibu hoja hapo mkuu, me sijatukana popote, ...acha kunikusingizia mkuu...jibu maswali yangu..sikatai na wala sitakataa , kuwa yeye ni kiongozi wa nchi hii hilo liko wazi , swali langu ni hili je aliiacha na hivo vote unavosema tanzania hii? kama aliviacha je alimuachia nani wakati mzee mwinyi alitoa hutuba kuhainisha haya?
walokuwepo enzi za Nyerere wtashuhudia maneno yangu,
NYERERE NI MWOKOZI na NABII wa Afrika na Tanganyika, mfano Yesu aliponya watu magonjwa yao, aliwasaidia wenye shida na Nyerere alilisha watu kwa aina yake, alilisha watu wengi kuliko Yesu, NYRERE enzi zake alijenga viwanda vya nguo vya Mwatex, Mutex, Urafiki, Sungura na Kilimanjaro, watu walipata ajira, walikula wakashiba, kwenye michezo Enzi za Mwalimu timu ya taifa ilikuwa moto wa kuotea mbali, wachezaji wengi wa timu ya taifa ya wakati huo walitokana na timu ya Pamba, enzi za Mwalimu kulikuwa na Shirika la Reli, Shirika la Posta, Benki ya NBC, TAZARA, ifuko ya hifadhi ya jamii,
PPF na shirika la Akiba ya Wafanyakazi
[National Provident Fund] leo hii ndo shirika la Hifadhi ya Jamii
[NSSF], Enzi za Mwalimu kulikuwa na viwanda vya korosho kila sehemu kunakolimwa korosho, kulikuwapo viwanda vya kuzalisha zana za kilimo na uvuvi, viwanda vya sukari, kama Kilombelo I na Kilombelo II, Mtibwa, TPC, Mgodi wa Almas, viwanda vya tumbaku vya Tabora na Morogoro, Mamlaka za Tumbaku, Mkonge, Pamba, Kahawa, Korosho, Mamlaka ya chai, Nyerere huyu au MWOKOZI WA TANGANYIKA na AFRIKA alianzisha mashirika na makampuni ya umma kama kampuni ya Ngombe wa maziwa
(DAFCO), kampuni ya ngombe wa nyama
(NARCO) National Insurance Coperation, Shirika la Sukari
(SUDECO) Shirika la Maendeleo
(NDC) Shirika la Usagaji National Milling Coperation, Shirika la Umeme
(TANESCO) Mamlaka ya Madawa, Board ya biashara ya ndani, Board ya biashara ya nje, Board ya Utalii, Shirika la ndege Tanzania (Air Tanzania) Benki ya Rasilimali
(TIB) Benki Kuu (BOT) nk.
SWALI LA KWAMBA ALIMUACHIA NANI TUMUULIZE MZEE WA RUKSA.
Mkuu siku zote mtu mwenye maarifa, hekima na busara, anatamani kuwa na karama kama za Mwalimu, maana hekima, busara na maarifa aliyokuwa nayo Nyerere ni mwongozo tosha wakumwongoza binadamu kufikia maisha bora yenye mafanikio, Nyerere hakuwa malaika, jambo ambalo hata yeye mwenyewe alilifahamu ndo maana alikuwa akiwaasa watanzania kuachana na mapungufu yake yote, na tuchukue mema yote, km mmeshindwa au tumeshashindwa wananchi kudai KATIBA ni makosa yetu si ya Nyerere, km ulikuwa ukitegemea Nyerere akufanyie kila kitu umefeli, alifanya alipoweza kadri Mungu alivyomjalia , dunia na watanzania wanajua juhudi zake kwa nchi yake, TUACHE KULALAMA NYUMA YA KIBODI, MWACHENI MZEE WA WATU APUMZIKE