Mwalimu Nyerere vs Thabita Siwale

Shikamoo...
 
uko sawa hii stori ndiyo yenyewe,mgonja alitaka bint kwa ajili ya ufuska akapelekewa bint yake mwenyewe, kilichofuatia hapo Nyerere alimtoa Mgonja kwenye uwaziri wa elimu akampa mama Siwale.
 
uko sawa hii stori ndiyo yenyewe,mgonja alitaka bint kwa ajili ya ufuska akapelekewa bint yake mwenyewe, kilichofuatia hapo Nyerere alimtoa Mgonja kwenye uwaziri wa elimu akampa mama Siwale.
Huyu mama bado yupo ni vzr ahojiwe kujua ukweli
 
Sishangai nasikia wanawake wa kinyakyusa ni magaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisoma korogwe girls mwl Siwale akiwa Headmistress wangu, tuliingia pale 1973 Korogwe girls ilikuwa ya mchepuo wa kilimo, Siwale alitulimisha mashamba ambayo kila mmoja alipangiwa plot yake kuanzia mwanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha 6 bila kujali ni mtoto wa kiongozi au wa nani, na pale walisoma watoto wengi sana wa viongozi na wengine wa matajiri wakubwa, alikuwepo Subira Nyerere mtoto wa kakake Julius Nyerere, mtoto wa kawawa, watoto wa sir Kahama, watoto wa Mtengeti....Asharose na wadogo zake 3 mmoja wao ni balozi South Africa kama hajahama nk kile kilimo cha mahindi kilikubali mno matikiti, matango nk hicho ndicho kilimpa sifa mama Siwale na 1974 Nyerere akampa uwazi wa Ardhi tukaendelea na mama Msemakweli, kipindi anaondoka nilikuwa form 2.Hiyo ndio ukweli mengine anaonewa tu.Tulipewa kila mtu jembe jipya na kila jembe lina namba ukipoteza unalo utalipa, kilimo kilikubali mno Nyerere alikuja pale alishangaa zile eka na eka zilivyokuwa zimezaa vizuri.
 
salome peter viongozi walikuwa hawaji kuchukua totoz za kustarehe nazo hapo korogwe girls
 
Hakukuwahi kutokea kiongozi yeyote achukue mwanafunzi pale kwa kweli, na tulifungiwa sana tulikuwa na ruhusa ya kutoka mara moja kwa mwezi kila week end ya mwisho wa mwezi na mwisho wa kuingia shule ni saa 11.30 jioni na si vinginevyo
 
Enzi hizo hakukuwepo na haya maswala ya ngono kwa kiasi kikubwa, na heshina ilikuwepo kwa wanafunzi, hivyo watu wazima waliwaheshimu sana watoto na wanafunzi heshima hiyo imetoweka kipindi hiki cha mitandao na tamaa ya pesa.
 
Aisee nimeamini watu wanajua kutunga jamani daaa, Siwale tunamfaham in and out bidii yake ya usimamizi wa shule, kulikuwa na nidhamu ya hali ya juu, shule ilikuwa safi mno, kilimo kilikubali sana shule ilijitegemea kwa chakula hapo ndipo alipoanza kupata umaarufu hadi Rais Nyerere akaja kujionea na kuja kumpa uwaziri.Ukweli sisi wanafunzi wake tuliona uwaziri hakuuweza kama alivyokuwa na uwezo wa kusimamia shule.Hakuwa mkali ila muelekezaji mzuri. Raha yetu mahindi yakikomaa lazima tuchemshiwe mnakula mtakavyo,kila tulicholima kilikuwa kwa ajili ya matumizi yetu
 
Huo ndio ukweli. Hata mimi ninafahamu hivyo
 
Makongoro na Madaraka wamesoma Tabora. Hapo umeteleza mkuu.
 
Angalau walijua MZEE Kambarage ataiona barua ya wito.
 
Shikamoo
 
1973 Upo O Level tuchukulie form 3 or 4 Hapo lazima ulikuwa na miaka si chini ya 18 means umeazaliwa miaka ya 1955-1957 so now una miaka kati ya 60--65. SHIKAMOO MAMA..
 
Marahaba mwanangu hujakosea kabisa kwa umri huo, aliyesoma nasi alikuwa mdogo kuliko wote darasani kwetu anastaafu 2020 mimi mwezi huu mwishoni naaga serikalini naachia gari za serikali nikajue kununua mafuta sasa [emoji86][emoji3]
 
Tuliobahatika kupata wazazi wasomi wenye madaraka hatukuanza shule na umri mkubwa sana,japo ukilinganisha na sasa bado ni umri mkubwa tu
 
Kiranga!!
Umeamua kutema yai. Hatari sana I seee!
 
Haikuwa rahisi hivyo kama ulivyosimulia. Kwanza kabisa Nyerere alimtuma mwakilishi aende na mtoto. Mama Siwale akakataa kuwa lazima aende na mzazi. Mwakilishi siyo mzazi. Ndipo ikabidi Julius mwenyewe aende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…