Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanayoyahubiri wao wenyewe hawayafanyi maana wanajua wazi hayana ukweli wowote. Utasikia matangazo yao ya mikutano kwamba wagonjwa waende waombewe wapone. Wao wenyewe wakipata matatizo ya kiafya hawaendi kuombewa wanaenda kutibiwa hospitali nzuri kwa pesa walizochuma kwa wajinga!Yeye mwamposa anajimaliza kwa nani?
Wajinga ndio waliwao. Nchi hii isingekuwa na wajinga akina Mwamposa wangekula wapi?Wanayoyahubiri wao wenyewe hawayafanyi maana wanajua wazi hayana ukweli wowote. Utasikia matangazo yao ya mikutano kwamba wagonjwa waende waombewe wapone. Wao wenyewe wakipata matatizo ya kiafya hawaendi kuombewa wanaenda kutibiwa hospitali nzuri kwa pesa walizochuma kwa wajinga!
Huko kwenye makanisa yasiyo na uratibu wowote ndio matapeli wanakimbilia siku hizi maana wanatapeli mchana kweupe wala hakuna mamlaka inayowatia mbaroni. They have found green pastures wanakula kwa raha zao! Utapeli in the name of Jesus!!!Wajinga ndio waliwao. Nchi hii isingekuwa na wajinga akina Mwamposa wangekula wapi?
Izi go benki izi take olu mane iz givu mwamposa izi not me.Wajinga ndio waliwao.
KaziKweliKweli/JobTrueTrue
Kweli kabisa mkuu. Kuna haja ya serikali kuwachunguza hawa wahuni na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa utapeli wanaowafanyia wapiga kura.Huko kwenye makanisa yasiyo na uratibu wowote ndio matapeli wanakimbilia siku hizi maana wanatapeli mchana kweupe wala hakuna mamlaka inayowatia mbaroni. They have found green pastures wanakula kwa raha zao! Utapeli in the name of Jesus!!!
UmemalizaAtaambatanisha na mstari wa bibilia ili watu wamuamini vizuri
Usipopata ulichokua unakiombea, visingizio vinakua vingi;
huna imani
kila mtu na wakati wake
laana na mikosi
unapitia majaribu
umeshikwa nyota/nyayo/kiganja cha mkono/wingu nk nk
Hii biahara ni fullproof
Hawa mitume ni mtaji wa ccm...
Wataendelea kuwepo na wapya pia watazuka kila siku....
Mwamposa anazidi kuwa tajiri Kwa ujinga wa watuNaingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Mtume Boneface Mwamposa (Bulldozer) amefafanua kwa ufasaha maana ya "sadaka ya kujimaliza" inayotolewa na waumini wa kanisa lake baada ya kupokea shutuma mbalimbali kutoka kwa wananchi kwamba amekuwa akiwakamua waumini hela zote hadi wanakosa nauli ya kurudia majumbani kwao.
Ufafanuzi uliotoka ni kwamba kutoa sadaka ya kujimaliza sio kutoa fedha zote ambazo mtu amekwenda nazo kanisani. La hasha! Maana ya sadaka ya kujimaliza ni kutoa fedha zako zote ulizonazo benki na kuziwasilisha kwa mtume kama sadaka. Kwa mfano, kama una akaunti 5 kwenye benki tofauti, komba pesa zote zilizomo kwenye akaunti hizo umtolee Mungu wako. Hii ndio maana halisi ya sadaka ya kujimaliza. Yaani unajimaliza kabisa na kuanza upya!
Mtume amesema hayo zikiwa zimesalia siku chache kabla ya mkesha wa mwaka mpya unaoenda kwa kaulimbiu ya "vuka na chako" utakaofanyika kanisani kwake katika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe jijini Dar es Salaam.
MAONI YANGU
Binafsi nimewahi kusimuliwa na muumini mmoja aliyetoa sadaka fedha zote alizokuwa nazo hadi nauli lakini wakati anaondoka kwa miguu kuelekea kwake Gongolamboto akitokea Kawe, mtume akamfanyia muujiza akaokota noti ya Tsh 5000 akaitumia kama nauli, yeye na wanawe wawili aliokuwa ameandamana nao.
Afadhali sasa ufafanuzi umewekwa wazi kwani waumini na wananchi walikuwa hasa hawafahamu maana ya sadaka ya kujimaliza. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Mungu wa Mwamposa hajawahi kushindwa.
Nawasilisha.
Pia soma > Sadaka ya kujimaliza ya kwa Mwamposa inatia watu umasikini
View attachment 2978474
Serikali inamchukulia Mwamposa kama mshirika wake kwenye utawala kwa kuwa anasaidia kuwapumbaza maskini ili CCM iwatawale vizuri.Labda kwa mbumbumbu aliyeshindikana ndie anaeweza kulamba pesa zote na kumpelekea binadamu mjanja. Serikali haioni huu upumbavu?
mtu ambaye ni kirusi cha taifa kwa sasa ni Mwamposa. anapaswa kushughulikiwa!Serikali inamchukuliaMwamposa kama mshirika wake kwenye utawala kwa kuwa anasaidia kuwapumbaza maskini ili CCM iwatawale vizuri.