Tetesi: Mwamposa mbioni kuinunua E-FM, TV-E

Tetesi: Mwamposa mbioni kuinunua E-FM, TV-E

Hapo tatizo unakuta hakuna mfumo wa uongozi ulio clear, pesa ya kampuno inatakiwa itoke kwa kufuata muongozo wa kampuni wa ulipaji au vikao rasmi.
Heheh kikao si ni whatsapp family chat inapitisha. Kwakifupi waafrika huwezi kuwatengenanisha na kampuni zao interms of matumizi. Ukikataa muhasibu watakuambia hizi mali si zako. Hujui tulipozipata. Kama umekua kiburi kesho tutaleta muhasibu mwingine.
 
Juzi napita kawe, nawaon wamama wamelala kwenye kordo za watu na watoto wao wakisubiria mkesha.
Ni wamama ambao ukiangalia hali zao zinatia huruma sana. Hawana hela za kulipia Vyumba vya wageni hata chakula sa ingine. Ila wanaenda kuacha hela zote tena kwa mtume wao ambae ni Billionea .

Naumiaga sana namna ya hao wamama kwa ujinga wao wanavyowatesa watoto kukesha na kuambatana nao kila mahali ilihali mtoto hajafika umri wa maamuzi.
Kumbe sio mimi peke yangu? Sasa Mkuu sisi tunaotumia usafiri wa umma wa magari yanayoelekea huko kanisani kwake ndio kila siku za mikutano/ibada nakutana nao wakiwa wamejazana kwenye gari watoto wadogo wamechoka naumia sana.

Wamama wenyewe ukiwatazama wanatia huruma kuliko hao watoto, wamejazana na chupa za maji kwenye gari wako hoi hadi wanapitiliza vituo!
 
View attachment 3184579

Katika kilichoonekana kama kusogeza ‘huduma’ karibu kwa waumini wa kanisa lake, Askofu na Mtume Boniface Mwamposa yupo kwenye mchakato wa kuinunua EFM Company Limited.

EFM ni kampuni iliyosajiliwa kama chombo cha habari, ikiwa na umiliki wa Redio na Televisheni.

Mwamposa na Mkurugenzi wameshibana…
Mkurugenzi wa EFM Bwana Francis Ciza maarufu kama Majizzo (Mume wa muigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’) wamekuwa wakishirikiana kwa ukaribu na Askofu Mwamposa katika kurusha matangazo ya moja kwa moja ya mikutano na ibada zinazoendeshwa na Mwamposa kwa kipindi kirefu.

Baada ya kufanya kazi pamoja kwa kipindi kirefu, hivi sasa wapo kwenye mazungumzo ya kumuuzia media hiyo Mwamposa.

Nimetaarifiwa kwamba vikao vya mauziano hayo vinafanyika kwa siri nyumbani kwa Majizo, huku dau likiwa bado halifahamiki lakini ikielezwa Majizzo anataka dau kubwa linalokwamisha taratibu za mauziano kuanza.

EFM Radio imemshinda Majizzo!
Kwa kipindi kirefu kumekuwa na minong’ono ya wafanyakazi kushindwa kulipwa mishahara kwa wakati, ikisemekana wanaolipwa bila kusumbuliwa ni wale watangazaji wenye majina makubwa pekee, huku wale wachanga wakipitia wakati mgumu kimalipo.

Taarifa za uhakika ni kwamba redio hiyo imemshinda Majizzo, changamoto za uendeshaji zimemuelemea na inasemekana kama sababu kuu ya yeye kufikia uamuzi wa kumuuzia Mwamposa kampuni yote hiyo ya habari iliyokuja kuzipa chachu redio kongwe miaka ya mwanzoni mwa uzinduzi wake.

Majizzo siye mmiliki pekee…
Taarifa za usajili wa kampuni zinaonesha kumilikiwa na ndugu watatu, yeye Majizzo (Francis Ciza 40%) ndugu zake kwa upande wa baba yake mlezi Mzee Ciza… Jean Ciza 40% pamoja na Justine Ciza 20%

Wenu katika unyetishaji, mimi na chanzo changu,

Nifah.
sawa dada makamasi chaumbea
 
Hii radio kwa Sasa haishawishi kbsaa, watangazaji wake hawana content kbsaaa hasa wale wa joto la asubuhi, yaan angalau kipindi kizuri kwa Sasa kweny hii radio ni "Genge"tu kile Cha usiku.
Sasa watangazaji hawalipwi vizuri miaka nenda rudi ari wataipata wapi?
Wanajikongoja hivyohivyo.
 
Hapo unakuta money withdrawn for family use kwenye kampuni ndio kipengele kikuu kinachokwamisha taasisi. Nimewahi kufanya kazi kwenye taasisi za kifamilia kama Hizo. Sikukuu kama christmas muhasibu unaforciwa kufanya transfer ya 15m kwa kila mwana familia ( kwa sikuku ya siku moja) na ilihali mishahara ya staff hawatoi approval. Unakuta familia inainyonya kampuni
Tunaofanya kazi kwenye kampuni za familia hiki ulikosema ni kama kupitisha kisu cha moto kwenye siagi, umekata kisawasawa.
 
ebwa
Hii radio kwa Sasa haishawishi kbsaa, watangazaji wake hawana content kbsaaa hasa wale wa joto la asubuhi, yaan angalau kipindi kizuri kwa Sasa kweny hii radio ni "Genge"tu kile Cha usiku.
ebwana dah genge kipind changu pendwa miaka na miaka toka kipind kile anafanya kicheko mtata mpaka miaka hii ya kina fido na samio ..
sema dah sijaskiliza redio siku nyingi tuko mikoani uku kwenye hrkt za kujikomboa na umaskin.
 
Back
Top Bottom