Mwalimu wa Madrasa apandishwa Kizimbani kwa tuhuma za kuwachapa fimbo (Ukatili) wanafunzi wa madrasa

Wapewe waislamu hii kesi....wajihukumu wenyewe...
 
Mimi hata nikimuona mtu anamchapa Punda wake huwa namuonya na kumwambia huyu ndio anakufanya uende chooni na wanao kama unao, halafu unampiga akiwa kabeba mzigo mzito.
Kweli fimbo sio sababu ya kufundisha na sioni sababu zozote za kupiga
Wanangu siwachapi na wana nidhamu sana kwa sababu nawafundisha

Hawaibi wala kutukana na shuleni wako vizuri pia, wakija nyumbani wanajua wajibu wao, homework kwanza, mengine yanafuata

Kuna watu wanafikiri kupiga ni nidhamu ila utakuta wauwaji wengi ukiwahoji makuzi yao watakuambia tulikuwa tunapigwa mpaka mangumi ya kichwani

Kama wanafuatilia hivyo basi mashule wanapiga mpaka mtoto anakufa
 
Wanazo wanafanya part-time tu tena bure,but huyo mwalimu kwa kweli amekosea thus watoto wengine uchukia madrasa
Halafu mbona huyo ustaadhi anapiga watoto wa kike kwa hasira na nguvu kubwa kuliko watoto wa kiume kwa nini?

Yaani hako kenye hijabu nyeusi alikuwa na hasira nako kama nini na alikapiga kwa nguvu hasa kuliko wa kiume alikatongoza kakamkataa au?
 
Kama hamtaki watoto wenu wagiswe muwe mnakaa nao nyumbani mnawafundisha , haiwezekani mtoto afanye makosa aangaliwe tu.
Katili mwingine huyu hapa. Kwanza unaelewa neno mtoto? Yaani watoto ndiyo mmeona ni wa kuchapwa tu? Nyinyi ndiyo huwafanyia watoto ukatili.

Mtoto kama kafanya makosa, ongea naye, fimbo haijawahi kuwa suluhisho, ndiyo maana tuna watoto watukutu, watoto wa mitaani waliokimbia vipigo majumbani na mateso. Hata hivyo mtoto wangu kafanya mafundisho, hakuwahi nilalamikia kuchwapwa.
 
Watanzania tulivyo wanafiki wanakusifikia unajua kulea na unakuja kujigamba?

Ukute wanakuchora 🤣🤣🤣
 
Kwa hiyo mwanao akipigwa au angepigwa namna hiyo, ungeridhia kabisa?

Be honest.
Binti yangu nienda kupiga shuleni mwenyewe fimbo 6. Nisingefabya hivyo asingemaliza shule alianza kwa kumugomea mwl kqenye parade taifa. Nisitoe story zaidi. Qatoto wafundishwe wachapwe ,ila kwa upendo. Period
 
Watanzania tulivyo wanafiki wanakusifikia unajua kulea na unakuja kujigamba?

Ukute wanakuchora 🤣🤣🤣
Ndiyo akili yako ilipoishia? Au kuna nyingine? Labda aina yako na unafiki wako. Nasisi tunaoishi naye hatumuoni? Walimu wake, yaani watu wote ni wanafiki hadi sisi wenyewe?
Acha roho mbaya ndugu, safisha roho hiyo ili mambo yaende.

Mwenzako ndiyo hivyo mtoto wangu ana nidhamu sana na namshukuru Mungu kwa hili. Hicho ulichosema hakibadilishi kuwa yeye ana nidhamu. Pole lea mtoto kwenye maadili halafu sukutua hiyo roho kaka.
 
Mufti wa Zanzibar na Mbagala Tena !??....
Kaandika kabisa na kutaja akionya ma ustaadhi wa Zanzibar kuwa wasifanye kama huyo wa Mbagala Dar es Salaam

Katoa waraka kabisha kuwa huyo maalim wa Mbagala Dar es Salaam anachafua na kuharibu taswira ya uislamu


Nashindwa ku attach tamko lake mwenye uwezo aweke humu
 
Binti yangu nienda kupiga shuleni mwenyewe fimbo 6. Nisingefabya hivyo asingemaliza shule alianza kwa kumugomea mwl kqenye parade taifa. Nisitoe story zaidi. Qatoto wafundishwe wachapwe ,ila kwa upendo. Period
Hapo ni wewe ulimpiga.

Ndio maana ulikuwa na Amani.

Vipi uone mtu baki anampiga mwanao mwenye umri kama wa hawa watoto?

Je utaona ni sawa tu?
 

Food for thought. Watanzania unatujua hatukuambii ukweli mpaka mambo yaharibike ndio tunaanza kunyoosha vidole.

Wewe hatuwezi kuikubali rating ya nidhamu ya mtoto wako mwenyewe kwasababu you can not objective. Kila mzazi anaona mtoto wake hana shida.

Hongera umepata mtoto ukiongea anasikiliza.

Haya mambo yana bell curve. There are extremes at both ends. Sasa kama wako yuko kushoto kuna wengine wako kulia mwa hiyo curve, hawasikii maneno ila wanarespond to bodily pain. Usitake system yako i apply kwao.

Nimekupa changamoto kidogo tu bingwa wa malezi umenivamia personally kuwa nina roho mbaya. Kwema huko? Unaweza kweli ukaongea na mtoto mtukutu akakuelewa kama challenge yangu tu umeshindwa kuipangua kiutu uzima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…