Disc Joker
Member
- Jun 21, 2019
- 41
- 59
Mkuu una pepelusha ndege wetu [emoji28]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ushauri mzuri sana kwa vijana endapo wataufuata..![]()
1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi. Anaweza somea ualimu akawa mhudumu wa bar au boda boda.
2. Mwambie kufaulu taaluma sio kufaulu maisha. Wapo watu wenye elimu kumzidi yeye ila hawana ajira. Hata wenye ajira bado maisha magumu.
3. Mwambie kupata alama nyingi sio kujua mambo mengi. Wapo walio kuwa wanashika nafasi za kwanza darasani ila leo wanazidiwa uchumi na wenzao walio onekana hawana akili.
4. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji. Ila akumbuke anatokea kijijini au wilaya iliyo duni, tena kule ndanindani. Hivyo asijikweze ili aonekane.
5. Mwambie marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester. Kuendelea kung'ang'ania wale wa awali ataisoma namba. Akumbuke chuo ndiko mlokole hujifunza kwenda club, kulewa na kuvaa nguo za ajabu.
6. Mwambie semester 1 atakuwa na wapenzi wengi sana ila atumie kinga kwa gharama yoyote ile. Kama ni wa kike akumbuke anasubiriwa na wale wa mwaka wa 2 na 3 ili asajiliwe katika orodha ya kontena jipya.
7. Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni.bAtapata marafiki wapenda starehe. Pesa zake zitaisha.
8. Mwambie boom huwa linakuja ila laki 5 ya chuoni sio laki 5 ya nyumbani. Hela ya chuoni huisha haraka na bila mpangilio hivyo awe makin katika matumizi yake.
9. Mwambie chuoni hakuna ndoa iila kuna uzinzi. Hivyo aache kubeba majukumu ya ndoa ikiwa kaenda kusoma. Mwambie kuishi kiunyumba na girl au boy kama wana ndoa sio ujanja ila ni ulimbukeni na kesho ataumbuka.
10. Mwambie awe na msimamo na asikurupuke kuanzisha mahusiano chuoni ikiwa nyumban ana mtu anayempenda kwa dhati. Chuoni kuna watu wapo kuharibu malengo ya wengine awe makini.
11. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanatamaa ya ngono hivyo akiwa mvivu darasani basi atafeli na ili apewe marks itabidi awe tayari kumvulia chupi kila muhadhiri, ambao wengi wao wagonjwa.
12. Mwambie chuoni kuna makanisa na misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 1,000 lakini waumini ni wachache. Akumbuke kusali.
13. Mwambie kama ni wa kike kuwa aridhike na hali ya nyumbani. Asifikirie kutafuta sponsor ili kupunguza ugumu wa maisha. Atajiingiza katika matatizo makubwa.
14. Mwambie kuwa asiwadharau watu alio soma nao nyuma kisa hawajapata nafasi kufika chuo. Siku akimaliza chuo wapo ataobwakuta wana biashara kubwa hivyo kumpa kibarua.
15. Mwambie simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima. Hivyo asipende tumia vibaya pesa ambayo anapewa kwa awamu maana siku atazikumbuka akimaliza masomo.
16. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau. Awaepuke marafiki wanafiki wanao mfundisha kutafuta wanawake au wanaume.
17. Mwambie chuoni ni sehemu ya kutengeneza connection na watu muhimu. Akae mbali na watu wasio msaada kwake.
18. Mwambie chuoni kuna watumishi wanao jiendeleza. Husoma huku wakiendelea kupokea mshahara wengi wao ni waume na wake za watu. Hawa ndo wanaotumia pesa zao kulaghai mabinti na vijana.
19.Mwambie pia baada ya kumaliza chuo haina maana amefanikiwa maisha. Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia. Anapowaona kaka na dada zake wamemaliza chuo ila wapo tu mtaani asifikiri ni wazembe ila usawa na mfumo unabana.
20. Mwambie maisha ni mafupi sana. Adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazuri. Lastly asimdharau mtu yeyote. Akumbuke na azingatie kuwa kuna maisha baada ya chuo.
Asijisahau sana maana mtaani kugumu. Mabinti wenye degree wanaamua kuolewa na vibabu nao vijana kutembea na wazee sababu ya kukosa ajira.
Atambue kuwa leo hii dereva boda boda au bajaji ana uhakika wa kuilisha familia yake kila siku kuliko muhitimu wa chuo kikuu. Hivyo asiwe na dharau kuwa hawezi olewa na mtu mwenye elimu ya chini.
Pia akumbuke sio kila dereva au konda hajasoma. Watu wana vyeti vyao na ufaulu mzuri.