Tetesi: Mwamposa mbioni kuinunua E-FM, TV-E

Uongo

Mwamposa hana mpango wa kununua hiyo radio. Wala majizzo hana mpango wa kuiuza

Majizzo yupo karibu na mwamposa sababu mwamposa anataka kufungua radio/tv yake so huyo ni kama mentor wake
 
Leo Vishu umeacha utata, umetema facts.
Safi.
Daaah haya, ila kwa kukupa siri tu taarifa zako huwa naziamini kwa asilimia kadhaa.

Bila shaka wewe ni mbea msomi, sijui ni jina gani linakufaa mbali na mbea au kufananishwa na wambea wapuuzi puuzi.
 
ebwa

ebwana dah genge kipind changu pendwa miaka na miaka toka kipind kile anafanya kicheko mtata mpaka miaka hii ya kina fido na samio ..
sema dah sijaskiliza redio siku nyingi tuko mikoani uku kwenye hrkt za kujikomboa na umaskin.
Na hicho ndo kipindi Bora kilichobakia efm, vile vingne vyote watangazaji hawana ubunifu yaan ni kusoma matangazo tu kwisha na kuongea story kidogo za kawaida kbsaa kwa kifupi hawanaga jipya. Vipindi vya michezo ndo vile vile tu
 
😂😂😂😂 Wajinga ndio waliwao,. Wanapata fedha wanazipeleka huko
 
Hata Bwana Yesu alifuatwa na makutano tena wengi ni wanawake imagine kama wale waliolishwa mikate na samaki walikua ni wanaume 5000 ukitoa wanawake na watoto ambao walikua hawahesabiki kwa hiyo usiogope show ya Jesus inaendelea alipoishia Mwamposa anaendeleza
Hutaki ishara na uponyaji weye?
😁😁
 
Afadhali, atuachie ITV yetu tutazame Al Jazeera usiku mpaka asubuhi!
 
KM Hawana ht Hela ya kula na ya kulala kwenye nyumba za wageni ,anakuwaje na Hela ya kumwachia Mwampos?

Ndugu shida zisikie tu,usiombe yakukute hata utahangaika
 
Tena ht mwam
Posa hawezi maliza Kuna wengine watapokea ,kazi inaendelea
 
KM Hawana ht Hela ya kula na ya kulala kwenye nyumba za wageni ,anakuwaje na Hela ya kumwachia Mwampos?

Ndugu shida zisikie tu,usiombe yakukute hata utahangaika
Hao viumbe wako radhi wasile ila wakajimalize na sadaka.. Kwani si tunakutana nao wakiomba omba hela ili wapate nauli ya kurudi makwao. Wengine wanatembea umbali mrefu kwasababu washajimaliza kwa kutoa vyote walivyokuwa navyo.

Kakudanganya nani shida zitaisha kwakuombea na binadamu mwenzako?

Unadhani hii akili wangekuwa nayo china,Japan, Ujerumami hata Israel Wangekuwa hapo unapowaona?

Mlokole yoyote hapigi hatua kwenda mbele ila atazidi kurudi nyuma . Atauza kila kitu anufaishe nabii/mtume wake ambae anaishi maisha ya kifahari yasiyo elezeka.

Na hilo ndo tishio lenu eti hujapata shida.
Kama ni maradhi basi Hospitali zipo . Kama ni shida za hela najua hela hainaga miujiza zaidi ya kutafutwa. Na tatizo lolote haliwezi kutatuliwa kwa kukanyaga mafuta au kuombewa zaidi ya kufata kanuni za ulimwegu
 
Baada ya ule mkesha,.
Nilipita maeneo ya TMJ hopistali mikocheni na kupishana na makundi ya wanawake na watoto wakitembea kwa miguu.wametoka mkesha na wanarudi kwao kinondoni, Mwananyamala na magomeni ni umbali wa kilometa 14.
Ukiwaangalia hali zao unapata picha aina ya waumini wa yule jamaa
 
Na hapo lazima walitoa sadaka, wakanunua maji na mafuta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…