Mwamuzi Omar Artan atalipwa Posho yote ya Kombe la Dunia, licha ya kunyimwa Visa ya Marekani

Mwamuzi Omar Artan atalipwa Posho yote ya Kombe la Dunia, licha ya kunyimwa Visa ya Marekani

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mwamuzi wa Womalia, Omar Artan, ambaye alinyimwa visa ya kuingia nchini Marekani kuchezesha Kombe la Dunia linaloendelea la 2026, atalipwa posho yake yote ya mashindano hayo.

1781438084038.png

Vyanzo vya habari vimeiambia BBC Sport kwamba, ingawa Artan hatashiriki kabisa katika Kombe la Dunia, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) imeahidi kumlipa stahiki zake alizokuwa anastahili kulipwa endapo angechezesha.

Waamuzi hawajui kiasi halisi cha fedha watakachopokea kwa ajili ya kuchezesha Kombe la Dunia, ambacho huwa kinalipwa baada ya mashindano hayo kumalizika.

1781436661927.png

Pia, Soma:
 
Kunyimwa Viza kwa huyu Msomali kumemfungulia maisha sana.
Akibaki katika kutumika u Refa kwa haki na weledi basi ndo mwanzo wa utajiri wake mkubwa.

Kila michuano mikubwa itakuwa inamgombania ili kuwa kivutio cha watu wengi kufatilia michuano hiyo Husika
 
Mwamuzi wa Womalia, Omar Artan, ambaye alinyimwa visa ya kuingia nchini Marekani kuchezesha Kombe la Dunia linaloendelea la 2026, atalipwa posho yake yote ya mashindano hayo.

Vyanzo vya habari vimeiambia BBC Sport kwamba, ingawa Artan hatashiriki kabisa katika Kombe la Dunia, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) imeahidi kumlipa stahiki zake alizokuwa anastahili kulipwa endapo angechezesha.

Waamuzi hawajui kiasi halisi cha fedha watakachopokea kwa ajili ya kuchezesha Kombe la Dunia, ambacho huwa kinalipwa baada ya mashindano hayo kumalizika.


Pia, Soma: Mwamuzi Omar Artan aliyenyimwa kuingia Marekani kuchezesha Kombe la Dunia apokelewa kishujaa Somalia
Kumlipa posho zote haisaidii kitu. Lengo lake halijatimia. Yeye alilenga kuwa msomali wa kwanza kuchezesha mechi kwenye kombe la dunia lakini ndoto yake ikazimwa na serikali ya kiqumer ya Trump.
 
Lakini bado FIFA wapo juu ya hilo, wangeweza kubadilisha vituo vya marefa.
Kumbuka marefa wameingia mkataba wa kazi. Haiwezekan maamuzi ya kijinga ya marekani yakawafanya wabadili ratiba zao.


Samia anaongoza vichaa.
 
Kumlipa posho zote haisaidii kitu. Lengo lake halijatimia. Yeye alilenga kuwa msomali wa kwanza kuchezesha mechi kwenye kombe la dunia lakini ndoto yake ikazimwa na serikali ya kiqumer ya Trump.
Amekaribishwa kuchezesha zinazochezwa Canada, Ila hii ilikuwa n ombi kutoka Canada, sijamjua upande wa jamaa, hvy lengo lipo pale pale. Fatilia.
 
Kumbuka marefa wameingia mkataba wa kazi. Haiwezekan maamuzi ya kijinga ya marekani yakawafanya wabadili ratiba zao.


Samia anaongoza vichaa.
Huwezi kusema maaumuzi ya kijinga ya Marekani. Kuingia nchi ya watu ni wenye nchi watake na hakuna mtu wa kuhoji. Hata hapa Tanzania watu wengi tu walishazuiwa mipakani kuingia nchini.Kama ungekuwa msafiri sana wa nje ungelijua hili ni la kawaida maelfu ya watu hurudishiwa airport tena wakiwa na Visa mkononi, na ndio sababu ya kutakiwa kuwa na return ticket ya huko uendako . Na Somalia tayari ilikuwa kwenye nchi ambazo Marekani iliwaweka kwenye blacklist ya raia wake kuingia Marekani, halafu bado FIFA ikampangia kituo cha Marekani
 
Back
Top Bottom