Mwambieni Haji Manara asijivishe U-mungu

Mwambieni Haji Manara asijivishe U-mungu

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Anakera sana huyu mtu. Sijui nani alimwabia yeye ndiye kila kitu katika hii dunia?

Halafu akiambiwa ukweli anajificha kwenye upungufu wa melanin kwenye ngozi yake (albinism) na kuanza kuomba huruma kwa umma. Haya siyo maneno ya kuongea hata kidogo.


IMG-20211024-WA0008.jpg
 
huyu jamaa hawezi kunyamaza kabisa mambo mengine ni kula kinya tu tatizo mdomo
 
GoooooooaaaaaaaaaaaaAAAAAaallllllllll
 
Watanzania wengi wanaamini huo upuuzi wake wa Karma na takataka nyingine za aina hiyo.

Hili si suala la Manara peke yake
Anakera sana huyu mtu. Sijui nani alimwabia yeye ndiye kila kitu ktk hii dunia?

Halafu akiambiwa ukweli anajificha kwenye upungufu wa melanin kwenye ngozi yake (albinism) na kuanza kuomba huruma kwa umma. Haya siyo maneno ya kuongea hata kidogo.

View attachment 1985591
 
Nadhani muda sahihi ya kumpuuza sasa

Ni moja ya watu wanaoishi kwa janja janja hawana taaluma yoyote ya kueleweka na wanamna hii hua hawadum popote pale, kuelezwa kashindwa kuendesha ndoa zake kila siku anaoa na kuacha imekua nongwa wakati kaelezwa kitu cha kweli japo aliekieleza hakutakiwa kukueleza mazingira yale ya press ya kuhamasisha mashabiki, ilikua amuandikie kama utani kwenye page zao huko
 
Kwanza hawa wahamasishaji ni kazi ambayo haiongezi chochote kwani mashabiki wa Simba na Yanga ni watu ambao popote walipo wapo royal kwa timu zao ni kazi ya viongozi kutengeneza timu bora na kusajili vizuri na kuweka benchi la ufundi lenye tija kwani timu ikishinda mashabiki wenyewe watajaa kila mechi na jezi watanunua tu bila kuhamasishwa, huu ujanja ujanja kwenye mpira haufai kwani unatupoteza kama taifa na matokeo yake tunakua na timu ya taifa mbovu kuliko kawaida.
 
Anakera sana huyu mtu. Sijui nani alimwabia yeye ndiye kila kitu ktk hii dunia?

Halafu akiambiwa ukweli anajificha kwenye upungufu wa melanin kwenye ngozi yake (albinism) na kuanza kuomba huruma kwa umma. Haya siyo maneno ya kuongea hata kidogo.

View attachment 1985591
Pole sana,lkn kwa mtazamo wangu hapo hajafikia hata robo ya robo ya yale aliyowafanyia Yanga...

Mna safari ndefu sana na huyu jamaa,mashabiki wa Yanga walikuwa wanasema hayo hayo na nyie mlikuwa mnazidi kumpa kichwa[emoji3525][emoji3525]
 
Saizi yake mwijaku, katekenywa kidogo tu na mwijaku kaanza kulia lia,, ili kumkomesha simba inabidi wamuongeze dida achambane nae,, jamaa mbulula kweli huyu,, yani matokeo yoyote mabaya yanayoikuta simba kwa akili yake anajua sababu ni yeye wakati huo ndio mpira, kafungwa man u 5 leo mpira ulivyo na matokeo katili
 
Kwa mujibu wa Haji Simba itafungwa mechi zote kwasababu yeye Haji kafukuzwa Simba.

Yaani sijaona timu ambayo haijawahi kufungwa na kwamba Simba ikifungwa basi nikwasababu ya kumtimua msemaji wa timu.

Hii ndio sababu Kwa mujibu wa Haji, unajiuliza kwanini yeye mtaalamu wa kushinda hakusababisha Yanga ishinde dhidi ya Rivers?

Kaka yetu anahasira Sana za kuachwa na Simba.
 
Back
Top Bottom