Mwamposa avunja rekodi zote tangu Tanzania iwepo kwa Kujaza watu viwanja vyote vya KAWE Jijini Dar es salaam

Mwamposa avunja rekodi zote tangu Tanzania iwepo kwa Kujaza watu viwanja vyote vya KAWE Jijini Dar es salaam

Nipo hapa Kawe Mungu wa Mwamposa kajaza viwanja vyote vya Kawe Jijini Dar es salaam.

Inakadiriwa Kuna wanaume zaidi ya 400,000 bila kuhesababu Wanawake na watoto.

Je, Watu hawa wote ni wajinga na Wapumbafu au na wewe uliyeko nyumbani ufuatilie kwa TV au kama uko Dar ufike Mara moja?​
Ukiwa YOTUBE
Ukiwa Tiktalk,
Facebook
Instagram​
Unajua maana ya watu Laki 4 lakini??? Unajua Stadium la Benjamin Mkapa likijaa full watu ni watu Elfu 60 tu?? Sasa kusema watu Laki 4 tena wanaume tu, hujaweka idadi ya wanawake ambao kwa kawaida ndio huwa wamelogwa zaidi na hawa "manabii".... Unataka kutuambia viwanja vya Kawe vinaweza kukusanya watu laki 8???
 
Si wajinga bali umasikini na maradhi yanayotokana na ukosefu wa huduma bora za afya.
 
Niko kawe hapa kuna foleni naona waumini ndo wanarudi home
 
Inaonesha na kudhihirisha jinsi WADANGANYIKA tulivyo desparate, njaa, dhiki, shida, UZUZU, elimu ndogo, kukosa muelekeo, kukosa imani na serikali yetu, tunakimbilia Udini, imani, tukidhani itatutalia hayo yote!
Kweli GEN Z WABABE, DINI HAITATUI SHIDA WEWE MWENYEWE NA MAAUMUZI YAKO TU.
MWAMPOSA NI TAPELI WA KIROHO KAMA KINA JOSHUA NK.NK
 
Unajua maana ya watu Laki 4 lakini??? Unajua Stadium la Benjamin Mkapa likijaa full watu ni watu Elfu 60 tu?? Sasa kusema watu Laki 4 tena wanaume tu, hujaweka idadi ya wanawake ambao kwa kawaida ndio huwa wamelogwa zaidi na hawa "manabii".... Unataka kutuambia viwanja vya Kawe vinaweza kukusanya watu laki 8???
Hiyo si wilaya nzima au pemba yote hao laki 8, jamaa kapamba hadi kaharibu
 
Hapo manake zimepigwa chain familia zaid ya Milioni moja hutawaambia kitu kuhusu Mwampopo
Ukiwa na ndugu au jamaa mmoja anaesali kwa Mwamposa utajua namansha nini
 
Kwa wanaotumia usafiri wa Umma njia ya kawe haipitiki, nimekaa zaidi ya saa zima kwenye foleni kwa kipande kidogo tuu kutoka pale bondeni mpaka round about ya kawe
 
Back
Top Bottom