Mwalimu wa Madrasa apandishwa Kizimbani kwa tuhuma za kuwachapa fimbo (Ukatili) wanafunzi wa madrasa

Lkn
Kuna aina ya upigaji kulinganisha na umri.

Sasa hao watoto umri wao ni mdogo sana, Halafu hilo li bakora nila kupigia watu wazima kabisa.

Sasa yeye anachapia vitoto vidogo tena kwa nguvu kubwa kama anaua nyoka.
Holo si swala la mahakani .
 
Ni kweli mkuu sikatai hilo, kuna watoto watukutu sijui ni kwa sababu ya mazingira wanayo kuwa nayo au vipi
Ila wapo watukutu kabisa ambao unajiuliza huyu mtoto au kibaka?

Inasikitisha sana ila bado wanahitaji msaada mkubwa sana maana unaweza kupiga mpaka ukavunja kila kiungo lakini bado kesho yake akarudia yaleyale,
Sasa wa hivyo utamfanya nini
Huku nilipo mwaka 2022/23 watoto wa miaka sita waliorudishwa nyumbani kwa utovu wa nidham walikuwa 22,000
Hebu imagine watoto wadogo namna hiyo waalimu wamewashindwa wanaamua wawe suspended from school
Hii ni 🇬🇧
 
Katazame video uwaangalie vizuri.

Halafu upime kama aina ile ya upigaji na nguvu ile ya upigaji ni sawa.
Mimi naona ni sawa tu kwasababu wote kawachapa mikononi na fimbo zisizozidi nne na hajagusa sehemu nyingine za mwili
 
Kwani wewe hujaiona hiyo video?

Hujaona mazingira ya kwenye hiyo video?

Maadili unafunzwa na wazazi wako au walezi wako tangu udogoni.

Pia maadili hayafunzwi kwa viboko kama vya huyu jamaa.
Kwaiyo wazazi wako wasipokuwa na madili wewe mtoto utajipimaje kuwa una maadili?
 
Hao shida ilianzia nyumbani wakiwa wadogo... They faced no consequences for their action, hawafuati structure.

Ukiongezea facr ya kwamba hakuna any tangible consequences shuleni, inabidi warudishwe wawe mzigo wa wazazi

Laiti kama wangewepa discipline, structure kuanzia nyumbani, up to and including viboko, hiyo idadi ingepungua
 
Acha nawewe ujinga. Mfano wa Serikali na kufungwa ni sawa na kosa la mtoto. Huko mahakamani kwenyewe kuna makosa ya vifungo vya nje, si kila kosa mtoto achapwe.

Ngoja nikufundishwe wewe, kuna mtoto alikuwa akichelewa shule kila siku. Anachapwa haswa, hakuna mwalimu aliyejitolea kukaa naye chini na kumhoji kwanini anachelewa ni mwendo wa viboko na adhabu za nje.

Mwalimu mpya aliyehamia hiyo shule, alikuwa na upendo sana. Aliamua kukaa na kila mtoto mwenye makosa ya kujirudia, huyu alimwambia anaishi na mama wa kambo na baba yake anaendesha magari makubwa, hayupo mara nyingi nyumbani.

Mtoto alisema anatakiwa afanye kazi zote za nyumbani, muda unakuwa unaenda akifika shule anachapwa. Ni mtoto ndiyo kaingia darasa la 5. Toka hapo wakajua tatizo lake, haya bila kuongea naye wangejua shida yake. Wakati mwingine shida si watoto ni wazazi na walezi. Wewe mtoto wako piga uwa ila jua ni mali ya Serikali.
 
Safi kabisa.

Haya mavaa kobazi lazima yadhibitiwe.

Dunia ipo kwenye kuwafunza watoto teknolojia, Yenyewe yapo bize kukaririsha watoto kiarabu na hekaya za vitabuni.
Uko nje ya mada kabisa.
Hoja hapa ni viboko kwa watoto.
 
Sjaangalia video yote lakin naona ni adhabu za kawaida tu,kuna madrasa moja ipo ujiji,mwalimu hasubir hvyo kama huyo jamaa,yeye huchapa fimbo za mvua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…