Mwalimu Nyerere vs Thabita Siwale

Mwalimu Nyerere vs Thabita Siwale

Marahaba mwanangu hujakosea kabisa kwa umri huo, aliyesoma nasi alikuwa mdogo kuliko wote darasani kwetu anastaafu 2020 mimi mwezi huu mwishoni naaga serikalini naachia gari za serikali nikajue kununua mafuta sasa [emoji86][emoji3]
Very interesting!!!
 
Haikuwa rahisi hivyo kama ulivyosimulia. Kwanza kabisa Nyerere alimtuma mwakilishi aende na mtoto. Mama Siwale akakataa kuwa lazima aende na mzazi. Mwakilishi siyo mzazi. Ndipo ikabidi Julius mwenyewe aende.
Kwa hiyo posts za mama Salome Peter hujaziona au ???
 
Hii story imevulugwa kidogo, ninavyojua mimi mtoto wa Nyerere aliyewahi kufukuzwa shule ni John ambae alikuwa anasoma Mazengo DODOMA wakati huo ikiitwa Illiance.

Kwa uhakika kabisa headmaster aliyemtimua shule mtoto huyo alikuwa anaitwa Mr. Kamuzola ambae baadae aliteuliwa na Nyerere huyo huyo kuwa RDD Dodoma mwaka 1972 wakati wa centralization.

Thabita Siwale aliibukia chuo cha ualimu Korogwe kule alikutana na Waziri mmoja wa elimu alikuwa mhuni mhuni hivi aliitwa Chediel Mgonja waliwaki kupishana na Siwale kwa ajili ya mambo yake ya ufsika(waziri) wakati huo mambo hayakuwa magumu kama ilivyo sasa ilikuwa ni kawaida kabisa Principal kumtafutia kitowewo waziri hata kama ni mwanachuo na mkuu wa chuo kuneemeka privilege fulani toka kwa waziri.

Haya Siwale aliyakataa kabisa, labda msimamo huu ulimfikia Mzee Julius kwani waziri huyo hakudumu. Sikumbuki kama Siwale alipata ubunge wa kuteuliwa, ila nadhani aliteuliwa maana enzi hizo viti maalum vilikuwa bado kuanzishwa, basi alipopata ubunge akawa ni waziri wa elimu.

Habari zinasema baada ya kuwaa waziri mama huyu akawa anacheza rafu sana mambo ya kiunyumba na mzee Siwale kila mala mzee akimhitaji basi alikuwa anamjibu kwamba amechoka na kwamba uwaziri wa elimu siyo mchezo, basi Mzee Siwale akatoa malalamiko kwa Nyerere ikabidi naye amwondoe kwenye nafasi hiyo ili amhudumie vizuri Mzee Siwale.

Chaguzi zilizofuata hakufua dafu alijaribu ubunge wa Afrika Mashariki pia hakufua dafu,akanzisha NGO yake akaiita WAT( women Advancement Trust) ofisi zake ziko Kinondoni barabarani kabisa nadhani ni Kawawa road .

Uliyeandika Tread hii nenda pale kinondoni utamkuta huyu mama akupe ukweli zaidi toka mdomoni mwake.
Hizo ofisi zilikuwa pale jengo LA Kinondoni hospital kwa Dr Mvungi. Nimeandika zilikuwa maana aina hakika kama bado zipo.
 
Ubarikiwe sana kwa utumishi wako wa Taifa hili. Miaka 15 hivi kuanzia leo, kama Mungu atanipa uzima, nitakuwa nastaafu pia.
Marahaba mwanangu hujakosea kabisa kwa umri huo, aliyesoma nasi alikuwa mdogo kuliko wote darasani kwetu anastaafu 2020 mimi mwezi huu mwishoni naaga serikalini naachia gari za serikali nikajue kununua mafuta sasa [emoji86][emoji3]
 
Hii story imevulugwa kidogo, ninavyojua mimi mtoto wa Nyerere aliyewahi kufukuzwa shule ni John ambae alikuwa anasoma Mazengo DODOMA wakati huo ikiitwa Illiance.

Kwa uhakika kabisa headmaster aliyemtimua shule mtoto huyo alikuwa anaitwa Mr. Kamuzola ambae baadae aliteuliwa na Nyerere huyo huyo kuwa RDD Dodoma mwaka 1972 wakati wa centralization.

Thabita Siwale aliibukia chuo cha ualimu Korogwe kule alikutana na Waziri mmoja wa elimu alikuwa mhuni mhuni hivi aliitwa Chediel Mgonja waliwaki kupishana na Siwale kwa ajili ya mambo yake ya ufsika(waziri) wakati huo mambo hayakuwa magumu kama ilivyo sasa ilikuwa ni kawaida kabisa Principal kumtafutia kitowewo waziri hata kama ni mwanachuo na mkuu wa chuo kuneemeka privilege fulani toka kwa waziri.

Haya Siwale aliyakataa kabisa, labda msimamo huu ulimfikia Mzee Julius kwani waziri huyo hakudumu. Sikumbuki kama Siwale alipata ubunge wa kuteuliwa, ila nadhani aliteuliwa maana enzi hizo viti maalum vilikuwa bado kuanzishwa, basi alipopata ubunge akawa ni waziri wa elimu.

Habari zinasema baada ya kuwaa waziri mama huyu akawa anacheza rafu sana mambo ya kiunyumba na mzee Siwale kila mala mzee akimhitaji basi alikuwa anamjibu kwamba amechoka na kwamba uwaziri wa elimu siyo mchezo, basi Mzee Siwale akatoa malalamiko kwa Nyerere ikabidi naye amwondoe kwenye nafasi hiyo ili amhudumie vizuri Mzee Siwale.

Chaguzi zilizofuata hakufua dafu alijaribu ubunge wa Afrika Mashariki pia hakufua dafu,akanzisha NGO yake akaiita WAT( women Advancement Trust) ofisi zake ziko Kinondoni barabarani kabisa nadhani ni Kawawa road .

Uliyeandika Tread hii nenda pale kinondoni utamkuta huyu mama akupe ukweli zaidi toka mdomoni mwake.
Umepatia; kwa sisi tuliokuwa vijana na mashuhuda enzi hizo. Makongoro (Mako) ndiye aliyekuwa anasoma Tabora Boys wakati huo na hahusiani kabisa na tukio (la John pale Mazengo). Ingawa Makongoro naye alikuwa mtukutu fulani hivi pale Tabora Boys (ndie aliyekuwa drummer wa bendi ya muziki pale shuleni). Wacha niishie hapo.
 
Thabita Siwale aliibukia chuo cha ualimu Korogwe kule alikutana na Waziri mmoja wa elimu alikuwa mhuni mhuni hivi aliitwa Chediel Mgonja waliwaki kupishana na Siwale kwa ajili ya mambo yake ya ufsika(waziri) wakati huo mambo hayakuwa magumu kama ilivyo sasa ilikuwa ni kawaida kabisa Principal kumtafutia kitowewo waziri hata kama ni mwanachuo na mkuu wa chuo kuneemeka privilege fulani toka kwa waziri.
Mimi niliambiwa alikuwa Headmistress Korogwe Girls, huyo waziri alipoomba apewe binti wa kulala naye, huyo mama aliresist, baada ya vuta nikuvute mwisho akasubiri jioni ifike akampelekea binti yake huyo Waziri ndipo ugonmvia ukaanzia hapo na siri kuvuja na kumfikia Rais
 
Kwa kweli Mwl. Nyerere alikuwa Rais haswaa na hakuacha jukumu lake la uzazi kwa familia yake.
Mh. Makongoro aliwahi kusimulia kuwa Baba yake (Mwl. Nyerere) alimzuia kupelekwa shule kwa gari la serikali na akamwambia, "kuwa mkubwa ununue la kwako". Hii ni baada ya kukataa kwenda shule kwa siku hiyo na dereva alipewa majukumu mengine na kuchelewa kuwapeleka shule, ingawa shule hiyo haikuwa mbali sana na makazi yao. Mh. Makongoro alisema alibahatika kumiliki gari yake ya kwanza alipokuwa Mbunge wa Arusha!
 
Maswali ya kujiuliza je kwa sasa hivi ni mkuu gani wa shule anaweza kumfukuza mtoto wa rais Shule achilia mbali watoto wa wabunge,mkuu wa wilaya au mkoa,waziri au hata wakurugenzi tu?
Hilo haliwezekani tena kwa sababu siku hizi viongozi wanasomesha watoto shule za International na shule za International hawafukuzi hela( watoto)
 
Shule za serikali ndio zina tabia ya kuogopa wazazi wenye vyeo vikubwa wenye watoto wanaosoma shule zao

Nenda shule za katoliki uone viongozi wakubwa serikalini wenye watoto hawana special previlege yeyote wao wala watoto wao

Hawaburuziki mzazi akitutumua mabega wanamwambia ondoka na mwanao
 
Kwa kweli Mwl. Nyerere alikuwa Rais haswaa na hakuacha jukumu lake la uzazi kwa familia yake.
Mh. Makongoro aliwahi kusimulia kuwa Baba yake (Mwl. Nyerere) alimzuia kupelekwa shule kwa gari la serikali na akamwambia, "kuwa mkubwa ununue la kwako". Hii ni baada ya kukataa kwenda shule kwa siku hiyo na dereva alipewa majukumu mengine na kuchelewa kuwapeleka shule, ingawa shule hiyo haikuwa mbali sana na makazi yao. Mh. Makongoro alisema alibahatika kumiliki gari yake ya kwanza alipokuwa Mbunge wa Arusha!
Ilikuwa watoto wa Nyerere wanadeka tu

Shule ya msingi waliyosoma ni Mbuyuni pale karibu na kanisa la St Peters mahali pa kutembea tu kwa mguu kutoka Msasani kwao pana urefu wa kutembea kama uwanja wa mpira tu

Ndio wapande gari ya serikali? Kwenda na kurudi? Nyerere alikuwa sahihi
 
Wadau wa historia habari zenu? naombeni msaada kuna habari nimewahi kuisikia zamani kidogo inamhusu Mwalimu Nyerere kipindi hicho akiwa Rais wa Tz na mwanasiasa mkongwe Bi Thabita Siwale waziri wa zamani wa elimu na utamaduni!

Hbr yenyewe ipo hivi huyu bi Thabita Siwale chanzo cha yeye kuteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa Waziri wa Elimu miaka hiyo ni ujasiri wa kipekee aliounyesha akiwa mkuu wa shule sekondari maarufu mkoani Tabora(jina nimelisahau) kwa kuumpa adhabu ya kurudi nyumbani kwa muda(sunspension)mtoto Mwalimu Nyerere aliyekuwa akisoma katika shule hiyo na kumuamuru siku ya kurudi shule aje na mzazi wake ili hali akijua kabisa mzazi wake ni rais wa nchi mwalimu Nyerere!

Aidha inasemekana baada ya kumpa adhabu hiyo watu wengi walianza kumtisha Bi Thabita kuwa atafukuzwa kazi kwa kumrudisha nyumbani mtoto wa Rais.

Baada ya adhabu kwisha yule mtoto alirudi shuleni akiwa na mzazi wake kama alivyoamriwa katika barua aliyopewa wakati wakurudishwa nyumbani Walimu na hata Bi Tabitha walistaajabu walipomwona yule mtoto kaja na Mwalimu Nyerere,wenyewe walimu na Bi Tabitha walitegemea mwalimu Nyerere angemtuma mwakilishi kutokana majukumu na hadhi yake ya urais wa nchi.

Baada ya kumwona Nyerere inasemekana mama Tabitha na staff nzima walichanganyikiwa wakajua sasa mwisho wao ndiyo umefika wa kufukuzwa kazi,lkn mwalimu Nyerere aliwatoa wasiwasi na kuwambia wasiwe na hofu yoyote yeye pale hajaja kama Rais wa nchi bali amekuja kama mzazi wa mtoto,baada ya hapo kengele ya paredi ikangongwa wanafunzi wakakusanyika wote yakaelezwa yale makosa ya mtoto wa Nyerere akaamriwa kuchapwa viboko na mwisho wa siku akaruhusiwa kuendelea na masomo,mwalimu Nyerere akarudi zake Dar es Salam.

Nasikia baada ya muda BiThabita badala ya kufukuzwa kazi akateuliwa kuwa waziri elimu kwa ushujaa aliounyesha!Maswali ya kujiuliza je kwa sasa hivi ni mkuu gani wa shule anaweza kumfukuza mtoto wa rais Shule achilia mbali watoto wa wabunge,mkuu wa wilaya au mkoa,waziri au hata wakurugenzi tu?

Kwa hakika Bi thabita alionyesha ushujaa wa hali ya juu sana!Kwa kizazi cha sasa tuna hitaji aina ya viongozi km Bi Tabitha Siwale ambao wanaweza kufanya maamuzi magumu bila kujali hadhi ya mtu!
Huyo bibi inaonekana alikuwa hana doa hapo shuleni.
 
Hii habari sijaisikia. Hili jambo naona ni distraction.Huyu Thabita Siwale sikuifuatilia sana career yake. I was too youmg at that time to be preoccupied with politics. Halafu hakuna mtoto wa Mwalimu ambaye amesoma Tabora.
Maoni yangu ni kwamba walimu wanaowabughudhi watoto wa viongozi,I hate them with perfect hatred. Hao watoto wa Wabunge,watoto wa Katibu Kata,mimi kaka yao. Tabia ya kuwaita vibaka,walevi,teja,na kuwafanyia fujo,ikomeshwe mara moja. I ask that they should be left in peace.
Vipi mlishamalizana na steve mengele?
Poppy Hatonn
 
Nyerere alikuwa Rais mnyenyekevu ambaye hakupenda kujikuza sana Wala kuabudiwa kama marais wa kipindi hichi
 
Back
Top Bottom