Mwambieni kocha Fadlu mashabiki wa Simba tumechoka na ufundishaji wake wa 'Back Pass'

Sidhani kama Fadlu ndiye anawafundisha hizo mnaita "back-passes".

Ukiangalia goli ambalo Chasambi kajifunga, Fadlu alikuwa anasisitiza wachezaji wapeleke mpira mbele. Ukiangalia pia goli alilofunga Kapombe mechi iliyopita dhidi ya Tabora, Fadlu alikuwa anasisitiza muda mrefu waende mbele ila ni kama walikuwa hawamzingatii.

Tatizo la backpasses ni sugu pale Simba limekuwepo kabla ya Fadlu na mimi nimeshawahi kulipigia sana kelele huko nyuma.
 
Ni kweli mkuu. Na bado ujinga mwingine wakishafunga goli moja, mbili au tatu hivi basi wanaanza ujinga wao mwingine wakupigiana pasi fupi fupi wenyewe kwa wenyewe mpaka adui afike badala ya kwenda mbele kuongeza magoli. Na mashabiki wao nao wanawasafia eti pira biriani na wachezaji wakisikia mashabiki wanakaanga chipsi jukwaani ndio wanazidisha show game badala ya kutafuta mtaji wa magoli mengi. Wenzao Yanga wakikuta kibonde wanakung'uta tano au sita. Wakija kulingana pointi mwishoni mwa ligi Yanga ataibuka kidedea kwa uwiano mzuri wa magoli na Simba watapiga kelele nyingi za lawama kumbe uzembe ni wa kwao wenyewe.
 
Umechoka wewe sio tumechoka
Semea nafsi yako boya wewe
 
Yule wa Objective football ndio alikuwa mwenyewe sasa. Pira linapigwa kwenda mbele kulisakama langu la mpinzani MWAMWI
 
Unakosea kusema mashabiki wa Simba walikuwa wanafurahia backpasses. Hakuna ubaya kufurahia udambwidambwi ukifanyika mara moja moja ila hapa tunaongelea backpasses.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…