Mwalimu Nyerere: Hii Katiba ya Tanzania, tukimpata Rais asiye na busara anageuka kuwa Mungu

Mwalimu Nyerere: Hii Katiba ya Tanzania, tukimpata Rais asiye na busara anageuka kuwa Mungu

Kama yy aliona katiba inampa rais kua mungu mtu na yy ndie aliekua raise mbona akubadili katiba ili kumuondolea kazi kubwa rais? Asitueke Watanzania kama wapofu wa macho. Yeye ndio aliusika na katiba mbovu tulio nayo.
Hata wewe mkuu ukiwa madarakani huwezi kuona kama katiba ni mbovu, marehemu Mkapa kwenye kitabu chake alitaka kuwe tume huru ya uchaguzi lakini kwenye awamu yake alikuwa anaona tume ni huru.
 
Kama aliliona hilo kwanini hakuanza kufanya mchakato wa marekebisho ya katiba maana katiba iliyopo ya mwaka 1977 yeye mwenyewe aliitia saini kwa maana aliridhika nayo.

Wala hakuna haja yakumsifia kwa kutamka tu maneno hayo ilitakiwa aibadilishe yeye akiwa madarakani.
 
Kama yy aliona katiba inampa rais kua mungu mtu na yy ndie aliekua raise mbona akubadili katiba ili kumuondolea kazi kubwa rais? Asitueke Watanzania kama wapofu wa macho. Yeye ndio aliusika na katiba mbovu tulio nayo.
Nyerere ana share kubwa ya matatizo tuliyonayo. Sitegemei kama ataupata utakatifu
 
Kwa kukosa neno bora zaidi nadhani kuna unafiki kidogo hapa. Nyerere alikuwa na nafasi ya kipekee ya kuweza kuwaachia watanzania katiba bora nakutoa vipengele vyote ambavyo kwa maoni yake yanamfanya rais awe dicteta. Kuna sababu za msingi kwake yeye kuongoza nchi changa kwa kutumia katiba hiyo hasa ubaguzi wa kikabila, rangi na dini.

Ili kuondokana na mambo hayo kulikuwa na haja ya kuwa na udicteta. Lakini baada ya miaka zaidi ya 20 ya uongozi wake uliofanya kazi nzuri sana ya kuondoa mambo hayo. angeweza kabisa kufanya marekebisho badala ya kutuachia dude hili ambalo sasa linatula na kutumika kutukandamiza.
 
Mwalimu alikuwa na imani kubwa mno kwa watanzania wake maskini Mzee wa watu kiasi kwamba hakuamini kuwa anaweza kutokea kiongozi mtanzania akafanya hayo aliyoyasema kuhusu katiba.

Imani kubwa kwa watanzania ndiyo iliyomfanya asibadikishe katiba wakati yeye anang'atuka 1984.

Ni kweli jambo hili linatughalimu sana watanzania tena kwa kiasi kikubwa mno. Tumeingizwa kwenye utamaduni ambao hatukua nao kabla. Utamaduni wa ukabila, kuchukiana, kupotezwa, kutekana, kujeruhiana ama hata wa kuuawana.

Kwa sasa hivi kama ukichoka kuishi uraiani wewe mkosoe Rais wako. Sasa huu si uhuru baba zetu waliupigania kuupata miaka ya 60 toka kwa wakoloni.

Ni wakati umefia sasa iwe mvua ama jua..iwe kwa jasho ama damu kunadilisha katiba hii maana hatujui 2025 atakuja wa sampuli gani nyingine.

Watanzania amkeni, katiba ni mali yenu.
 
Kwa kukosa neno bora zaidi nadhani kuna unafiki kidogo hapa. Nyerere alikuwa na nafasi ya kipekee ya kuweza kuwaachia watanzania katiba bora nakutoa vipengele vyote ambavyo kwa maoni yake yanamfanya rais awe dicteta. Kuna sababu za msingi kwake yeye kuongoza nchi changa kwa kutumia katiba hiyo hasa ubaguzi wa kikabila, rangi na dini.

Ili kuondokana na mambo hayo kulikuwa na haja ya kuwa na udicteta. Lakini baada ya miaka zaidi ya 20 ya uongozi wake uliofanya kazi nzuri sana ya kuondoa mambo hayo. angeweza kabisa kufanya marekebisho badala ya kutuachia dude hili ambalo sasa linatula na kutumika kutukandamiza.
Mwalim Nyerere amefariki siku nyingi sana. Na sisi tumeshapata muda mrefu sana wa kubadilisha hiyo katiba. Ilitakiwa viongozi watafakari maneno aliyosema na kubadilisha. Kumlaumu sasa hivi ni kama kulaumu ulikoangukia badala ya ulikojikwaa. Ni kama kumlaumu baba aliyefariki na kumwachia mwanae urithi wa shamba na yeye badala ya kulima apande mazao akabaki kumlaumu baba yake ni kwanini hakulima kabisa kabla hajafa.
 
Nyerere is overrated
Katiba ya USA iliandikwa mwaka 1787 na inatumika mpaka leo. Mwl Nyerere na uwanafalsafa wake wote alichokishindwa ni kutuachia katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi. Ila kutuambia eti akija mtu mwenye nia tofauti katiba haifai ni udhaifu mkubwa. But kila kitu alichofanya nyerere kinaonekani ni chakishujaa
 
Sasa kama alilijua hilo yeye Nyerere alifanya nini kuondoa hilo tatizo?

By the Way katiba hii hii si iliandikwa kipindi cha utawala wake?
Fikiria mambo mawili kwanza:

Matatizo yote ya nchi yot! aliyapa kipaumbele sawia na chanzo chake na ugumu wake! vilevile na manufaa yanayopatikana humo! hili lilikuwa ni tatizo la 259 katika mambo aliyotaka kuyafanya mapema zaidi!!

alipooongelea km ulifuatilia hotuba yake ya usiku ule ailtamka litaangaliwa na kurekebishwa upya!! lkn akaacha madaraka mapema! akawapa waliomfuatia mikakatai ya ufuatiliaji hawakufanya waliona lita wafaa! jua Rais akisema atafanya tu!

.............nakuja kwanza
 
Sasa kwa nini asingefanya mchakato wa kuibadilisha wakati alipokuwa madarakani?
 
Back
Top Bottom