Camilo Cienfuegos
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 18,960
- 67,654
Shikamoo...Hii story imevulugwa kidogo, ninavyojua mimi mtoto wa Nyerere aliyewahi kufukuzwa shule ni John ambae alikuwa anasoma Mazengo DODOMA wakati huo ikiitwa Illiance.
Kwa uhakika kabisa headmaster aliyemtimua shule mtoto huyo alikuwa anaitwa Mr. Kamuzola ambae baadae aliteuliwa na Nyerere huyo huyo kuwa RDD Dodoma mwaka 1972 wakati wa centralization.
Thabita Siwale aliibukia chuo cha ualimu Korogwe kule alikutana na Waziri mmoja wa elimu alikuwa mhuni mhuni hivi aliitwa Chediel Mgonja waliwaki kupishana na Siwale kwa ajili ya mambo yake ya ufsika(waziri) wakati huo mambo hayakuwa magumu kama ilivyo sasa ilikuwa ni kawaida kabisa Principal kumtafutia kitowewo waziri hata kama ni mwanachuo na mkuu wa chuo kuneemeka privilege fulani toka kwa waziri.
Haya Siwale aliyakataa kabisa, labda msimamo huu ulimfikia Mzee Julius kwani waziri huyo hakudumu. Sikumbuki kama Siwale alipata ubunge wa kuteuliwa, ila nadhani aliteuliwa maana enzi hizo viti maalum vilikuwa bado kuanzishwa, basi alipopata ubunge akawa ni waziri wa elimu.
Habari zinasema baada ya kuwaa waziri mama huyu akawa anacheza rafu sana mambo ya kiunyumba na mzee Siwale kila mala mzee akimhitaji basi alikuwa anamjibu kwamba amechoka na kwamba uwaziri wa elimu siyo mchezo, basi Mzee Siwale akatoa malalamiko kwa Nyerere ikabidi naye amwondoe kwenye nafasi hiyo ili amhudumie vizuri Mzee Siwale.
Chaguzi zilizofuata hakufua dafu alijaribu ubunge wa Afrika Mashariki pia hakufua dafu,akanzisha NGO yake akaiita WAT( women Advancement Trust) ofisi zake ziko Kinondoni barabarani kabisa nadhani ni Kawawa road .
Uliyeandika Tread hii nenda pale kinondoni utamkuta huyu mama akupe ukweli zaidi toka mdomoni mwake.