KERO Mwalimu wa Sanaa, nafanya kazi Miaka 4 sasa Ilala bila Malipo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari za muda huu wana JamiiForums!

Kwanza kabisa naomba kuwasilisha kero iliyopo kwenye halmashauri yetu ya jiji la ilala.

Mimi ni mhitimu wa shahada ya ualimu wa masomo ya sanaa Mwaka 2016 kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Baada ya kuhitimu chuo niliendelea na harakati zingine za kimaisha ila sikuwa na fundisha tena.

Ilipofika Mwaka 2023 nikamua kurudi kwenye taaluma yangu niliyosomea na kuomba ikitokea kwenye shule secondary X iliyopo Chanika.

Nilikubaliwa na kuanza rasmi kuitumikia taaluma yangu Kwa kuwafundisha watoto wa watanzania wenzangu pasina kulipwa chochote.

Nilikutana na wenzangu wa masomo ya science wawili,wakati huo wote tulikuwa hatulipwi chochote na mamlaka husika.

Mwaka mmoja baadae uongozi wa halmashauri ukaja na mpango mwingine wa kuanza kuwalipa walimu wa science.Wenzangu waliingizwa kwenye mpango huo Mimi nikaachwa Kwa kuwa si mwalimu wa science.

Mpaka hivi sasa bado naendelea kuwafundisha watoto huu Mwaka wa nne sasa.

Sikuwa na shida nalo hili japo kuwa huwa inaniumiza Sana kuona wenzangu wanalipwa na Mimi silipwi hata kidogo.

Ombi langu Kwa mamlaka,ninaomba utuangalie Kwa jicho la kipekee hata Sisi tunajitolea Kwa masomo ya sanaa angalau na Sisi tuwezekujikimu kimaisha kupitia taaluma tuliosomea.

Ningekuwa na mtaji nisingefanya kazi ya kujitokea bure bali ningejikita hata na baishara ndogo ndogo.

Asanteni naomba kuwasilisha
 
Si ukafundishe hata Private Schools..kwani lazima Serikalini?!
Dar Bila Mishahara mbona kipengere?
 
Kaka pole ila kama unaweza na huna majukumu ya msingi ,kuhudumia familia wewe mwenyewe tegemezi ,amka jifute vumbi anza kuikataa hio hali kwa nguvuu moja wanakubeba ujinga,saka ata dili za ujenzi anza nazo kisha tujue nini cha kufanya ila kujitolea hapana
 
Miaka 4 kujitolea tafuta sehemu kazi nyingine kwanza unaishije?
 
Chukua hata boda boda uache uo ujingwa kujitolea
 
Si uache kazi. Kwani hapo wamekuteka na kukulazimisha ?

Kama unajitolea sawa. Ila hutakiwi kulalamika
 
Anajilipa kwenye mabinti zetu huyuu😂😂😂
 
Habari za muda huu wana JamiiForums!

Kwanza kabisa naomba kuwasilisha kero iliyopo kwenye halmashauri yetu ya jiji la ilala.

Mimi ni mhitimu wa shahada ya ualimu wa masomo ya sanaa Mwaka 2016 kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Baada ya kuhitimu chuo niliendelea na harakati zingine za kimaisha ila sikuwa na fundisha tena.

Ilipofika Mwaka 2023 nikamua kurudi kwenye taaluma yangu niliyosomea na kuomba ikitokea kwenye shule secondary X iliyopo Chanika.

Nilikubaliwa na kuanza rasmi kuitumikia taaluma yangu Kwa kuwafundisha watoto wa watanzania wenzangu pasina kulipwa chochote.

Nilikutana na wenzangu wa masomo ya science wawili,wakati huo wote tulikuwa hatulipwi chochote na mamlaka husika.

Mwaka mmoja baadae uongozi wa halmashauri ukaja na mpango mwingine wa kuanza kuwalipa walimu wa science.Wenzangu waliingizwa kwenye mpango huo Mimi nikaachwa Kwa kuwa si mwalimu wa science.

Mpaka hivi sasa bado naendelea kuwafundisha watoto huu Mwaka wa nne sasa.

Sikuwa na shida nalo hili japo kuwa huwa inaniumiza Sana kuona wenzangu wanalipwa na Mimi silipwi hata kidogo.

Ombi langu Kwa mamlaka,ninaomba utuangalie Kwa jicho la kipekee hata Sisi tunajitolea Kwa masomo ya sanaa angalau na Sisi tuwezekujikimu kimaisha kupitia taaluma tuliosomea.

Ningekuwa na mtaji nisingefanya kazi ya kujitokea bure bali ningejikita hata na baishara ndogo ndogo.

Asanteni naomba kuwasilisha
Unatumia ujana wako vibaya, mtu umemaliza chuo 2016 uwezekano wa kuwa age kuanzia 30 ni kitu cha kawaida harafu bado unafanya kazi ya bure! huwezi kusema labda unakazi nyingine ndio inakupa kula kwanini usiweke muda wako huko?
 
Back
Top Bottom