Mwamba wa Lusaka, Clatous Chota Chama kutua Jangwani!

Taarifa za ndani ni kwamba bado Simba wanajadili mahitaji ya Chama kwa ajili ya mkataba mpya.

Inaelezwa kuwa nyota huyo anahitaji pesa ya usajili shilingi milioni 250 kwa mkataba wa miaka miwili na mshahara wa Shilingi milioni 16 kwa mwezi. Siyo uongo kuhusu Yanga kumtaka Chama.

Taarifa tulizonazo ni kwamba Yanga wametenga dau nono zaidi ya Simba lakini tatizo ni kwamba tayari Chama ana ofa kubwa zaidi Afrika Kusini na Uarabuni na iwapo atashindwana na Simba, hatamani kujiunga na timu yoyote ya Tanzania.

Lolote linaweza kutokea, lakini ni wazi kuwa Simba hawapo tayari hata kidogo kumpoteza Chama.

Zipo fununu kuwa dau walilotenga Yanga linafikia Milioni 300 na mshahara wa milioni 18 kwa mwezi, lakini ipo nadharia pia kwamba Yanga wanawachezea Simba mchezo ili watumie pesa nyingi zaidi ya walivyopanga katika dili hilo.
 
Msiba huko msimbazi utakuwa si nchi hii boss.
Atakuwa mpumbavu kama akisaini hapa Tanzania tena.

Kwa kiwango alichoonesha alipaswa asogee mbele zaidi na si kubaki level ile ile.
 
Nini kinakwamisha kwa masheikh wa kaskazini na kwa madiba kama umekubali kuwa Chama ni mchezaji mzuri?
Chama ni mchezaji mzuri kwa afrika mashariki lakini sio kwa wale masheikh wa kaskazini au kwa madiba ndo maana hawashoboki nae. Kama jamaa wangemtaka tena ni free agent wangembeba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…