Adimu
JF-Expert Member
- Aug 22, 2013
- 661
- 297
Ninaandika uzi huu kwa maslahi ya ligi yetu na ustawi wa soka letu liweze kupiga hatua. Katika mchezo wa tarehe 10/4/2022 mwamuzi wa akiba Eli Sasii alionyesha maumivu ya wazi kabisa kutokana na matokeo ya pale Kilimanjaro kati ya Polisi Tanzania dhidi ya Simba.
Hii imejidhihirisha kwa vitendo vya kukosa weledi kabisa hasa kulingana na kazi yake na uhusika wake kwenye mechi kati ya Geita gold dhidi ya Yanga. Jambo la kwanza ni kitendo cha yeye kushangilia goli la Geita Gold.
Kitu cha pili ni kitendo cha mshambuliaji wa Yanga Fiston kalala Mayele kukanyagwa kwa makusudi mchezo ukiwa umesimama na beki wa Geita gold Kelvin Yondani na kocha wa Yanga alipokwenda kwa mwamuzi wa akiba Eli Sasii kulalamika huyu mwamuzi alimjia juu na kumtolea maneno makali na kisha kumuita mwamuzi wa kati akimuelekeza kumpa kadi nyekundu kocha wa Yanga.
Kama haitoshi mwamuzi huyu wa akiba alidiriki kulusha chupa ya maji kwa mashabiki wa Yanga huu ni upuuzi uliotukuka. Mamlaka husika natambua mnaweza kupitia hili na huenda mliona pia pale uwanjani, sasa kazi ni kwenu kuwakumbatia watu kama hawa au kuwaadabisha kwa maslahi ya soka letu.