Maswali ni mengi sana sio hilo tu mkuu. Hivi ni kwanini miujiza ya Mwamposa inahusu watu kujisaidia nyoka, minyoo, jongoo, mende, nge na kufa kwa paka, panya, vyura, vinyonga na wanyama wengine kama hao. Hivi mtu hawezi kupata ukombozi hivi hivi pasipo kutokewa na miujiza ya hawa wanyama na wadudu? Sijawahi kusikia ushuhuda wa waumini wa Mwamposa unaoenda mbali na hivi vimbwanga.