Mwambie mdogo wako anaenda shule kusomea taaluma sio kazi, anaweza kusoma uhasibu akawa dobi

Hizi taarifa wazazi inatakiwa mzitumie Kama ushauri wa mwisho kwa Watoto wenu wanaoenda kuanza masomo ya mwaka wa kwanza Maana Najua wengi bado wanamiliki Nokia za tochi Ila wakirudi likizo utashangaa wanarudi na Sumsung+Apple[emoji519].
 
Kwamba Mwanza ina nini hasa mpaka aliyetoka Mbeya akatae kwao Green city?? Mfano hauna uhalisia
 


1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi. Anaweza somea ualimu akawa mhudumu wa bar au boda boda.

2. Mwambie kufaulu taaluma sio kufaulu maisha. Wapo watu wenye elimu kumzidi yeye ila hawana ajira. Hata wenye ajira bado maisha magumu.

3. Mwambie kupata alama nyingi sio kujua mambo mengi. Wapo walio kuwa wanashika nafasi za kwanza darasani ila leo wanazidiwa uchumi na wenzao walio onekana hawana akili.

4. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji. Ila akumbuke anatokea kijijini au wilaya iliyo duni, tena kule ndanindani. Hivyo asijikweze ili aonekane.

5. Mwambie marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester. Kuendelea kung'ang'ania wale wa awali ataisoma namba. Akumbuke chuo ndiko mlokole hujifunza kwenda club, kulewa na kuvaa nguo za ajabu.

6. Mwambie semester 1 atakuwa na wapenzi wengi sana ila atumie kinga kwa gharama yoyote ile. Kama ni wa kike akumbuke anasubiriwa na wale wa mwaka wa 2 na 3 ili asajiliwe katika orodha ya kontena jipya.

7. Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni.bAtapata marafiki wapenda starehe. Pesa zake zitaisha.

8. Mwambie boom huwa linakuja ila laki 5 ya chuoni sio laki 5 ya nyumbani. Hela ya chuoni huisha haraka na bila mpangilio hivyo awe makin katika matumizi yake.

9. Mwambie chuoni hakuna ndoa iila kuna uzinzi. Hivyo aache kubeba majukumu ya ndoa ikiwa kaenda kusoma. Mwambie kuishi kiunyumba na girl au boy kama wana ndoa sio ujanja ila ni ulimbukeni na kesho ataumbuka.

10. Mwambie awe na msimamo na asikurupuke kuanzisha mahusiano chuoni ikiwa nyumban ana mtu anayempenda kwa dhati. Chuoni kuna watu wapo kuharibu malengo ya wengine awe makini.

11. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanatamaa ya ngono hivyo akiwa mvivu darasani basi atafeli na ili apewe marks itabidi awe tayari kumvulia chupi kila muhadhiri, ambao wengi wao wagonjwa.

12. Mwambie chuoni kuna makanisa na misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 1,000 lakini waumini ni wachache. Akumbuke kusali.

13. Mwambie kama ni wa kike kuwa aridhike na hali ya nyumbani. Asifikirie kutafuta sponsor ili kupunguza ugumu wa maisha. Atajiingiza katika matatizo makubwa.

14. Mwambie kuwa asiwadharau watu alio soma nao nyuma kisa hawajapata nafasi kufika chuo. Siku akimaliza chuo wapo ataobwakuta wana biashara kubwa hivyo kumpa kibarua.

15. Mwambie simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima. Hivyo asipende tumia vibaya pesa ambayo anapewa kwa awamu maana siku atazikumbuka akimaliza masomo.

16. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau. Awaepuke marafiki wanafiki wanao mfundisha kutafuta wanawake au wanaume.

17. Mwambie chuoni ni sehemu ya kutengeneza connection na watu muhimu. Akae mbali na watu wasio msaada kwake.

18. Mwambie chuoni kuna watumishi wanao jiendeleza. Husoma huku wakiendelea kupokea mshahara wengi wao ni waume na wake za watu. Hawa ndo wanaotumia pesa zao kulaghai mabinti na vijana.

19.Mwambie pia baada ya kumaliza chuo haina maana amefanikiwa maisha. Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia. Anapowaona kaka na dada zake wamemaliza chuo ila wapo tu mtaani asifikiri ni wazembe ila usawa na mfumo unabana.

20. Mwambie maisha ni mafupi sana. Adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazuri. Lastly asimdharau mtu yeyote. Akumbuke na azingatie kuwa kuna maisha baada ya chuo.

Asijisahau sana maana mtaani kugumu. Mabinti wenye degree wanaamua kuolewa na vibabu nao vijana kutembea na wazee sababu ya kukosa ajira.

Atambue kuwa leo hii dereva boda boda au bajaji ana uhakika wa kuilisha familia yake kila siku kuliko muhitimu wa chuo kikuu. Hivyo asiwe na dharau kuwa hawezi olewa na mtu mwenye elimu ya chini.

Pia akumbuke sio kila dereva au konda hajasoma. Watu wana vyeti vyao na ufaulu mzuri.
 
Ushauri mzuri sana kwa vijana endapo wataufuata..
 
CHUO kinaweza kuwa CHOO

Mkumbushe ndugu au rafiki yako kuwa maisha ya CHUO ni sawa na BONGO MOVIE watu wengi huigiza. Hata yule wa MBEYA vijijini atasema kwao MWANZA.

1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi. Anaweza somea Ualimu akawa mhudumu wa Bar au boda boda

2. Mwambie Kufaulu Taaluma sio Kufaulu maisha.wapo watu wenye elimu kumzid yeye ila hawana ajira. Hata wenye ajira bado maisha magumu

3. Mwambie Kupata alama nyingi sio kujua mambo mengi. Wapo walio kuwa wanashika nafas za kwanza darasan ila leo Wanazidiwa uchumi na wenzao walio onekana hawana akili

4. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji. Ila akumbuke anatokea kijijini au wilaya iliyo duni, tena kule ndanindani. Hivyo asijikweze ili aonekane

5. Mwambie Marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester. Kuendelea kung'ang'ania wale wa awali ataisoma namba. Akumbuke chuo ndiko mlokole hujifunza kwenda Club, kulewa na kuvaa nguo za ajabu

6. Mwambie semester 1 atakuwa na wapenzi wengi sana ila atumie kinga kwa gharama yoyote ile, kama ni wa kike akumbuke anasubiriwa na wale wa mwaka wa 2 na 3 ili asajiliwe katika orodha ya Kontena jipya.

7. Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni. Atapata marafiki wapeta starehe. Pesa zake zitaisha

8. Mwambie Boom huwa linakuja ila Laki 5 ya chuoni sio Laki 5 ya nyumbani, hela ya chuoni huisha haraka na bila mpangilio hivyo awe makin katika matumiz yake.

9. Mwambie chuoni hakuna. NDOA ila kuna uzinzi.. Hivyo aachane kubeba majukumu ya ndoa ikiwa kaenda kusoma. Mwambie kuishi kiunyumba na girl au boy kama wana ndoa sio ujanja ila ni ulimbuken na kesho ataumbuka

10. Mwambie awe na msimamo na asikurupuke kuanzisha mahusiano chuoni ikiwa nyumban ana mtu anayempenda kwa dhati. Chuoni kuna watu wapo kuharibu malengo ya wengine awe makini

11. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanatamaa ya ngono hivyo akiwa mvivu darasani basi atafeli na ili apewe Marks itabid awe tayari kumvulia chupi kila muhadhiri ambao wengi wao wagonjwa

12. Mwambie Chuoni kuna Makanisa na Misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 1000 lakini waumini ni wachache. Akumbuke kusali.

13. Mwambie kama ni wa kike kuwa aridhike na hali ya nyumbani. Asifikirie kutafuta SPONSOR ili kupunguza ugumu wa maisha. Atajiingiza katika matatizo makubwa

14. Mwambie kuwa asiwadharau watu alio oma nao nyuma kisa hawajapata nafas kufika chuo. Siku akimaliza chuo wapo ataowakuta wana biashara kubwa hivyo kumpa kibarua

15. Mwambie Simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima. Hivyo asipende tumia vibaya pesa ambayo anapewa kwa awamu maana siku atazikumbuka akimaliza masomo

16. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau. Awaepuke marafiki wanafiki wanaomfundisha kutafuta wanawake au wanaume

17. Mwambie chuoni ni sehemu ya kutengeneza Connection na watu muhimu, akae mbali na watu wasio msaada kwake

18. Mwambie chuoni kuna watumishi wanao jiendeleza, husoma huku wakiendelea kupokea mshahara wengi wao ni waume na wake za watu. Hawa ndo wanaotumia pesa zao kulaghai mabinti na vijana

19. Mwambie pia baada ya kumaliza chuo haina maana amefanikiwa maisha. Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia. Anapowaona kaka na dada zake wamemaliza chuo ila wapo tu mtaani asifikiri ni wazembe ila usawa na mfumo unabana

20. Mwambie Maisha ni mafupi sana Adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazurii, Lastly Asimdharau mtu yeyote. Akumbuke na azingatie kuwa kuna maisha baada ya chuo.

Asijisahau sana maana mtaani kugumu.. Mabinti wenye DEGREE wanaamua kuolewa na vibabu nao vijana kutembea na wazee sababu ya kukosa ajira.

Atambua kuwa leo hii dereva boda boda au bajaji ana uhakika wa kuilisha familia yake kila siku kuliko muhitimu wa chuo kikuu. Hivyo asiwe na dharau kuwa hawezi olewa na mtu mwenye elimu ya chini

Pia akumbuke sio kila dereva au konda hajasoma, watu wana vyeti vyao na ufaulu mzuri

Kama haelewi basi tumuache

Tumsubiri akimaliza.

IKIKUFAA IFANYIE KAZI

MUNGU AWAONGOZE KATIKA NJIA ILIYO SAHIHI NA AWAPE UJUZI UTAKAOWASAIDIA HATA KAMA WATAKOSA AJIRA.

Ameen..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…