Mwalimu unapata 0 halafu ukafundishe watoto wetu?? Hongera psrs

Hili panga lina balaa kuanzia mwenye 65, 60, 55, 48, 30, 20, 9 na 0 wote hawajachaguliwa.
 
Vipi kuhusu watunga sera za nchi walioishia la 5B wenye maono ya miaka ijayo 50 ya nchi yetu?...
 
Ndio walitaka kupangiwa vituo bila interview? Kweli HAPANA katika hili.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Hawa ndio walikuwa wanataka kupangiwa vituo bila interview.

Mtu anapata 8 atafundisha watoto wa nani sasa?
Kwa sisi ambao ELIMU zetu za mwanzo tumesomea Ualimu. Mimi pia ni mwalimu nilifundisha kwa miaka miwili nikaachana na hio kazi.

Mwalimu ni CONTENT, mfano Kuna ambao wapo vizuri kwenye kujibu mitiani na kupata GPA kubwa Ila wasiwe wazuri kwenye ku deliver material darasani

Kuna jamaa mmoja tulikua tuna muita kitivo/ professor Ila jamaa ni hatare anaingia na chaki na anafundisha vizuri Sana Ila kwenye mitiani tuna mgaragaza anapata matokeo ya kawaida kabisa...

NB.
Mwalimu sio GPA , Mwalimu ni Content.

Kushindwa hiyo OBJECTIVE TEST sio kwamba ndio mu jump to the conclusion kua hao walimu ni ma bogus sababu ni nyingi wakuu.
 
Ukweli๐Ÿ’ฏ
 
Mtu amekaa mtaani miaka zaidi ya mitano umpe mtiani unategemea apate 100๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Mbona wenzake wamefaulu? Kwani alipoitwa kwenye Usaili alidhani anaenda kwenye bufee? Kwa nini asijiandae kama wenzake?. Hao ndo baadaye utawasikia kuna zengwe, kuna upendeleo na blah blaaa nyingi za kujitetea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ