Tuyuku
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 3,292
- 1,927
Siyo kweli; mama Tabitha alipandishwa kutokana na ujasiri wa kumshitaki Chediel Mgonja aliyekuwa Waziri wa Elimu wakati huo ila akawa anafanya umalaya na wanafunzi wa kike, mmoja wa wanafunzi waliokuwa wakifanya ufuska na Mgonja alikuwa mwanafunzi wa Korogwe Girls ambako Tabitha alikuwa Headmistress. Hivyo Tabitha akamfuata Mwalimu pale Magogoni akiwa na makbarasha ya ushahidi dhidi ya Mgonja ka kumpa makavu makavu Nyerere kuhusu waziri wake huyo; huku akimtaka akome kuvurugia wanafunzi wake. Ndipo Mwalimu alifurahia ujasiri wa mama yule, akamfuta Mgonja Uwaziri wa Elimu mara moja na kumpa nafasi hiyo mama Tabitha.
Siku hizi ukiwa na ujasiri huo lazima ung'olewe kucha.