Mwamba Mpina abishana na Bunge zima, wamzomea. Asimamisha Bunge kwa dakika 20

Binadamu hamna shukurani hata kidogo!! Ukifanya hivi wanakufanya mjinga. Ndo maana Mwenyekiti wenu kaamua kutafuna tu Ruzuku za chama

Mkojo shida ni nini, mbona unapanick sana.
 
Hana uchuma wowote, ni tapeli tu. Kinachoendelea huko bungeni ni igizo version ya katikati.
Mmezoea mpaka wahoji chadema ndo muawaamini wanatetea wananchi ila wakihoji wa chama tawala mnaona maigizo!! Ninyi watu ni wajinga sana akili zenu zote ni ushabiki wa vyama tu, anachosema mbowe ndo hivo hivo mnatii!

Mwenye akili pale chadema ni mbowe tu ndomana kila kitu anaamua yeye, yaani nyinyi mmeshindwa kabisa kufikiri na mmemuachia mbowe afikiri alafu mnajiona mna akili!!

Mimi sio CCM ila kwa akili zenu hizo chadema imeshakufa tayari bado kuzikwa tu, na chama cha kweli cha upinzani kitakacho chukua nchi bado hakija zaliwa.

Yaani nyinyi mpaka kuhoji bungeni mnataka muhoji nyinyi tu wakitokea watu wakihoji wengine mnaona ni maigizo! Ajabu kweli kweli..
 

Huna haja ya kupanick, huyo Mbowe unamuamini ww na mkeo/mumeo. Ni hivi huyo Mpina anafanya maigizo akidhani atatupoteza maboya. Ni haki yako kuamini hilo igizo lake lakini usilete jazba ili kila mtu aamini usanii wake.
 
Wote sawa tu hata huyo mpina hamanishi ni vile kapokonywa chakula/ uwaziri! Huyu si ndo alikuwq anachomq nyavu za wavuvi? Huyu si aliwapora wananchi hearing 300 za ardh huko moro huyu?
Sisi tunao kaa mwanza,tunaofadika na ziwa tunamwomba rena rais ampe mpina wizara ya maliasili na uvuvi,kwa sasa uvuvi wa kutumia makokolo umeanza tena,mpk sumu wanavulia,kwa hiyo wewe unae mtuhumu mpina tunakuona kama mpumbavu furani hivi.
 
Wote sawa tu hata huyo mpina hamanishi ni vile kapokonywa chakula/ uwaziri! Huyu si ndo alikuwq anachomq nyavu za wavuvi? Huyu si aliwapora wananchi hearing 300 za ardh huko moro huyu?
Haitoshi tu kusema "...alichoma nyavu za wavuvi....", eleza kwa nini hizo nyavu zilichomwa. Zilichomwa bila ya sababu yoyote, kwa uonevu tu? Hakuna sheria inayozuia uonevu wa aina hiyo?

Na huko "kupora" sijui unamaana gani hapa?

Kwa hiyo wewe unawafahamisha watu hapa JF kwamba Mpina ni jambazi? Nchi hii hakuna sheria kiasi kwamba "mporaji" bado anaruhusiwa kuwa Bungeni?

Watu wa aina yako mnadharau akili za watu wengine kwa kudhani kwamba ukisema chochote watu hao watakiamini kwa vile hawana akili kama ulivyo wewe.
 
Hata KAMA nini mimi lazima nigechoma tu Hayo makokoro waafrika tunapenda sana kujiangalia sisi kwa wakati huu .mtu anavua hadi viluwiluwi sojui kesho atavua nini
Mbona leo upo sawa! Kuna nyakati huwa unapungukiwa akili?
 
Inawezekana hii ikawa kweli, haya uliyosema hapa, na nikwambie siayaafiki kabisa mambo kama hayo.

Lakini kwa sasa kwa mwonekano na kazi anayofanya Mpina huko Bungeni, yaweke haya pembeni angalia haya yanayoendelea.

Tukumbushane kwa wakati mwafaka kama haya bado utakuwa umeyashikilia moyoni. Wakati huo ukifika, tumwangalie Mpina wa sasa na rekodi yake, na tumpime pia kwa mzani wa hayo mabovu aliyoshiriki huko nyuma.

Tutampima kama atajitokeza na apewe hukumu yake na wananchi anayostahiri tukiangalia haya na hayo unayoeleza sasa.
Kwa sasa hivi acha afanye hii kazi, maanake siioni kuwa kazi anayofanya ni ya kuwaumiza wananchi, sasa kwa nini tusimsikilize?
 
Wafugaji ni pasua kichwa. Bonde la kilombero ni eneo oevu, hawatakiwi kuwepo kabisa ila serikali imekaa kimya mpaka wafugaji wakajaa kule na kuwa tatizo kubwa sana wanatishia uhai wa vyanzo vya maji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…