Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Buji...Kuna mtu anataka historia iandikwe upya, watoto wasifundishwe Tena habari za Nyerere.
Kabila lenye historia ni Wamasai peke yao😅🤣😂
Fikra zako unazilazimisha kuwaza jambo ambalo haliwezekani labda kwa kughadhibika.
Ukitulia utatambua kuwa hilo la kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika bila Nyerere haliwezekani.
Labda nikurudishe.
Haikuwezekana kuwa na historia ya uhuru wa Tanganyika bila ya kumtaja Abdul Sykes pamoja na wazalendo wengine.
Hili mimi nimelithibitisha kwa kuandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.
Kila aliyekisoma ikawa kama vile anajifunza upya historia ya uhuru wa Tanganyika na pia historia ya Julius Nyerere.
Hebu angalia hii video hapo chini:
View: https://youtu.be/iHMVNAYEwZo