Mwalimu wa Shule ya Msingi aliepata Div IV ya Pts 28 kidato cha nne anaandaa msomi gani hapo baadae?

Bora hawa wamegusa walau O-level. Unakumbuka wale walimu wa UPE(Ualimu Pasipo Elimu - jus a kid) ambao wengi wao ni std vii na mpaka leo wapo na hawa ndo wamenifundisha na leo najivunia kadegree kangu kako poa. :coffee:

UPE (Universal Primary Education) ilikuwa sera ya umoja wa mataifa wakati ule lengo likiwa kuhakisha watoto hasa kutoka nchi masikini wanapata elimu ya msingi. Kulingana na wingi wa watoto na uchache wa walimu, ilikubaliwa wale waliomaliza la saba kwenda mafunzo ya muda mfupi na baadae kuwa walimu na hii haikufanyika Tanzania pekee.
 
Ona red uone kwamba hayo ndio matatizo ya wewe kufundishwa na walimu waliopata division iv ya pts 28!(Eti Diproma) kazi ipo!
 
Utasikia kauli kama 'walimu ni wito'...WTF!! Failures=Teachers nijitahidi kuulewa huu mlinganyo lakini wapi natoka kapa.
Na vyeti vyenyewe vya kuazima,unafikiri wanaweza hata kudai haki zao?wakitishiwa nyau tu wanajiuliza kazi watapata wapi tena,maana mwenye vyeti alishavichukua zamaaaaaani!
 
ndo wasomi tulionao wanaishia kuropoka tu,haya mambo ndo yanavyoenda kote dunian,wakishayasikia mtaan wanayaleta vivyo hivyo bila kupima,haya waje watetee hoja yao
Sio kuropoka,hivi unajua kuna mwalimu wa shule ya msingi hajui kutofautisha kipi ni moa kati ya Mara au Musoma,Kilimanjaro au Moshi
 
 

cku nyingne kabla ujapost fanya thorough research
kwanza
NIULIZE KWA NINI.,Haya uliza kwa nini?nikumwagie mipoint
ndo uamin hata ss walm wa dv4 ya 28 twawekuwafundisha wanachuo wa
university.
 
nashangaa watu wamesahau walipotoka tokea walipokuwa na makamasi wamefundishwa na huyo mwalimu halaf sasa hv kajua kuvaa suti analeta nyodo acheni dharau hao ndio wametufisha hapa mpaka tunajua kusoma comment hayo sio mambo ya kuongelea hasa wasomi weenye akili timamu kichwani.
 

Pamoja sana mkuu.Wametutoa mbali....
 
Rais yuko facebook... nenda kampe huu ujumbe
 
Tatizo kijana wa kitanzania akisha graduate na kupata kazi nzuri basi dharau mtindo mmoja wewe mwenye dv 1 au 2 unaweza kwenda kuchukau diploma ya uwalimu na ukawa mwalimu wa o-level?
 
cku nyingne kabla ujapost fanya thorough research
kwanza
NIULIZE KWA NINI.,Haya uliza kwa nini?nikumwagie mipoint
ndo uamin hata ss walm wa dv4 ya 28 twawekuwafundisha wanachuo wa
university.

kwa taarifa yenu hao mnaowaona na kuwaamin leo kuwa ni wasom walifundisha na walm weupe yaani wale walioishia drs la 7.
 
WAJUMBE mnatakiwa mkumbuke uyo mwalim mwenye div 4 ndio uyo aliyekufundisha wewe na leo uko JF hapa ... pamoja na wasomi wengine wengi ...
 
Baba na mama katika familia yako anaweza akawa hajui kusoma,kuandika na kuhesabu lakini unakuta ndiyo kakulipia ada mpaka ukafika ulipo. Dharau ni mbaya sana unadhani kuna kijiji kinachokosa wazee?Hao ndiyo wamezalisha wataalamu tele ktk nchi hii sasa wewe ukae chini utafakari kwa umakini.UKIMUUDHI MCHINJA MBWA LAANA ITAKURUDIA.
 
Mimi sioni haja ya kubishana hapa.ukweli uko wazi,mwl yeyote ambaye hayuko fit kitaaluma,kwanza ni mwoga wa kuulizwa maswali,pia anamnyenyekea afisa elimu wake kama kamungu kake hata akipewa nafasi ya kuchangia hoja utasikia hapo safi mkuu hata kama mkuu huyo amepotosha ukweli.vilevile mfano halisi hapa tz,hakuna mgomo wa walimu uliowahi kufanikiwa-sababu ya kutojiamini kwao. Japan wanafunzi waliofaulu kupita wengine ndio wanakuwa walimu na wanapewa mshahara mkubwa. kwa kuwa umeshaingia hapa "the home of great thinkers" usikurupuke kutetea walimu ambao ni failures kisa hawa ni ndugu,jamaa na marafiki zako. angalia migomo mingi inaanzia vyuo vikuu kwa wasomi. Tuwaambie viongozi wa nchi wabadili sera za nchi tupate elimu nzuri.
 
Reactions: Kig
Ni kweli mfumo wa elimu yetu una matatizo mengi sana. Si kweli kwamba mtu aliyepata division four point 28 hana uwezo wa kufundisha elimu ya msingi. Naamini kama akipata mafunzo mazuri chuoni na kazini na akajengewa mazingira mazuri ya kufundisha, akapewa vifaa bora vya kazi, akalipwa vizuri, bila shaka atafundisha wanafunzi vizuri na watapata elimu bora. Vijana wengi wenye division four ya 28 wanauwezo mzuri tu na wengine wamejiendeleza na wamefika hadi vyuo vikuu. kwa hiyo tatizo siyo division four ya point 28, tatizo ni namna gani wanakuwa supported kimafunzo, vifaa na malipo ili wafanye kazi yao vizuri na kwa moyo wa kujituma.

Wasomi wengi waliopo sasa ni zao la walimu waliokuwa na elimu ya darasa la saba (maarufu kama walimu wa UPE). hawa walimu walifanya kazi na ndio wameandaa wasomi karibu wote waliopo tanzania sasa hivi. kama wale waliweza, bila shaka mtu mwenye division four ya pts 28 itakuwa mzuri. ila awezeshe vizuri.
 
Bora hawa wamegusa walau O-level. Unakumbuka wale walimu wa UPE(Ualimu Pasipo Elimu - jus a kid) ambao wengi wao ni std vii na mpaka leo wapo na hawa ndo wamenifundisha na leo najivunia kadegree kangu kako poa. :coffee:

Aisee hawa walimu wa UPE nawaheshimu sana,ni watu ambao wanajua hasa maana ya ualimu kwa kweli najivunia kupita mikononi mwao.
 
Sio kuropoka,hivi unajua kuna mwalimu wa shule ya msingi hajui kutofautisha kipi ni moa kati ya Mara au Musoma,Kilimanjaro au Moshi

malimbukeni wa elimu mna tabu sana si ye huyo aliye kufundisha ukajua kusoma neno musoma
 
nenda shule za kata point 28 alafu umwangalie kama angelikuwa mzumbe,tabora,ihungo n.k uone ingekuwaje?fikiria tena mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…