Mwalimu Nyerere kwanini alichagua Twiga? Ni Mnyama dhaifu sana!

Mwalimu Nyerere kwanini alichagua Twiga? Ni Mnyama dhaifu sana!

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Posts
22,584
Reaction score
27,817
Nijuavyo mimi Dunia nzima Kihistoria nchi zimekuwa zikichagua Wanyama kama alama inayowawakilisha, yaani unaweza kusema mnyama wa nchi, na wengi hapa huchagua mnyama mwenye sifa ya UKUU na UTAWALA, ndo maana nchi nyingi kubwa kama Ujerumani, USA, na Falme nyingi kubwa Duniani wamekuwa wakichagua ndege Tai, huyu ana sifa za ajabu kama nguvu, uvumilivu, ufanisi na pia mwendo mkali kwa kifupi anatawala anga, kwanza wanasema Tai anaweza kuishi mpaka miaka 70, huku kwetu kwa nini hatukuchagua Simba? Huyu Twiga ana nini? Twiga ni alama ya Udhaifu, na hakupaswa kuwa alama ya kutuwakilisha.

Simba ndo Mfalme na mwamba Nyika, hata kwenye Biblia na vitabu vingine vitakatifu sijaona mahali Twiga akitajwa isipokuwa Simba au Ndege Tai, ...

Mfalme wa Anga Tai- USA, Ujerumani na Falme kubwa Duniani!

1572634772387.jpeg


Urusi brown bear.

1572634872120.jpeg


Huyu ndo alifaa awe alama yetu, Simba Mfalme wa Nyika na siyo huyo twiga wenu, kwanza analiwa na Simba!
1572635034103.jpeg
 
Leo nakuunga mkono wewe mwana Lumumba, kweli tulitakiwa kuwa na nembo ya mnyama mwenye nguvu ma akili. Nahisi twiga katufanya tumekuwa wapole kama tulivyo
 
Alikuwa na maana nzuri Twiga ni mrefu kuliko wanyama wote anaona mbali na hatari za mbele.
Na ndio maana porini Twiga akihamaki na kuanza kukimbia wanyama wengine kama nyumbu na pundamilia wanamfuata wanajua kuna hatari inakuja mfano simba niliona hii Mikumi.
Sasa Nyerere alikuwa na maono ya mbali mno kabla hayajatokea.Na ndio maana kuna mambo alituasa kuhusu ukabila na udini taratibu yanaanza kujitokeza.
Alituasa kuhusu hatari ya kutawaliwa na mabeberu kifikra japo tuko huru.Hii tunaona jinsi mataifa makubwa yanavyojaribu kupangia nchi changa cha kufanya mfano kutufundisha demokrasia mfano mwingine kulazimishwa kukubali mapenzi ya jinsia moja.
RIP Mzee Nyerere
Screenshot_2019-11-01-22-26-48-1.jpeg
 
Umechunguza kwa karibu sifa zote za twiga?? Madhaifu ya Tai je?? Ya Simba je?? Hujiulizi kwanini Simba jike ndiyo anasifiwa ni hatari linapokuja suala la kuwinda ajabu bado anabeba mimba??
 
Back
Top Bottom